Narudia tena na tena kwako Rais John Pombe Magufuli

okiwira

JF-Expert Member
Jul 23, 2018
2,787
2,853
IKUTI MBEYA RUNGWE ni sehemu ambayo binadamu na wanyama wanashea sehemu kunywea maji katika mto rumbe.

Kila uchao wanasiasa wanawalaghai wananchi watawaletea mabomba ya maji ili wapite bila kupingwa. Lakini hawaleti.

Je, wewe nawe hii sehemu ya siasa zako? MJOMBA WA HAPA KAZI TU?

Mhe. Rais, Zahanati ya Ikuti mbali na kujengwa chini ya kiwango kama makusudio husika ya Serikali hivi unajua manesi wa zahanati kwa uchache wao baadhi yao mi malaika wakuu.

Muda wote wanahitaji kuabudiwa mwanachi anaona bora akatibiwe Tukuyu na sio Ikuti.

Hivi unatambua mwanachi yampasa afue shuka alilo lalia zahanati pindi alipokuwa anauguzwa?

Mh. Rais wananchi wa Ikuti muda wote wanatamka sehemu yao wengi wanatamka kwa wema.

Je, wajua wananchi wanaiingiizia serikali kuu tsh ngapi na huduma ya barabara ina ubora kiasi gani?

Hivi si unajua barabara ya kuingilia KK kwenda mkoa wa songwe ni barabra kuu kwa sasa?!

KARIBU siku moja

Mara ya mwisho ilitengenezwa alipokuja Wazir Jafo kuangalia zahanati ya Ikuti naamini kabisa alikuta zahanati ina madudu mengi sijui kama alikupa taarifa.

Maana wanachi wenyewe walishikana mashati uwizi wa mabati ya zahanati.

MH RAIS NINA MENGI ILA TIA MGUU WAKO RUNGWE WENDA UKAWA RAISI MBARIKIWA IKUTI asante.
 
Ana I.D usiwe na hofu anasoma hongera sana kashaona hitaji lako inabidi raia wa ikuti wakuchague wewe kuwa mwakilishi wao bungeni maana unajitolea sana
 
Back
Top Bottom