Narudia tena... Tigo mnadharau wateja kwa hili...

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,178
7,319
Nilishawahi kueleza tena hapa, na wachangiaji wengi wakaunga mkono. Nimeshapiga customer service zaidi ya mara tano kuhusu hili tatizo, bila mafanikio...
Can you imagine.... Nina mgonjwa na nataka kuwasiliana na daktari kwa dharura, napiga namba yake ya tigo, mara naanza kusikia ...'Mpendwa mteja, tigo inakupa ofa maalum kupitiga huduma ya tigo extreme, piga *1.....' Yaani wakati nataka nijue nini hatma ya simu yangu ninayopiga nakutana na matangazo ya biashara chungu nzima... nalazimika kusubiri kwa sekunde zaidi ya 30, ndipo nije niambiwe 'namba ya simu unayopiga, haipatikani kwa sasa'!!!
Yaani nimenunua simu kwa hela yangu, nimeweka vocha kwa hela yangu lakini pale ninapotaka kuitumia, naanza kupewa hadithi za vitu ambavyo kwangu sio muhimu kwa wakati ule!!! Is it fair?

Nauliza jamani, Huu ni uungwana? Yaani napiga simu, nina haraka zangu lakini nalazimika kusikiliza kwanza matangazo ya biashara!!!, ni uungwana jamani huu?

Tigo kwa sasa wana majivuno kwa sababu wana wateja wengi. Lakini wasisahau kuwa miaka kadhaa iliyopita airtel nao walikuwa na wateja wengi na wakaanza kuvimba kichwa na kudharau wateja. Waangalie jinsi airtel wanavyoteseka leo...
 
ndugu huduma ya mawasiliano tanzania ni soko huria huyo anazingua unatoa chip(line) unaweka kando unatafuta nyingine ambao kidogo hawana dharau sana maana cdhani kama ipo isiyo kuwa na dharau Tz hii
 
daah pole mkuu, ni kweli wanatulazimisha kusikiliza matangazo yao ya biashara.... terms and conditions applies ndio inawapa kiburi
 
Pole sna pia Wanatuma msg zao za huduma hadi kero,,,

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
ndugu huduma ya mawasiliano tanzania ni soko huria huyo anazingua unatoa chip(line) unaweka kando unatafuta nyingine ambao kidogo hawana dharau sana maana cdhani kama ipo isiyo kuwa na dharau Tz hii

Wengine chip zetu ni maisha yetu(contacts za kikazi) hatuwezi kuzi discard at will!lazima itafutwe solution ya kuwanyoosha hawa.
 
mi naona Tuko we hawakukeri mi nachukia mfano hakuna!halafu hili la kumpigia mtu hapatikani lakini wanakata hela yako!hela zinapotea kwenye tigopesa!
ukifuatilia unaambiwa masaa 24!usubiri!ah
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli wanakera, wasipokusikia safar hii, Jaribu kuwaona TCRA Uone kama ni sawa mteja kulazimishwa jambo ambalo halikuwepo wakat unajiunga nao.
 
its true inakera kweli kweli, Mi nadhani kuna haja ya Serikali na wadau wengine waweke ule mfumo wa mtu kuhamia na namba yako ya simu kwenda mtindao mwingine! kama SA na hata kenya! Tigo ikisumbua unaenda kwa wakala wa voda anasajili namba yako ya tigo baada ya 1 hr namba yako inakuwa katika mtandao wa voda! itaondoa ujinga wote huu
 
Ugonjwa huo unikuta nami mwezi wa saba nilikuwa natumiwa ujumbe kutoka tigo kila baada ya sekunde 30 kwa muda wa siku mbili ikanibidi kufunga simu yangu 2*60*48 sms
 
Wanakera sana hao, tena saa nyingine wanapiga kabisa simu, saa nyingine uko busy na kazi zako unapokea simu ukijua ni ya maana unakutana na matangazo yao!!! Fyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!!! wanaudhi kama nini!!!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom