aka2030
JF-Expert Member
- Jan 5, 2013
- 2,630
- 3,578
Hakika album yako imesheheni sana madini ambayo kwa kipindi hiki ni ngumu kuyapata kwa wanamuziki wengne
Nmpenda pia ubunifu wako wa njia ya usambazaji wa watu kulipia kwanza mwezi mmoja kabla kwani kwa njia hiyo hata sasa watu wakisambaziana nyimbo zao angalau jasho lako utakuwa umelifaidi
Nimependa pia bei ya album 7000 si kubwa ambayo kila mtu ambaye anapenda muziki anaimudu
Nimependa kusikia baadhi ya wanamuziki wakubwa kama jay dee na fatma kwenye album yako
Nmependa kusikia uchambuzi mzuri wa lugha na fasihi ya kweli kwenye nyimbo zako
Nimependa jinsi ulivyogusa nyanja mbalimbali ya jamii kama maradhi, elimu,uchumi,siasa, na sanaaa huku ukiwa na nyimbo yenye ujumbe mzito wa makamanda wetu walinda nchi <barua kutoka bangui>
Mwisho my best song ambayo hakika umenikumbusha mbali ni Salaam za Amani
Nyimbo ni nzuri ila zingne biti zipo oldschool sana pamoja na chorus mda mwngne hilo hebu lifanyie kazi