Napinga uteuzi wa Prof. Sifuni Mchome kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu

Acha ujinga huo...yaani wewe mambo yako ya dhahania huko shuleni kwenu ndo unakuja kutletea hapa wizarani?
hivi wewe kufeli wanafunzi 25 unaona ni maajabu ya mwaka? muulize mulugo takwambia kwenye necta yake wali disco wangapi mwakajana.
hivi kujua kiingereza ndo kigezo cha kuwa katibu mkuu?? acha upuuzi wewe na je kama ni mtaalamu wa kiswahili au kifaransa, kichina na kijerumani?
yaani wewe nakuona kama "green guard" uliyekosa japo ukuu wa wilaya tu ndo unakuja kulia lia hapa.
 
Lukolo

Hakuna mtu anaeteuliwa bila ya yeye mwenyewe kuidhinisha uteuzi huo kabla ya kutangazwa.

Huombwa hata miezi kadhaa kabla yake.

Sasa huyo Professor wenu angesema hataki tu kama anaona huo wadhifa hauwezi, hauwndani nae au hauna tija kwa taifa kama yeye kufanya shughuli nyengine

Hashurutishwi mtu
Ok, tufanye professor aliyekubali kuteuliwa kutoka kitengo cha sheria kwenda kuwa katibu mkuu wizara ya Elimu ni Zezeta. Na je aliyemteua mtu ambaye anajua wazi hana utaalamu na mambo ya elimu na kumpeleka kuwa mtendaji mkuu tumuitaje?

Jifanye wewe Gaijin ndiyo Principal wa chuo, halafu unamteua mwalimu wa hesabu kuwa mkuu wa idara ya Kiingereza. Wewe unakuwa ni nani katika context hiyo? Maana naona kama hiyo sifa ya uzezeta tu itakuwa haikutoshi, labda kichaa kabisa. How on earth unamjua mtu kwamba amesomea ufugaji wa nyuki (unajua kabisa) lakini unamteua kuwa katibu mkuu au msimizi wa kitengo cha ujenzi wa barabara? Kama si utaahira huo ni nini?

Kuhusu mteuliwa nimeshasema awali kwamba kwa mtu kama Professor wa UDSM mwenye lundo la kazi zisizoisha, na mshahara usioridhisha, ukimpa cheo kama hicho atakubali tu maana anaona hiyo ndiyo sehemu yake ya kwenda kupumzika. Na ndiyo maana hii nchi imejaa resources za kutosha lakini ni maskini ya kutupwa. Planners wa masuala ya madini wengi wao wamesoma bachelor of arts in public administration. Anajua nini kuhusu madini huyu?

Yaani kuna wakati mwingine tunafanya mambo kama machizi hivi. Kila mmoja ndani ya nchi anajifanyia anachokitaka, na hakuna wa kumkemea mwenzie kwa kuwa wote wana uchizi unaolingana.
 
Nawe imekuwa hadithi ya kipofu aloona jogoo sasa.

Kitila Mkumbo huyu huyu aloweka model ya kuchagua wabunge wa viti maalum CHADEMA iliyokuwa subjective?

Huyu huyu aloweka model ambayo inatoa a 20% advantage kwa mbunge wa viti maalum aliyekuwa katika Bunge lililotangulia regardless ya utendaji wake kwenye hilo Bunge?

Huyu huyu aliyeweka model ambayo haiwezi kutumika ilivyo zaidi ya Mara moja?

Huyu huyu aliyeweka model inayopendelea elites waliopata elimu ya juu na kufanyakazi kwenye mashirika makubwa katika nchi iliyojaa watu wasio hata na elimu ya msingi? Baada ya Chama kulalama hakuna fursa sawa kwa elimu nchini?

Huyu huyu alokuwepo kwenye Chama cha Demokrasia aliyeridhia uteuzi usio wa kidemokrasia?

Huyu huyu ndio unampigania apewe Wizara ya Elimu?
Nafikiri sasa tunaongea lugha inayofanana, Kitila Mkumbo ni mtaalamu wa mambo ya Elimu, alipewaje kazi ya kutengeneza model ya mambo ya uchaguzi ambayo hakusomea? Wewe mtu hakuwahi kusoma hata course moja ya political science ndiyo anapewa kuratibu na kupanga utaratibu wa program za kisiasa, are we wicked? Kitila ni mtaalamu wa mambo ya saikolojia na ufundishaji. Masuala ya watoto wanajifunzaje ndiyo anayoyajua.

Ujinga wa aina hiyo hiyo wa kuwaweka watu wasio wataalam wa eneo huska unafanywa kila mahali katika nchi hii! Ndiyo maana awali nimesema hii nchi ni kama ya machizi, kila chizi aliyemo ndani ya nchi anafanya kinachompendeza yeye na hakuna mwenye kumkemea mwenzie kwa kuwa level ya uchizi ni almost inalingana. Hakuna mwenye unafuu.
 
Last edited by a moderator:
ndio maana tunataka kuwatoa madarakani
MaCCM wao kukbali kila kitu kinachotoka ndani ya Chama chao na hawataki mtu apinge kisa wao ndio wamefanya
mtoa mada ameelezea hisia zake kuhusu uteuzi wa hawa makatibu wakuu.
Ni maoni yake, sishangai kwani ndio nyie nyie mnataka Shein amtimue kazi Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar kisa
hakajubaliana na nyie kuhusu serikali 2 mkasahau yeye sio mwanasiasa.

Kuhusu kudisco wanafunzi napingana na mleta hoja.
wanafunzi kudisco dean of faculty hausiki ni uzembe wa wanafunzi wenyewe
mnashinda mabweni,skype,whattsApp, madisco,vipindi mnakosa, hamtaki kusoma mnategemea nini?
Wacha tusubiri utendaji wake kama atafanya changes yoyote.

nadhani nawe Hamy-D kwa akili zako za kutokujua kujenga nawe ulistahili kudisco kupokea buku 7
kwa sasa huna jipya zaidi ya kuponda wapinzani,na sijakuona hata siku moja unaibua madudu yaliyo
katika chama chako kama ufisadi,wizi,mauaji,rushwa, madawa ya kulevya na kupeana vyeo kwa kujuana.

Mleta mada hivi una umri gani?

Kama umeweza kuhitimu shahada ya sheria ukiwa na akili hizi, basi napata shaka na vyuo vyetu, maana mtu kama wewe ulipaswa ku-disco ili chuo kilinde hadhi yake.

Eti napinga uteuzi, unajua nini maana ya mamlaka wewe?
 
ukoo wa panya dah!

hii ndo Tanzania, Nchi yenye maajabu haihitaji elimu kubwa sana kuleta mabadiliko na pia huwa hatuzingatii ni mabadiliko chanya, hasi or else na ikiwezekana ukiona unafaa wahusishe hata wakweo katika kazi zako za ofisini hamnaatayekuuliza
 
Nafikiri sasa tunaongea lugha inayofanana, Kitila Mkumbo ni mtaalamu wa mambo ya Elimu, alipewaje kazi ya kutengeneza model ya mambo ya uchaguzi ambayo hakusomea? Wewe mtu hakuwahi kusoma hata course moja ya political science ndiyo anapewa kuratibu na kupanga utaratibu wa program za kisiasa, are we wicked? Kitila ni mtaalamu wa mambo ya saikolojia na ufundishaji. Masuala ya watoto wanajifunzaje ndiyo anayoyajua.

Ujinga wa aina hiyo hiyo wa kuwaweka watu wasio wataalam wa eneo huska unafanywa kila mahali katika nchi hii! Ndiyo maana awali nimesema hii nchi ni kama ya machizi, kila chizi aliyemo ndani ya nchi anafanya kinachompendeza yeye na hakuna mwenye kumkemea mwenzie kwa kuwa level ya uchizi ni almost inalingana. Hakuna mwenye unafuu.
Mkuu Lukolo sikuelewi kwa nini unazunguka sana kuelezea wasifu wetu Watanzania.

Siamini kama Watanzania 'waliosoma' ni machizi kama unavyodai kwa vile chizi ni yule anayefanya mambo bila kujitambua.

Hawa binadamu wanaelewa sana kile wanachokifanya ikiwa ni pamoja na malengo ya kuwepo kwao kwenye hivyo vyeo vya 'kupeana'.

Tatizo linaloisumbua jamii yetu ni ubinafsi na unafiki. Ninaamini kuna Watanzania wachache sana kama wapo wanaweza kupewa kazi ya Ukatibu wa Wizara na kukataa kwa sababu wanaamini hawana uwezo au wanaamini nguvu zao professionally lazima ziwe sehemu fulani. They can't let it go.

Watanzania wengi wako tayari kujaza au kukubali kujaziwa madaraka bila hata ufanisi wowote kwa sabau wamegubikwa na ubinafsi.

Mpaka ubinafsi na unafiki utakapoondoka, tutaendelea kuona action kama hizi nchini kutaka vyote au kupewa vyote kwa nothing.
 
Wasifu wa Prof sifuni Mchome nimeanza kuujua pindi nipo katika kitivo cha Sheria pale Udsm aalifanya madudu yafuatayo.
1. Mwaka 2007 waliokuwa second year ya mwaka 2007 kitivo cha sheria wakati huo yeye akiwa Dean wa Faculty walidisco wanafunzi 25 kati ya 150 sitaki kuamini kama kweli wote waliodisco walikuwa hawana uwezo jibu analo Sifuni mchome.
2. Mwaka huo huo akiwa Dean wa Fuculty yeye ndiye muasisi wa kitu kinaitwa "Lawskul" kwa upande wangu naona ni ukilitimba na alifuta kitu kiitwacho Intership mpaka leo usipo enda lawskull yaani wewe ni sawa na bure japo umehitimu digrii ya sheria anajua sifuni mchome kwa nini alifuta Intership hata baada ya maandamano ya kitivo cha sheria pale Mlimani sifuni mchome kwa dharau akawaambia kama hawataki si lazima kusoma kikao ambacho kilikaa Yombo lecture rooms kwa takribani zaid ya masaa 3.
3. Ni mchome huyuhuyu aliyekuwa akiwanyima wanafunzi wa kitivo cha sheria Special fuculty Requirment lakin hakufua dafu kwa second year ya mwaka 2007 baada ya kuwapa 60% badala ya mia moja.
4. Ni sifuni mchome aliye kuwa katibu wa TCU ambaye alisababisha wanafunzi wengi kukosa udahili na hata waliopata hawakufanikiwa kupata mkopo.
5. Tusitarajie mapya katika wizara hii ambayo ina sifa ya kuwa na waziri asiyejua English na kwa CV hiyo tutarajie ubabe mkubwa wa sifuni Mchome usio kuwa na tija katika elimu.
Ni hayo tu.

Tutajie unaeona anafaa ili tujue uelewa wako.
 
We hujui kwamba Katibu Mkuu anasimamua utekelezaji kwa kufuata misingi ya SHERIA. Kwani fani gani inafundisha makatibu wakuu?

mPEEEEE aelewe.
Teuzi zote zinakataliwa.Sasa ni nani anatakiwa?
Nani ateue ili watu waridhike? Nyie mnaolalama mkipewa pia mtajikataa kuwa mmeteuliwa na dhaifu hivyo hamfai?
MAJANGA!
 
Mkuu Lukolo sikuelewi kwa nini unazunguka sana kuelezea wasifu wetu Watanzania.

Siamini kama Watanzania 'waliosoma' ni machizi kama unavyodai kwa vile chizi ni yule anayefanya mambo bila kujitambua.

Hawa binadamu wanaelewa sana kile wanachokifanya ikiwa ni pamoja na malengo ya kuwepo kwao kwenye hivyo vyeo vya 'kupeana'.

Tatizo linaloisumbua jamii yetu ni ubinafsi na unafiki. Ninaamini kuna Watanzania wachache sana kama wapo wanaweza kupewa kazi ya Ukatibu wa Wizara na kukataa kwa sababu wanaamini hawana uwezo au wanaamini nguvu zao professionally lazima ziwe sehemu fulani. They can't let it go.

Watanzania wengi wako tayari kujaza au kukubali kujaziwa madaraka bila hata ufanisi wowote kwa sabau wamegubikwa na ubinafsi.

Mpaka ubinafsi na unafiki utakapoondoka, tutaendelea kuona action kama hizi nchini kutaka vyote au kupewa vyote kwa nothing.

Ukipewa utakataa? Sema ukweli!
Tatizo nilionalo mimi pia ni wivu kuwa kwanini fulani kapata na siyo mimi, au kwanini siyo ndugu yangu kateuliwa?
Akiteuliwa baba/mama yako utamshauri akatae kwa vile hawezi??
 
Lukolo umenena kama nlvokuwa nawaza..(likes 500) haiwezekani, labda atuambie anashahada ya elimu ili tuweze kuamini walau kwamba atakiweza kikombe alchopewa...nan katuloga jamani??? elimu iko mahututi, badala ya kuweka watu wenye uwezo stahiki tunalpana fadhila. Agrrrrrrrr!!!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Lukolo sikuelewi kwa nini unazunguka sana kuelezea wasifu wetu Watanzania.

Siamini kama Watanzania 'waliosoma' ni machizi kama unavyodai kwa vile chizi ni yule anayefanya mambo bila kujitambua.

Hawa binadamu wanaelewa sana kile wanachokifanya ikiwa ni pamoja na malengo ya kuwepo kwao kwenye hivyo vyeo vya 'kupeana'.

Tatizo linaloisumbua jamii yetu ni ubinafsi na unafiki. Ninaamini kuna Watanzania wachache sana kama wapo wanaweza kupewa kazi ya Ukatibu wa Wizara na kukataa kwa sababu wanaamini hawana uwezo au wanaamini nguvu zao professionally lazima ziwe sehemu fulani. They can't let it go.

Watanzania wengi wako tayari kujaza au kukubali kujaziwa madaraka bila hata ufanisi wowote kwa sabau wamegubikwa na ubinafsi.

Mpaka ubinafsi na unafiki utakapoondoka, tutaendelea kuona action kama hizi nchini kutaka vyote au kupewa vyote kwa nothing.
Thanks Ng'wamapalala kwa kuliweka sawa hili. Ninafikiri nilikuwa na hasira zilizopitiliza kiasi cha kuona kila mtu ni mwehu tu. Maana siamini kama haya yanatokea halafu hakuna hata wa kukanusha au kuyapigia kelele kukemea. Maana kwa hakika hata kama ni ubinafsi umezidi kipimo. Lakini mimi namlaumu mteuaji, maana yeye anajua kazi gani inahitaji sifa gani, ni kwa vipi akurupuke kumteua mtu anayemjua wazi kwamba hana sifa za kufit hapo. Ndiyo maana kazi nyingi kwenye maofisi ya serikali haziendi ipasavyo, maana watu wanaopewa kazi ni wale wasio na sifa, huku watu wenye sifa stahiki wakiachwa.
 
Last edited by a moderator:
Ukipewa utakataa? Sema ukweli!
Tatizo nilionalo mimi pia ni wivu kuwa kwanini fulani kapata na siyo mimi, au kwanini siyo ndugu yangu kateuliwa?
Akiteuliwa baba/mama yako utamshauri akatae kwa vile hawezi??
Katika hali ya kibinadamu na katika nature ya selfishness ya binadamu ni vigumu sana. Ndiyo maana personally namlaani mteuaji. Na hiki ndicho ninachokisisitiza kwa Gaijin ambaye anataka tumlaumu aliyeteuliwa.
 
Last edited by a moderator:
Wasifu wa Prof sifuni Mchome nimeanza kuujua pindi nipo katika kitivo cha Sheria pale Udsm aalifanya madudu yafuatayo.
1. Mwaka 2007 waliokuwa second year ya mwaka 2007 kitivo cha sheria wakati huo yeye akiwa Dean wa Faculty walidisco wanafunzi 25 kati ya 150 sitaki kuamini kama kweli wote waliodisco walikuwa hawana uwezo jibu analo Sifuni mchome.
2. Mwaka huo huo akiwa Dean wa Fuculty yeye ndiye muasisi wa kitu kinaitwa "Lawskul" kwa upande wangu naona ni ukilitimba na alifuta kitu kiitwacho Intership mpaka leo usipo enda lawskull yaani wewe ni sawa na bure japo umehitimu digrii ya sheria anajua sifuni mchome kwa nini alifuta Intership hata baada ya maandamano ya kitivo cha sheria pale Mlimani sifuni mchome kwa dharau akawaambia kama hawataki si lazima kusoma kikao ambacho kilikaa Yombo lecture rooms kwa takribani zaid ya masaa 3.
3. Ni mchome huyuhuyu aliyekuwa akiwanyima wanafunzi wa kitivo cha sheria Special fuculty Requirment lakin hakufua dafu kwa second year ya mwaka 2007 baada ya kuwapa 60% badala ya mia moja.
4. Ni sifuni mchome aliye kuwa katibu wa TCU ambaye alisababisha wanafunzi wengi kukosa udahili na hata waliopata hawakufanikiwa kupata mkopo.
5. Tusitarajie mapya katika wizara hii ambayo ina sifa ya kuwa na waziri asiyejua English na kwa CV hiyo tutarajie ubabe mkubwa wa sifuni Mchome usio kuwa na tija katika elimu.
Ni hayo tu.

Duh!!! MKUU ulisoma sheria? Uandishi wako kweli unashahidia kuwa ulisoma UDSM enzi za huyu Mchome
 
Ukipewa utakataa? Sema ukweli!
Tatizo nilionalo mimi pia ni wivu kuwa kwanini fulani kapata na siyo mimi, au kwanini siyo ndugu yangu kateuliwa?
Akiteuliwa baba/mama yako utamshauri akatae kwa vile hawezi??
Mkuu inategemea wivu unauweka katika mtazamo gani. In fact wivu ni kichocheo cha mabadiliko katika jamii, kwa lugha nyingine wivu ni unaweza ukawa katika hali chanya au hasi. Wivu unaweza kuwa mzuri au mbaya.

Hali chanya kwa maana kuwa inakufanya upatwe na msukumo kufanya au kupata zaidi ya kinachokufanya kuwa na wivu. Hali hasi kwa maana kuwa, inakufanya kuangamiza kile kinachokufanya kuwa na wivu.

Katika dunia hii, siamini kama kuna binadamu asiyekuwa na wivu na kama yupo, basi huyo ni binadamu mfu.

Kwa jinsi Tanzania ilivyo, wananchi wengi naamini wangeshangaa sana kama Prof. Sifuni angekataa uteuzi lakini siyo kukubali uteuzi kwa sababu unafiki na ubinafsi imekuwa ni kawaida katika maisha ya wananchi nchini.

Swala la mimi kukubali au kukataa ni subjective na ni kujiingiza kwenye udaku kuanza kulijengea hoja kwa sababu halipo na halitakuwepo.
 
Ok, tufanye professor aliyekubali kuteuliwa kutoka kitengo cha sheria kwenda kuwa katibu mkuu wizara ya Elimu ni Zezeta. Na je aliyemteua mtu ambaye anajua wazi hana utaalamu na mambo ya elimu na kumpeleka kuwa mtendaji mkuu tumuitaje?
Kwanini tufanye ni zezeta wakati si zezeta?

Mtu hadi anafika kuwa Professor wa Sheria, utatakaje tuchukulie kuwa ni zezeta?

Utasemaje dean wa sehemu, au kiongozi wa TCU kuwa hana utaalamu wa elimu?

Au unadhani kazi ya u-dean ni kuhukumu kesi pale?

Jifanye wewe Gaijin ndiyo Principal wa chuo, halafu unamteua mwalimu wa hesabu kuwa mkuu wa idara ya Kiingereza. Wewe unakuwa ni nani katika context hiyo? Maana naona kama hiyo sifa ya uzezeta tu itakuwa haikutoshi, labda kichaa kabisa. How on earth unamjua mtu kwamba amesomea ufugaji wa nyuki (unajua kabisa) lakini unamteua kuwa katibu mkuu au msimizi wa kitengo cha ujenzi wa barabara? Kama si utaahira huo ni nini?

Kwanza unachokifungia macho ni kwamba, hata huko wizara ya elimu kunahitajika sana, tena mno, ujuzi wa sheria.

Pili mtu aliyekuwa na vyeo vya kiuongozi kwenye taasisi za kielimu, huwezi kuniaminisha kuwa yeye alikuwa anatumia sheria tu pale, na hafanyi yaliyo nje ya hapo

Kama amekuwa katibu wa TCU na Dean basi huyu hatumii sheria peke yake katika utendaji wake.

Kuhusu mteuliwa nimeshasema awali kwamba kwa mtu kama Professor wa UDSM mwenye lundo la kazi zisizoisha, na mshahara usioridhisha, ukimpa cheo kama hicho atakubali tu maana anaona hiyo ndiyo sehemu yake ya kwenda kupumzika. Na ndiyo maana hii nchi imejaa resources za kutosha lakini ni maskini ya kutupwa. Planners wa masuala ya madini wengi wao wamesoma bachelor of arts in public administration. Anajua nini kuhusu madini huyu?

Yaani kuna wakati mwingine tunafanya mambo kama machizi hivi. Kila mmoja ndani ya nchi anajifanyia anachokitaka, na hakuna wa kumkemea mwenzie kwa kuwa wote wana uchizi unaolingana.

Kwa hiyo mteuliwa tumpe a pass kwa sababu ana dhiki hawezi kutoacha ulaji

Inayomaanisha na wewe pia unaona ukatibu mkuu ni ulaji na huwezi kuuacha.

Kama tunataka kutaka watu wenye integrity, tutake kuanzia juu mpaka chini.

Sio tunamkosoa mmoja na mmoja tunakubali matendo yake kuwa ni sawa kwa vile tu ule ulaji
 
Nafikiri sasa tunaongea lugha inayofanana, Kitila Mkumbo ni mtaalamu wa mambo ya Elimu, alipewaje kazi ya kutengeneza model ya mambo ya uchaguzi ambayo hakusomea? Wewe mtu hakuwahi kusoma hata course moja ya political science ndiyo anapewa kuratibu na kupanga utaratibu wa program za kisiasa, are we wicked? Kitila ni mtaalamu wa mambo ya saikolojia na ufundishaji. Masuala ya watoto wanajifunzaje ndiyo anayoyajua.

Ujinga wa aina hiyo hiyo wa kuwaweka watu wasio wataalam wa eneo huska unafanywa kila mahali katika nchi hii! Ndiyo maana awali nimesema hii nchi ni kama ya machizi, kila chizi aliyemo ndani ya nchi anafanya kinachompendeza yeye na hakuna mwenye kumkemea mwenzie kwa kuwa level ya uchizi ni almost inalingana. Hakuna mwenye unafuu.

Sasa kama Kitila haikuwa kazi yake kutunga model ya uchaguzi kwa nini aliikubali?

Au kama ni miongoni mwa aliyoyasomea, mbona model ovyoo kabisa?

Jibu lolote kati ya hayo mawili linaonyesha kuwa Kitila ama hana integrity ya kukataa kitu asichokiweza ama hana uwezo wa kufanya katika aliyoyasomea ama yote mawili kwa mpoigo na hafai kupewa cheo cha ukatibu mkuu wa Wizara ya Elimu
 
It was a keyboard mistake which is curable wherever there is the Illegularities look on the content and not form.

Na wewe unamtetea wakati bado unachapia. Hakuna neno illegularities ni "irregularities". Hawa ndio wasomi wanaotaka wapewe madaraka makubwa.
 
Napinga uteuzi:
1. Mchome kwa taaluma yake ni mwanasheria maarifa aliyo nayo ni kuhusu sheria za mikataba, katiba, biashara, haki n.k, angepaswa kuwepo kwenye vyombo vya kisheria ili kupata zao haswa la ujuzi wake. Kumtuma mwanasheria kwenye sekta ya elimu kama mtendaji mkuu ni sawa na kumpa mtu ndoano akavue samaki jangwani.
2. Elimu na usimamizi wa elimu hauishi tu katika kuhimiza walimu kuchapa kazi na kukimbiza watu mchakamchaka. Bali usimamizi huusisha pia swali la kuratibu ubora wa MITAALA, SERA ZA ELIMU NA MIONGOZO. Kwa mtu anayetafakari kwa kina ataona kwamba maswala hayo yanahitaji ujuzi na maarifa ya kiUALIMU thabiti. Mchome hajui andalio la somo, muhutasari, mpango wa kazi, jedwali la utahini n,k, anakuja kufanya nini kwenye ELIMU. Hajui UKAGUZI wa elimu hupima mambo gani, ataweza nini?
3. Tuko katika mkakati wa mabadiliko makubwa sasa BIG RESULTS NOW. Kwa mwenendo huu WE WON'T EVEN MOVE AN INCH. Ni sawa na kuharibu mkondo wa mto halafu usitegemee mafuriko.
4. Mwisho TUTEGEMEE MADUDU. MUNGU TUBARIKI WANAO.

Alikuwa ni mwalimu UDSM, kweli asijue hayo kwenye RED!
 
Katika hali ya kibinadamu na katika nature ya selfishness ya binadamu ni vigumu sana. Ndiyo maana personally namlaani mteuaji. Na hiki ndicho ninachokisisitiza kwa Gaijin ambaye anataka tumlaumu aliyeteuliwa.

Ni upuuzi wa mwisho kuwatetea watu wanaopokea kazi ambazo hawana uwezo nazo

Na hilo hasa ndilo lililotufikisha Tanzania hapa tulipo.

Tunawapa wanatetea mambo ambayo ni kinyume na kanuni za maendeleo

Mbona nchi nyingine watu wanakataa, au wale si binaadamu kama sisi?

Yoyote anaepewa cheo asichokimudu na akakipokea ni mkosa mbele ya watanzania kama huyo alomteua.
 
at least sasa umekubali kwamba na mteuaji ana makosa. Maana mwanzoni ulikuwa kama vile unamsukumia mzigo mteuliwa tu.
 
Back
Top Bottom