Nasaha zangu kwa akina dada wa vyuo vikuu vya nchini, wakati vinapoelekea kufunguliwa

CR wa PROB

Senior Member
Sep 21, 2011
170
29
Awali ya yote nipende kuwapongeza dada zangu kwa kuwa na mwamko wa Elimu!!

Pili nichukue fursa hii kuwaomba dada zangu kuwa wakati tunapoelekea kufungua vyuo tunaomba muache kuvaa nusu Uchi!!! kiukweli mimi kwa nafsi yangu huwa nakereka sana pindi ninapomwona msomi wa chuo kikuu amevaa nguo ambayozo hazina mfano wa uigwa na jamii inayotuzunguka, Nijuavyo mimi msomi anatakiwa awe ni kielelezo bora cha maadili kwa jamii inayotuzunguka lakini kwa bahati mbaya kwa sasa akina dada wengi hilo swala wamelitupilia mbali na hadi jamii inayotuzunguka pindi waonapo mdada kavaa nguo fupi au suruali inayombana sana huwa wanasema huyu ni MWANACHUO, Hivyo basi hata kama nchi yetu ina uhuru wa mavazi naombeni muweze kujirekebisha ili wadogo zetu waweze kuiga kwenu!!

Naomba kuwasilisha!!!

Mungu ibariki Africa, Mungu ibariki Tanzania na Mungu wabariki akina dada wa vyuo vikuu waweze kuwa na mavazi ya heshima!!!
 
Hebu tuweni wakweli....Inakera, ila ni inaburudisha macho ehh?

Kwani wakivaa inakuuma nini? Acha kumwangalia kama inakukera. Acheni kuhukumu, kwani lazima jamii iige unachofanya?

Kila mtu ana style zake za kuishi, kama haumlishi na hakuadhiri mwache, yamkute ndio ataona mabaya yake.
 
hebu tuweni wakweli....inakera, ila ni inaburudisha macho ehh?

Kwani wakivaa inakuuma nini? Acha kumwangalia kama inakukera. Acheni kuhukumu, kwani lazima jamii iige unachofanya?

Kila mtu ana style zake za kuishi, kama haumlishi na hakuadhiri mwache, yamkute ndio ataona mabaya yake.

asiye funzwa na mamaye atafunzwa na ulimwengu.
 
We nae acha kutuharibia fahari ya macho yetu, au unataka watu wote tuwe tunapiga 'pull' kama wewe? Waache watembee hata uchi kabisa.
 
..Haya yote yatapita..i wish wangetembea Uchi Kabisa!!...Kwa sababu Pilipili usiyoila...
..Nadhani tuzilazimishe akili zetu kuamini hawa tunaopishana nao njiani ni wanaume wenzetu tu..
 
hahaaa haaaaa bahati mbaya wengi hawajui na wala hawataiona hii thread yako...
 
We nae acha kutuharibia fahari ya macho ye2,au unataka wa2 wote 2we 2napga pull kama wewe?waache watembee hata uchi kabisa.


kaka umeona ngumu kuandika tu umeamua kutumia 2? Wengine humu ni wazee wa miaka ya 60 hawakusomi mkuu
 
Mmmmmhhhhh!!

Ni kweli huwa yanakera, lakini pia huwa yanapunguza msongo wa mawazo wakati fulani!!!
 
Na hv bumu limepanda cant imagne vijana wa sosho kule udom watakavyokuwa wanavaa vibana mwili!
 
ninyi mnao shabikia wakina dada waendelee kuvaa nusu uchi mbona mnataka kuleta mabishano yasiyokuwa namsingi mkizingatia ninyi ni wasomi? ? ? Basi na ninyi vaeni nusu uchi ili mfurahishaneni macho na hao kinadada, vaeni hata na hvo vimini vyao ili iwe bomba!
 
kweli ulosema mwenye thread! Inabidi kuwakemea na kuwakumbusha pia maana siku ya mwisho tutaulizwa na Muumba kwanini hatukuwakemea hivyo kuhukumiwa kwa makosa yao pia! Tusichoke wandugu
 
ninyi mnao shabikia wakina dada waendelee kuvaa nusu uchi mbona mnataka kuleta mabishano yasiyokuwa namsingi mkizingatia ninyi ni wasomi? ? ? Basi na ninyi vaeni nusu uchi ili mfurahishaneni macho na hao kinadada, vaeni hata na hvo vimini vyao ili iwe bomba!

tehtehtehteh, mkuu umenfurahisha xna, tehteh.. cpat pcha senetor anapita pale cafeteria 2 na kimini chake... dh hii kal
 
Back
Top Bottom