Nash MC hakika album yako ya Diwani Y Maalim umekata kiu ya wengi

Mmmh wabongo bwana kwa kujifanya much know!! Kwa iyo wewe unaifahamu hip hop kuliko Nash Maalimu! Sijui umenielewa au nirudi nimelewa?
Ukipeleka ngoma kama ni hiphop basi utaulizwa umetaoka mkoa gani
Kama ni bongofleva utaulizwa umetoka nyumba gani (nash mc maneno)
Hiphop najua tangu kusaga hajaaanzisha mawingu sio dar sio arusha.Huyo maalumu alikuwa anafika kilingeni sua kuongeza uelewa wa hiphop ndio akakutama na wajuba ndio akaandika penalty ya mwisho
Unavyo sema wabongo wewe ni mkongo?,acha uphala.
 
Tustick kwenye hiphop mkuu,nash anafanya hiphop ya kishamba sio kwamba anarap content ndio maana wabongo hawamsikilizi nyimbo kama zima,homa imenizidia na asiyehisika na hiphop atoke zina content gani?.
Nash hagusi hata robo ya bonta maarifa alafu sikwamba anabaniwa na media ni kwamba hana good conscious rap song ya ku offer kwenye hiphop industry amebaki kujisifia tu mtaani.
We jamaa usitake kufanya kila mtu achane ww unavyotaka.sasa kila mc akianza kurap matrap yenu sijui ndo new school unadhani itakuaje.ndomana wapo rappers wenu wa new skuli zenu na wapo wa oldskuli na tupo pia mashabiki wa mcs dizaini ya kina nash.unatolea mfano wa ngoma kama zima,homa imenizidia kua hazina content,kwahiyo ngoma zake zipo hivyo?
 
Kuna challenge katika distribution model ya kazi za albamu. Hapa naona kuna fursa ya kuwasaidia wasanii wetu upande wa kuuza kazi zao. Kukua kwa ICT kumefanya soko la albamu likafa, maana hakuna ambaye alikuwa ananunua CD wala kaseti tena. Sasa hii mfumo wa kuuza kwa kutegemea Whatsapp wenyewe nao ni mgumu. Ndo maana sasa hivi watu wana rely kwenye streaming zaidi. Lakini hakuna mfumo wa streaming ambao ni rafiki kwa wasanii wa kibongo. Lakini ipo fursa ya wasanii kufaidika na kazi zao iwapo tutakuja na mfumo bora wa streaming au kununua kazi online.

Yafuatayo ni baadhi ya mapungufu kwenye mfumo anaoutumia Maalim Nash. Mahesabu yake ya kuuza albamu kwa shilingi 7000 mpaka 10,000 yatamfanya asipate wanunuzi wengi kwa sababu zifuatazo. Tuangalie demography ya mashabiki wake. Je amezingatia uwezo wao wa kulipa? Bei anayouza anaweza akauza mfano kwa watu 1000. Lakini angeuza kwa bei ya chini zaidi, angepata watu wengi zaidi (economies of scale). Kwa analysis ya haraka, mashabiki wa Nash EMcee huwezi kuwakuta Mbezi Beach au Kimara. Wengi watakuwa mitaaa ya Temeke zaidi. Je amelifikiria suala hilo? Market segmentation ni muhimu sana.

Kitu cha pili ambacho hakipo sawa ni mode ya distribution yake ina gap kubwa na mode ya payment (decoupled). Hivi vitu vinatakiwa viwe ndani ya mfumo mmoja. Kitu kingine anachokosea ni yeye kuonekana anafanya kila kitu, mfano marketing, kuimba, n.k. Kazi zingine inabidi zifanywe na menejimenti. Kama msanii unatakiwa uweke focus kwenye kutengeneza kazi halafu uwe na timu nzuri inayokusimamia...
 
Kwanza lazima kumpongeza Nash MC kwa kutoa album licha ya mazingira kuwa magumu kwa wasanii wa TZ na majority wamegoma kutoa album pia pongezi kwa kutoa moja ya album bora kwenye kizazi cha sasa

Sidhani kama bei ya 10,000($4.3) kwa album ni kubwa ukilinganisha na content iliyopo kwenye album (20 +3 bonus track ) ni sawa na 500 per track.Uki-calculate cost za production za album ambayo ameitumia

Kwa music wa TZ ni wasanii wachache sana wenye uwezo wa kuwalipa management ya kuwasimamia kazi zao na bado tunalalamika bei ya album ni kubwa sijui hiyo hela ya kuwalipa itatoka wapi
 
Hawa jamaa kama watajipanga vizuri soko la albam linalipa vizuri sana wanatoboa kwa ushauri tu jamaa wangeongea na basata wapate hati miliki ya kazi zao hii itafanya kuwabana wamiliki wa blog zote bongo wasisambaze nyimbo zao hii ingesaidia sana

Kweli kabisa, hawa jamaa wanatengeneza njia kwa madogo wanaokuja, cha ajabu watu wanawaponda tena!! Yani nashindwa kuelewa tufanyeje sasa? Maana hawa wasipoforce kuleta album sokini nani ataleta. Kwanini tusikubali kwamba wanafanya mapinduzi kubadili mtazamo wa kwamba hip hop haiuzi
 
[/QUOTE
mashabiki wa bongo fleva wanaponda wanazani mziki wa bongo fleva ndo unaolipa kumbe mabosi wa wasanii ndio wanaonufaika na sio wasanii
 
Hiphop anayo fanya Nash na lunduno tukimtoa unju ni ya kizamani sana ilishafanywa miaka ya 90 Arusha ndio maana wakifikaga sua wanachorwa tuu.Abadilike afanye swagah kidogo na content.
Wewe ni wale vijana wanaovaa suruali za kubana chini za kike..haya mambo ya kina Nash MC huyawezi kaa kimya😬
 
Kwanza lazima kumpongeza Nash MC kwa kutoa album licha ya mazingira kuwa magumu kwa wasanii wa TZ na majority wamegoma kutoa album pia pongezi kwa kutoa moja ya album bora kwenye kizazi cha sasa

Sidhani kama bei ya 10,000($4.3) kwa album ni kubwa ukilinganisha na content iliyopo kwenye album (20 +3 bonus track ) ni sawa na 500 per track.Uki-calculate cost za production za album ambayo ameitumia

Kwa music wa TZ ni wasanii wachache sana wenye uwezo wa kuwalipa management ya kuwasimamia kazi zao na bado tunalalamika bei ya album ni kubwa sijui hiyo hela ya kuwalipa itatoka wapi
Nadhani sijaeleweka mkuu hasa kwenye market segments. Nimezungumzia mashabiki wa Nash wapo wapi. Nimezungumzia suala la economies of scale. Unaweza uza kitu kwa elfu kumi wakaishia kununua watu elfu 1000. Lakini ungeuza pengine kwa elfu tatu wangenunuua watu laki moja. Hiyo ndo maana ya economies of scale. Suala la pili ni distribution strategy. Unapokuwa na product unaiuza online , hatua ya kwanza huwa ni kuwashawishi watu kununua, kupitia mbinu mbali mbali. Then utapeleka watu katika kufanya maamuzi ambapo inatakiwa njia yakununua iwe rahisi na kiwango kiwe kidogo mpaka mtu asighairi katikati. Njia ya manunuzi ikiwa ndefu na sio intuitive inawafanya wananuzi wengi waishie kusema nitanunua. Lengo langu nilikuwa ni kuangalia nini kinaweza kufanyika kuwasaidia wasanaiii kama Nash EMc kudistribute kazi zao kwa urahisi kupitia teknolojia
 
Serious unataka hii album iuzwe Tshs 3000 so 10,000 ni expensive ?

Kila mtu anapenda fleva tofauti,mbona souljer boy amechokwa na swaga zake mpya na Kendrick Lamar anafanya hip hop kama zamani na ana tuzo nyingi,tatizo wabongo hampendi mziki wa kufikirisha ubongo mnapenda beat(mdundo) na swaga zisizo na maana.
Kweli ndugu vijana wa sasa wengi wavivu wa kufikiria hawataki kuumiza ubongo sasa shida huu uvivu unaenda mbali zaid hadi kwenye uvivu wa kazi,kushindia chipsi,kukosa nguvu za kiume nk. Kwanza wengi hawajui mziki wanasikiliza beats tu hata ukirudia maneno yaliyopo kwenye wimbo atakuuliza nan kaimba hivyo
 
Kila mtu anapenda fleva tofauti,mbona souljer boy amechokwa na swaga zake mpya na Kendrick Lamar anafanya hip hop kama zamani na ana tuzo nyingi,tatizo wabongo hampendi mziki wa kufikirisha ubongo mnapenda beat(mdundo) na swaga zisizo na maana.
Hapa umenena!
 
Mkuu Mansuli alishakwama tangu nimemsikia 2006 hivi na bado yuko kwenye mziki na hasikiki,yeye ni kama block 41 kina kalapina ambao hawasikiki,Mbona Nash anazungumzia mambo ya sasa ,ni media tu zinaangalia kick,ila Nash kazungumzia vitu vingi vya sasa,...sema tu akili za watu wengi sasa hivi bongo hawasikilizi vitu vya maana zaidi ya inama,nyege nyegezi
Najuta kwanini sikuisoma hii komenti mapema iliyojaa ukweli usiopendwa kusikika masikioni mwa wengi...
 
Tustick kwenye hiphop mkuu,nash anafanya hiphop ya kishamba sio kwamba anarap content ndio maana wabongo hawamsikilizi nyimbo kama zima,homa imenizidia na asiyehisika na hiphop atoke zina content gani?.
Nash hagusi hata robo ya bonta maarifa alafu sikwamba anabaniwa na media ni kwamba hana good conscious rap song ya ku offer kwenye hiphop industry amebaki kujisifia tu mtaani.

Ile ngoma ya Zima ilikua ni darsa kwa wote wanaozingua kwenye maswala ya mziki

ZIMA haina content??

Dj unataka hela aisee sina, kwenye kipindi chako wimbo wangu zima/

Hata redio yenu kucheza kazi zangu wala sio lazima/

Hapa nash alikua anazungumzia madj wala rushwa ambao bila hongo hawapigi nyimbo zake, anamaanisha kua yeye hana hela ya kutoa kukupa wewe kama imeshindikana kupiga basi achana nayo

"Oya nanii p the mc washa tv, bunge lakatiba! Hua siangalii zima"

Pia kagusia na siasa kidogo hususani bunge, bunge la siku hizi limepoteza umakini unakuta wabunge wanatukanana hakuna hoja za msingi mfano yule msukuma alishawahi kusema anaiomba serikali itoe ile sanamu ya posta waweke sanamu ya diamind maana anaiwakilisha nchi pamoja na kuitangaza.

"Watangazaji wanaigana amanene, dzaini kama, ushoga mtupu vipindi vya mchana sisikilizi zima"

Hapa hakuna haja hata ya kueleza nadhani hili linaeleweka vyema, juzi nimesikiliza redio nikasikia mtangazaji kila baada ya maeno mawili anasema upepo wa kisuli suli

"Mpigie kura msanii unayemtaka kwenye tuzo za kili, tangazo kama hili hakuna cha kusubiri ZIMAAA baba unasemaje ZIMAAA"

hapa ujumbe huu ni maalumu kwa wadhamini wa hii tuzo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom