Nasema kwa hasira, kila chama cha siasa kina maslahi yake binafsi. Nchi imejawa na uchama na usiasa

Heavy User

JF-Expert Member
Feb 2, 2020
954
1,732
Roho inaniuma sana ninapoona TZ ina wasomi wengi wenye maneno mengi wanaojua kila kitu lakini nchi yetu bado masikini inategemea kuombaomba. Rais kazungukwa na wasomi na washauri wazuri lakini shida zilizotakiwa kutatuliwa miaka mingi iliyopita bado zipo na hazionekani kuisha leo wala kesho.

Shida zote hizi ni kwasababu ya FIKRA ZA KIZEE zinaonekana ni ujanja ukizizungumza mbele za watu, fikra zenyewe ni uchama, usiasa na kusifusifu watu.

Vyama pinzani vinaonekana kuwa na uchungu wa hali mbaya ya nchi, lakini nao ni walewale tu, wakipewa nchi watatanguliza maslahi yao kuliko maendeleo ya nchi.

Vyama pinzani ni masikini, vikipewa nchi vitajineemesha kwanza. Vyama pinzani mkitaka tuwape nchi hakikisheni chama chenu kimojawapo kimekuwa tajiri. La sivyo msahau.

Na mnaopiga makelele mitaani na kwenye social media kwa mawazo mengi mazuri na kukosoa, na ninyi ni walewale, mkipewa hata kacheo kadogo tu mtatanguliza maslahi yenu binafsi.

ROHO INANIUMA SANA
 
Ndivyo ilivyo mkuu, siasa ni kazi kama kazi zingine, Kila mmoja anavutia kwake ili mradi wanaomtegemea pamoja na yeye wapate chochote mkono uende kinywani, wajilimbikizie na Mali.

Japo angalau wananchi tunaanza kuamka, ila safari Bado ni ndefu kutokana na aina ya wanasiasa tulionao, mwanasiasa akiwa hajala keki ya Taifa anakuwa mwingine, akishaonja keki anakuwa mwingine.
 
Back
Top Bottom