Tuyuku
JF-Expert Member
- Jan 6, 2011
- 3,292
- 1,919
Tatizo watu hamsomi historia wala kufuatilia mambo halafu mnang'ang'ania kuwaambia watu haya mambo yanafanyika kwa mara ya kwanza. Kikwete hana la maana kabisa.
Mwalimu alifanya maamuzi mengi mazito ikiwa ni pamoja na kumruhusu Mwinyi aliyekuwa akimpenda sana ajiuzulu japo hakuwa na makosa yeye kama yeye isipokuwa watu wa chini yake. Mwalimu alisimamia rais wa Zanzibar ajiuzulu alipokwenda kinyume na katiba....na mengine mengi.
Tukija kwa Mwinyi, pamoja na upole wake wote, mwaka 1994 mwishoni hakuona taabu kulivunja baraza la mawaziri na kumpiga chini waziri mkuu Malecela na katibu mkuu wa CCM hayati Kolimba alipoona mambo yanakwenda kombo kutokana na ushauri wao mbovu.
Tukija kwa Mkapa, alimfungulia mashitaka ya ufisadi waziri wa zamani wa ujenzi Nalaila Kiula. Alifanya maamuzi makubwa sana kuunda TRA ili kodi zetu zikusanywe kwa jitihada zote. Alikubali na kuwashinikiza maswahiba wake wajiuzulu, kama waziri wa fedha Prof Mbilinyi, Mporogomyi. Na pia waziri wa biashara Idd Simba. Na hata Simba alipoleta siasa za ukaburu za uzawa Mkapa hakuona haya kuzipinga bayana. Mkapa akafanya maamuzi makubwa zaidi kuanzisha mfuko wa barabara baada ya kuona wafadhili wanaleta nyodo kusaidia kujenga barabara. Akafanya maamuzi magumu kuamua majengo ya Chimwaga yapewe serikali ianzishe Udom ila nashangaa sana hizo compliments anapewa popo. Akafanya maamuzi makubwa sana ya kujenga uwanja wa mpira ingawa yeye si mwanamichezo. Akafanya maamuzi makubwa sana ya kujenga uwanja wa kimataifa kule Mbeya mfupa ulioishinda serikali toka miaka ya 70. Mkapa pamoja na ufisadi wake alifanya kazi inayoonekana. Na ujasiri wake mkubwa ni kudhibiti mfumuko wa bei kwa miaka kumi jambo ambalo hakuna rais wa Tanzania kawahi kuweza kulifanya.
Mkapa akafanya ujasiri mwingine kuwanyang'anya Tanesco (tena bora kabisa ma...fa...la sana hawa) majengo yao na kuwapa waislamu waanzishe nao chuo kikuu.
Mie nawashangaa sana mnaomsifia mtu ambaye uamuzi wake wa kijasiri ni kukesha angani kama popo, kuyafahamu majina ya mafisadi na wauza unga na kuyakalia chumbani na mkewe na watoto wake.