Narudi Dar es Salaam kumpigia kampeni Mtulia. Hakika atalia!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Nimeshaanza safari ya kurejea Dar es Salaam nikitokea Kinampanda, Iramba mkoani Singida. Narejea Dar es Salaam kwa kazi maalum. Kazi ya kampeni bila 'shampeni'. Kampeni za kutangaza machungu ya wanaKinondoni kuanzia asubuhi hadi jioni. Nitampigia kampeni mgombea wetu wa CCM, Ndugu Mtuulia, kwa nguvu zangu zote.

Bila majukwaa wala kukaa, nitawaambia wanaKinondoni jinsi Mtulia asivyo mkweli na wa kumwamini. Nitawaambia wananchi mitaani na majumbani mwao jinsi Mtulia alivyoharibu hata utaratibu wa kichama kwa kutopitishwa kuwa mgombea ipasavyo. Nitawaambia na kuwapa nyaraka zenye baraka kuhusu kilichojiri alfajiri ya yeye kujiengua CUF na kujiunga CCM.

Mtulia, kaa chonjo. Jiandae. Nakuja 'kukuuza' kwa wananchi kwa maneno matamu ya kinidhamu na yatiayo hamu kwa mwanadamu. Nitapiga kampeni ili USICHAGULIWE. Kukuchagua Mtulia ni kuchagua hasara kwa Taifa kupitia Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Ingekuwa nafuu na kueleweka kama usingegombea tena. Ungemuunga mkono Rais nje ya Bunge.

Sitakuwa na mgombea wa kumfagilia Kinondoni. Lakini, nina mgombea wa kumwanika kwa wanaKinondoni ili wakimchagua tena wasije wakachoshwa na kusikitishwa na mchezo wake wa kuhamahama. Mtulia, jiandae. Nakuja kukupigia kampeni za nguvu bila kutumia mabavu wala ukakamavu. Nyaraka zitatosha na kutisha.

Nabii Tito!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (safarini kurejea Dar es Salaam)
 
Una hela ya kwenda ubeligiji?
Kama huna kaa tu kimya ndg yangu zama zimebadilika.
Save my words.
 
Wewe tulia Wakinondoni wanajua kilichowakuta hakuna kujuta ni mwendo kutupa na kuokota mwenyewe...
 
Aliambiwa, kwanza aende kwa Mshana jnr ! Alikwenda? Ona sasa,anaisaidia polisi huko Dodoma!
Jee Kampeni atakuta inamngojea yeye?
 
ila andaa ulinzi mkuu kwa sasa chama cha majambazi kimejiharalishia uharamia kwa kila namna .......... Ni bora uombe ulinzi toka kwa serikali yetu pendwao_O tena sio humu maana humu huwa hawasikii labda wanasikia tu ikiwa unawapaisha :(:(:(:(....sawa mkuu ila chunga sana
 
Huu uchaguzi ni mwepesi sana kwa upinzani kushinda. Sijajua ni nini wanaccm na Mtulia wataambia wapiga kura wa kinondoni.

Hofu yangu ni kwa polic ndio tutakuwa tunapambana nao badala ya ccm.
 
IMG-20180124-WA0004.jpg
 
Back
Top Bottom