Elice Elly
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 1,268
- 1,593
Upo sahihi Lakini pia hata hao wakubwa wetu wawe wanatumia maneno mazuri na siyo ya kuudhiKwanza naunga mkono hoja ya ukosoaji ,Kukosolewa kwa kiongozi au raia yoyote yule ni jambo linalokubalika kabisa ,na wala halina mjadala wowote.
Kwani kukosoa humfanya yule aliekosolewa kujitathimni utendaji wake au mwenenendo wake,kisha kufanya marekebisho kama ataona kuna umuhimu wa kufanya hivyo,halazimishwi hata kidogo.
Na ukosoaji mzuri,au mkosoaji mzuri ni ule/yule wenye Lugha ya staha na wenye kuweka njia mbadala (way foward),duniani kote wakosoaji hufanya namna hii.
Kumezuka tabia ya baadhi ya watu kupitia mgongo wa siasa, kufanya utovu wa nidhamu kwa kumtusi rais kwa kigezo cha kwamba wanakosoa ,na wakishughulikiwa ipasavyo kwa mujibu wa kanuni na sheria hudai wanaonewa,wanazibwa midomo,si kweli ,kama unatukana utazibwa mdomo tu,utake usitake,Rais ni kiongozi mkuu wa nchi ,ni alama ya taifa ,kumtukana ni kosa la jinai,si jinai tu,inakwenda mbali zaidi ,unapoonyesha utukutu uliokomaa.
Ushauri wangu kwa vijana hasa ndio ambao damu inachemka na mara nyingi ndio lika lenye misukosuko,kama kuna watu wanakutumieni kumtukana rais Magufuli ili mpate umaarufu na chochote kile ,kisha wao kuwatumia kama jukwaa lao kufikia malengo yao , mjichunge sana ,ni hatari kwa future yenu.
Naamini vijana nyie ni wasomi wazuri na mna elimu nzuri ya kukosoa yenye kuonyesha njia mbadala,itumieni ipasavyo sehemu ambayo mnaona haiendi sawa kwa kukosoa kupitia staha na si matusi.
Kumbukeni rais huyu alichaguliwa na watazania wengi,unapomtukana umetukana wale waliomchagua na wale wote wanaokubaliana na kazi yake,hivyo kujikuta wewe unajitengenezea wigo mpana wa maadui.
Badilikeni wakati ni sasa.kuna vijana ambao nawapongeza na ni vizuri mkawaiga,kuna Zitto kabwe,Hussein Bashe,hawa vijana wanaikosoa sana serikali bila ya matusi na huja na way foward,ndivyo inavyotakiwa,vinginevyo kosoaji ya umagharibi si asili yetu,mtaumia tu.