Nashangaa hadi sasa wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa wilaya za Morogoro bado wako kazini

The Assassin

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
4,355
17,321
Kwa watu tunaofuatilia siasa na matukio yanayotokea nchi hii tunafahamu kua waziri mkuu alifanya ziara ya kikazi kwa siku 4 mkoani Morogoro, na kila wilaya alioenda kulikua na ubadhirifu wa pesa usio na kipimo. Watu wanakula hela za serikali kama vile ni pesa zao binafsi. Waziri mkuu alikua hadi na majina ya hao watumishi na kuyasoma hadharani.

Kwa serikali hii inayojinasibu kupambana na ufisadi hata wa kiwango kidogo kabisa, nashangaa kuona bado inawaacha ofisini maafisa madhuhuri(accounting officers) kama wakurugenzi, mhazini wa wilaya na wakuu wa vitengo.

Mbaya zaidi kila wilaya kuna mkuu wa takukuru, mkuu wa polisi na mkuu wa usalama wa taifa na watu wao, wakati hizi rushwa na wizi wa mali ya umma unatokea wao walikua wapi na kwa nini hadi sass bado wako kazini.

Kwa kweli nashangaa kuona bado hao jamaa wako kazini hadi sasa.
 
Mkuu unafikiri kama sio kazi nzur ya TISS na takukuru Waziri Mkuu angejuwa yote hayo?
Nimekuelewa Sana
Nadhani Hao Waliwasilisha Kwa Waziri Mkuu Halafu Kwa Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
 
Hiv mnafikir teeth ni malaika kutoka mbinguni kwamba hawatendi maovu, hawali rushwa hawa.....? Mnajidanganya
 
Wazir alienda kule strategically , hakujiendea tuu , mchongo mzima alipewa before, na Mzee Baba huenda alikuwa anajua what is going on, na huenda hao hao wahasibu ndo walitoa taarifa kuwa wakubwa wao wanakula sahani moja na waharifu...... Pia huwez kuondoa system yote at once , damage itakuwa kubwa zaidi, istoshe rushwa na ufisadi, ni matatizo endelevu hayawez kuisha unapambana nayo tu to the last
 
Nchi yanuka ufisadi. Wa Jumba jeupe anajichotea mihela pale kwa mpwawe, mara 1.6 trill, Mara 2.4 trill. Ununuzi wa midege, Ujenzi wa Chato International Airport; havikufuata taratibu za nchi lakini vinasifiwa pamoja na mengine mengi .....ya zamani na mapya. Watu na hasa wateuliwa wake, wanamuona ( mzalendo namba 1), nao wanachota japo kidogo mezani kwao.
POLISI,TISS na hao TAKUKURU pamoja na kuwatumia kuiba kura, kudukua maongezi ya watu, kunyanyasa maadui WAO na kutisha wananchi, nao vilevile wanaisoma namba. Ni wanadamu kama wewe na yeye, wana njaa.
Nyerere aliwahi kusema " .....maji yaliyo kwenye ndoo, na yaliyobaki ziwani/mtoni ni yaleyale......"
Kaunda nae alituasa kuwa hakuna uongozi usiotegemea au kufanana na aliye juu yao. Penye punda pale juu , wa chini nao watakuwa wakipundapunda tu.

Usafi ukianzia juu , utafanikiwa na utadumu. Mchawi kamwe hawezi kupambana na uchawi.

Hayo mapambio na kutajataja majina yake yote ni kelele za kuwasaidia wapambe kujaza matumbo. Amen.
 
Hao wote ni makada wa ccm! Sasa tangu lini ccm ikatenganishwa na wizi na ufisadi ndani ya nchi hii! Ccm ni ukoo wa panya!
 
Hao ni ccm kindakidanki wezi wao,mafisadi wao,yani ukoo wa panya uwizi ndio ilani ya chama chao
Kwa watu tunaofuatilia siasa na matukio yanayotokea nchi hii tunafahamu kua waziri mkuu alifanya ziara ya kikazi kwa siku 4 mkoani Morogoro, na kila wilaya alioenda kulikua na ubadhirifu wa pesa usio na kipimo. Watu wanakula hela za serikali kama vile ni pesa zao binafsi. Waziri mkuu alikua hadi na majina ya hao watumishi na kuyasoma hadharani.

Kwa serikali hii inayojinasibu kupambana na ufisadi hata wa kiwango kidogo kabisa, nashangaa kuona bado inawaacha ofisini maafisa madhuhuri(accounting officers) kama wakurugenzi, mhazini wa wilaya na wakuu wa vitengo.

Mbaya zaidi kila wilaya kuna mkuu wa takukuru, mkuu wa polisi na mkuu wa usalama wa taifa na watu wao, wakati hizi rushwa na wizi wa mali ya umma unatokea wao walikua wapi na kwa nini hadi sass bado wako kazini.

Kwa kweli nashangaa kuona bado hao jamaa wako kazini hadi sasa.
 
Ubadhirifu ni hulka ila tusaidiane kwa mifumo ambayo itadhibiti hizo hulka. Mifumo hutengenezwa kwa kutunga sharia. Hii ni kazi ya Bunge.
 
Back
Top Bottom