Nashangaa hadi sasa Serikali iko kimya kuhusu ajira za Walimu wa Sayansi

Abuwhythum

JF-Expert Member
Jan 7, 2015
837
495
Serikali iliahidi kuajiri watu katika kada ya elimu (Walimu wa sayansi na Mafundi sanifu wa maabara) mwezi wa tatu, wengi tulijua hizo ajira zitatangazwa mwishoni mwa FEBRUARI ili MACHI watu wawasili katika vituo watakavyokuwa wamepangiwa, cha kushangaza Februari yote ilipita kimya wala hakuna maelezo yoyote yaliyotolewa kwa ufafanuzi.
Machi nayo imebakiza takriban wiki 1, ukimya bado umetawala hadi sasa!
Fafanueni basi ili lifahamike moja kama mlivyofafanua kwa walimu wa sanaa, ahadi zisizo na ukweli ndani yake (uongo) zimetuchosha
 
Serikali imetutaka tutumie mitandao ya kijamii katika kuishauri na kujadili mambo yatakayo tuwezesha kupata mchicha, ugali, nguo, ada za watoto n.k. Mambo yenyewe ndo haya, hebu tufanyie hivyo sasa tuone mrejesho nyuma (feedback) unakuwaje!
 
Fungua tovuti ya utumishi usome ndugu!! Walimu mnaambiwa tumeni maombi na vyeti hamtaki na waliotuma ni wachache na hao wachache waliotuma wengine vyeti vyao vina walakini si halali.

Vuta subira tu kama ajira yako IPO IPO tu
 
Hakunaga kitu kirefu na kifupi kama muda. 2020 tunasubiri kupewa ahadi tena na wasichokijua ni kuwa wasaka kazi watakuwa wameongezeka mara 4 kwa maana ndani ya hii miaka minne iliyobaki vyuo vitakuwa vinaendelea na production.
Story zao ni uhakiki na zoezi kwa bahati nzuri lishakamilika na waliobainika tayari wameondolewa. Kwa sasa ni matamshi ambayo kila mtu hawezi kuyaamini. Hakuna anayeongelea suala la ajiri, waziri mwenye dhamani ni kama anasita kutoa tamko maana aelewi na yeye serikali yake inaendeshwaje. Vipaumbele vya bajeti havijaguswa kwa sehemu kubwa.
Nii'kama Tanesco wamekata umeme, kila kiliahadiwa imebaki story. Picha ya kitaifa ni Makonda na namna rais anavyohaha kumkinga dhidi ya maovu yake kwa kada zingine. In short tumepatwa na seikali, bora kina Kikwete walikuwa wanajieleza tunawaelewa. Hapa kazi tu inatuchanganya. Hatuelewi na hatujielewi. Watumishi wana hali mbaya kimaisha. Vitu vimepanda bei mara kadhaa lakini serikali kimya. Hata ile nyongeza ya kila mwaka sasa pia mgogoro.
 
Mods wamebadili baadhi ya maneno kwenye post mama (ya mwanzo)
Hasa heading
 
Fungua tovuti ya utumishi usome ndugu!! Walimu mnaambiwa tumeni maombi na vyeti hamtaki na waliotuma ni wachache na hao wachache waliotuma wengine vyeti vyao vina walakini si halali.

Vuta subira tu kama ajira yako IPO IPO tu
Mbona hamna tangazo kama hilo!
 
mkuu usiitegemee hii serikali ya sizonje tena angalia sehemu nyingine za kufanya kazi

Nina ndugu zangu wamesoma education wengi wameenda private wengine wameena ad Kenya maana bongo amna ishu
 
Seikali yote iko busy kumlinda Daudi Albert Bashite anayejiita Paul Makonda hivyo hawana muda na hao walimu wa sayansi!
 
Back
Top Bottom