Nasaha za Nicolas Jovine Clinton kwa Vijana wa NCCR-MAGEUZI

Dr Shekilango

Senior Member
Dec 30, 2013
192
117
MISINGI YA UTU YA NCCR-MAGEUZI

"PAMOJA TUTASHINDA"

SALAAM ZA KAIMU MWENYEKITI WA KITENGO CHA VIJANA WA NCCR-MAGEUZI TAIFA.

Ndugu; Nicolas Jovine Clinton.

Nawasalim sana Vijana wote Nchini ambao mnaendelea kujiunga na NCCR-MAGEUZI na wengine tiari mmejiunga na Chama chetu katika maeneo yote Nchini.

Naendelea kuwakaribisha na kuwatia moyo kwa pamoja mje tujenge chama chetu na Muhimu sana zaidi ni Taifa letu yaani Mama Tanzania.

Hali ya chama chetu ina mazingira wezeshi kwa sasa na ni salama kwa vijana wa kiume na wa kike wote, wale mliyo na vyama na wale msiyo kuwa na vyama, NCCR-MAGEUZI ni jukwaa muhimu na mahali salama pa kujenga Taifa letu katika Misingi ya UTU ambayo ni;

*Udugu
*Maadili
*Usawa
*Haki
*Imani
*Mabadiliko
*Uhuru
*Wajibu
*Asili
*Kazi na
*Endelezo.

Misingi hii ya UTU ndo inakiunda chama chetu katika nyanja zote za Maisha. Kwa hiyo wewe kijana ambaye unajiunga leo, umejiunga jana na utajiunga na sisi NCCR-MAGEUZI ni sehemu sahihi katika mazingira ya siasa za sasa na muda wetu huu kama Vijana.

NCCR-MAGEUZI sisi ni ndugu na binadamu wote ni Ndugu zetu na Afrika ni moja, sisi sote tunaunganishwa na Itikadi moja tu ya UTU, kabla ya mambo yote Duniani au binadamu anafanya jambo la msingi ni UTU.

Vijana tunawajibu wa kuendeleza mazuri na mema ambayo yaliachwa na wasisi wa Taifa letu yaani Mama Tanzania. Jukumu hili ni langu na wewe ili kufikia hatua ya maendeleo kama Taifa kuliko tulivyo leo.

Jukumu letu pia kama Vijana katika Nchi yetu siyo kuwatukana watu na kutweza UTU wao kama binadamu mahali popote pale mitandaoni na katika jamii yetu, narudia kusema sisi sote ni Ndugu. Na hivyo Vijana wetu hakuna maana kuwatukana watu au washindani wetu kisiasa tujenge nao Hoja bila Matusi, na kutweza UTU wao, kazi yetu ni kujenga chama na Taifa kwa ujuzi wetu na Maarifa yetu ili kuwaandalia mazingira bora kizazi kitakachofuata baada ya sisi. Waheshimu wote na huo ndiyo UTU wetu kama NCCR-MAGEUZI.

Nawasihi Vijana wa NCCR-MAGEUZI na wengine pia tujifunze kuheshimu mawazo na uhuru wa wengine tunapokutana watu wenye Itikadi tofauti tukumbuke jukumu letu ni kujenga Taifa la watu wenye Ujuzi, Maarifa na watu wenye kujijenga katika suala la Technologia na sayansi.

NCCR-MAGEUZI haipo kupambana na Vijana wa chama flani au na chama flani NCCR-MAGEUZI ina Itikadi yake, Sera yake katiba yake, taratibu na miongozo na hivyo sisi tutafanya siasa kwa mjibu wa katiba na sheria za Nchi yetu na siyo kupambana na chama flani, isipokuwa lengo letu au la chama cha siasa ni kushika dola na ili kushika dola Sharti CCM iondoke Madarakani kwa Amani na kutuachia Taifa moja na lenye kuheshimu Uhuru na Umoja wetu.

Siasa za UTU Kiitikadi zituunganishe Vijana kwa pamoja ndani ya chama kimoja NCCR-MAGEUZI na wale mnaojiunga na sisi endeleeni kuja kwa utulivu wa fikira Someni katiba yetu jifunze Itikadi yetu kwa wale ambao hatuwezi kuwafikia kwa wakati mmoja pitieni sera za NCCR-MAGEUZI. Katiba yetu ni bora na imesukwa vyema kuliko chama chochote kile Hapa Nchini kwetu.

Sisi kama Vijana ndani ya NCCR-MAGEUZI tunawasubili tufanye kazi kwa pamoja kama ndugu wa Taifa moja bila fujo, vurugu na matusi dhidi ya watu wengine, Utulivu wa kifikira na amani ya Moyo iwaongoze kujiunga na sisi katika zama za MAGEUZI ya kiuchumi, Demokrasia na Uhuru.

Na hata wale Vijana mliyopo katika taasisi za Elimu ya kati na Juu (Vyuoni) tutawafikia maana nyinyi ni chemchem na cheche za mabadiliko katika Taifa letu.

Kwa pamoja Sisi Vijana tuliyo tiari ndani ya NCCR-MAGEUZI tunawakaribisha nyinyi mliopo nje ya MAGEUZI tuungane pamoja kujenga chama Kimoja, Taifa Moja na Watu wamoja katika Maendeleo ya Taifa.

Pamoja na Salaam za Demokrasia na Maendeleo

UTU ITIKADI YETU.
UTU NGAO YETU.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nachokiona hapa NCCR mtagawana kura na ACT na CHADEMA kwa faida ya CCM if at all mpango wenu ni kuchukua wabunge wanaokimbia CHADEMA na CCM!

Cha kufanya msahau yote ya nyuma muungane, wabunge wa CHADEMA waliokimbilia NCCR waachwe wagombee wapinzani wasisimamishe mtu.

Same to majimbo yaliyo chini ya CHADEMA. Ila kma kila chama kitaingia kivyake mtapoteza wote majimbo ambayo mna uhakika wa kuyabeba.

Nilitegemea Nicholas J Clinton utahamasisha umoja na vyama vingine kumbe ndio kwanza unahamasisha wahame vyama vyao!! Kwa staili hii tutafika kweli?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom