Napitia wakati mgumu sana naombeni ushauri na msaada kwa kadri utakavyolipokea linalonisibu

Poleeeh sana mpendwa, jah awe nawe ktk kipindi hiki kigumu.
Akuvushe salama.
 
Poa kaka! Maisha ni changamoto sana! Nimeweza kumcheki msela! Nimechangia pia! Mungu ampe nguvu avuke kwenye hili!
Nashukuru sana kaka kwamsaada wako mchango wako unamaana sana ndugu yangu hasa kwahuyu mama anaenyonyesha halafu anaumwa anahitaji lishe japo sijamuona ingekuwa mambo ya chakula tungesema wapambane nakuomba ndugu yangu nawengine mliojitoa kwaajiri yafamilia hii najua mmefanya hivo kwakuwa namiayo yakutoa kutoa hela kwamtu usiemjua inataka moyo hasa kwadunia hii naomba tuendelee kusaidia kwachochote hakuna kidogo kwenye mazingira haya ukipenda kuwasiliana na mm no yangu iko hapo
 
Nawashukuru wote mliojitoa kumsaidia huyu ndugu mmefanikisha mgonjwa amepata matibabu nimefanikiwa kuonana nae tumezungumza mengi niwatoe wasiwasi juu yahuyu ndugu nimuhitaji kwasasa
Nashauri uzi wake uambatanishwe na namba yake WENGINE sadaka zetu tumeacha kuzipeleka kwenye minada mshenzi ya KANISANI yaani eti kuku anashindanishwa bei mpaka ananunuliwa kwa laki saba huku mtaani kwako kuna mtu hajui atakula nini.?
Pili serikali iangalie hasara zitokanazo na kodi na tozo kwenye kampuni binafsi matokeo yake watu waliokuwa wanategemewa na familia wanarudi mtaani kwa sababu kampuni zina incur loss alafu unalikuta li mwanasiasa linasifia kama mwehu eti KIPATO CHA MTANZANIA KIMEPAA,mara uchumi wa kati ,mara nchi ya uchumi wa viwanda,lingine utasikia linasema eti sector binafsi zimeimarishwa wahitimu wengi wamepata ajira kuliko awamu zote.Yaani kuna mavitu yanaendelea nchini unaweza shika rungu upasue TV kwa hasira.
Kaka mtoa mada nakushauri usikate tamaa hata mimi nilipitia wakati mgumu mimi na mchumba angu tulikuwa watu wa stress mpaka (mchumba enzi hizo)mke wangu akapata vidonda vya tumbo mimi nilikonda uso wangu ulikuwa kama shoka yaani nilikuwa naonekana kama DAZBABA yule wa DAZNUNDAZ (Ila leo MUNGU ni mwema mwonekano wangu unashangaza ukilinganisha na waliokuwa wananijua) in short tulitiana MIMBA na huyu mke wangu(mchumba wangu wa enzi hizo) akafukuzwa kwao tukiwa bado tupo chuoni nilisoma kwa stress mpaka nikachukia chuo anyway kaza usiwe na mda wa kulalamika jitahidi uwe na muda wa kukimbizana na life kuna sehemu utagusa patatick na utashangaa. MUNGU AKUTIE NGUVU MAPITO NI FUNZO TUSIYACHUKIE WALA KUYAOGOPA.KUYACHUKIA NA KUYAOGOPA KUNAYAPA NAFASI ILI YAKUADHIBU IPASAVYO.
 
Nashukuru mkuu hata kwakumtia moyo no ataweka ili walau tumtoe kwenye kuuguliwa
 
Nawashukuru wote mliojitoa kumsaidia huyu ndugu mmefanikisha mgonjwa amepata matibabu nimefanikiwa kuonana nae tumezungumza mengi niwatoe wasiwasi juu yahuyu ndugu nimuhitaji kwasasa
Nimeonana naye jana -jamaa ana uhitaji serious kabisa.
...the good thing yuko imara kiafya na kiakili pia...Mungu mkubwa yatapita.
 
Nimeonana naye jana -jamaa ana uhitaji serious kabisa.
...the good thing yuko imara kiafya na kiakili pia...Mungu mkubwa yatapita.
Nakushukuru ndugu yangu kwamda wako mungu akubariki sana naomba tushirikiane tumtoe hapo alipo nitashukuru mkuu kama nitapata mawasiliano yako ndugu
 
Sijui cm yako ina thaman gani, lakini km ningekuwa mm nipo katika hali hiyo ningeuza cm nipate mtaji wa biashara ya kuuza mahindi ya kuchoma Dar inalipa na mtaji ni mdogo ni kupata sehemu tu hasa mitaa ya watu wengi au barabarani.

Au hata biashara ya kuuza maji ya kufunga (sijui km bado ipo). Kwa kifupi DSM fursa nyingi sana na ukiwa sio mvivu utatok
Nashukuru mkuu kwamoyo huo mm pia nifundi ila kwasasa sina kazi yakueleweka ila kuna mtu alitoa wazo achome mahindi ila tatizo ni mtaji ambao ni kama 60000 niwaombe wadau kama kuna mwenye chochote tufanikishe hili
Wazo la mahindi ni zuri sana,mahindi pale mawasiliano Bei ya jumla Mhindi mmoja ni Tsh 100 ili ukuze mtaji unaweza ukaanza na ya kuchemsha tu.Kwa kujibana hata 30,000 unaanza nayo
 
Wazo la mahindi ni zuri sana,mahindi pale mawasiliano Bei ya jumla Mhindi mmoja ni Tsh 100 ili ukuze mtaji unaweza ukaanza na ya kuchemsha tu.Kwa kujibana hata 30,000 unaanza nayo
Nikweli mkuu ila hata ingekuwa 20000 huyu ndugu hana kuna watu wamejitoa sana kuhangaikia hili ila kwasasa tunajaribu kuangalia matibabu ya huyu mama kama unavojua mtu anaetoka kwenye mambo yauzazi kilichopatikana kimeishia hospitali hata hivo nashukuru kwa wazo lako
 
Mwanaume mwenzangu pole na changamoto, utavuka tu...zaidi ya yote umekuwa wazi kueleza hapa naamini bado kama wanaume tunaweza mtoa mwenzetu sehemu alipo. Nakutia moyo simama imara na hili litapita.
 
Mwanaume mwenzangu pole na changamoto, utavuka tu...zaidi ya yote umekuwa wazi kueleza hapa naamini bado kama wanaume tunaweza mtoa mwenzetu sehemu alipo. Nakutia moyo simama imara na hili litapita.
Nashukuru kwaniaba yake chakufurahisha kiakili yuko viZuri sana hajafikia kuchanganyikiwa tumsaidie ndugu zangu msaada anaohitaji sio mkubwa sana kikubwa nihuyu mama
 
Niko Mbezi hapa Dar nimepanga chumba kimoja nina mke na mtoto mmoja mchanga. Ingawa haukuwa wakati sahihi wa kuishi na mke ila kwakuwa ilitokea akabeba ujauzito na hakuwa na namna nyingine ya kuishi ikabidi tu niishi nae.

Nilikuwa nafanya kazi mahali kwa mtu ambapo nilikuwa nikilipwa kwa mwez ingawa malipo yalikuwa kiduchu sana. Wakati huo mke baada ya kubeba ujauzito alipokuja tuishi wote akawa anajishughulisha na kazi ndogo ndogo za kutembeza mboga za majani.

Baadae nilipokuwa nafanya kazi kulingana na hali ya biashara kuwa mbaya tulipunguzwa baadhi ya wafanyakazi wa pale na mimi nikiwa miongoni mwao. Na ni tangu mwezi wa 1 mwanzon mwaka huu.

Tangu hapo maisha yakaanza kuwa magumu ikanibidi sasa niwe natoka asubuhi nyumbani kwenda huko kutafuta vibarua vya kufanya. Maisha yameendelea hivo hivo kwa kupata na kukosa maana c kila siku utafanikiwa kupata kibarua.

Sasa hivi navyoandika hapa mke wangu anaumwa na mtoto tuliye nae ni mchanga sana na mimi hii inaenda kuisha wiki kila nikitoka sipati kibarua.

Nawaza sana sijui chakufanya ingawa wapo wanaonishauri kuitelekeza familia yangu lkn ni kitu ambacho sifikirii hata kidogo na siwezi kukifanya maana nampenda sana mke wangu na mtoto wetu.

Naombeni ushauri wenu na msaada wenu nifanye nini katika huu wakati mgumu nilionao. Ambao mm naamini ni kipindi kigumu sana nachopitia.

Niko tayari kufanya kazi yoyote ile ilimradi tu iwe halali hata iwe ni kibarua kwa siku kama kuna mahali kunahitajika kibarua mm niko tayari ili tu nihudumie familia yangu.

Sijasoma sana Elimu yangu ni kidato cha nne fairule nina miaka 27.
Nichukue nafasi hii kuwashukuru nyote katika changamoto yangu ngumu sana nayopitia.

Wako baadhi wamenifata inbox na kunisaidia kwa chochote kile walichonacho nawashukuru sana.

Wako pia ambao wamenitia moyo na kunishauri mawazo mazuri nao pia nawashukuru.

Naami wako ambao hata kama hatukuwasiliana nao lkn baada ya kuliona hili huko waliko kwa namna moja ama nyingine wakaguswa na kuniombea kheri nao pia nawashukuru sana.

Wako ambao tumebahatika kuonana nao ana kwa ana na kufahamiana pia nawashukuru.

Kwa pamoja Mungu awabariki sana.

Sikuwa na pesa ya kumpeleka hata mke wangu hospital lakin kupitia walionichangia siku ya jana nilimpeleka na alipata vipimo na matibabu na sasa anaendelea vzr, kwa hilo nawashukuruni sana.

Ingawa bado naendelea kupambana na mengine ya kutoka kwenda kutafuta vibarua ili sasa kupata chochote kwaajili ya familia kula, huku afya ya mke wangu ikiwa inaendelea vzr, naamin haya yote kwa uweza wa Mungu ntayavuka.

Wako watu wamekuwa wakinishauri kuweka no ya Simu hapa hapa kwa yeyote mwenye ushauri, kibarua huko aliko au hata chochote anachowiwa kusaidia ili iwe rahisi. Nimeona ni wazo zuri na mm naiweka hapa hiyo no ambayo tunaweza kuwasiliana. Ambayo ni: 0742843490. Inapatikana na tutawasiliana moja kwa moja.
 
Back
Top Bottom