Napinga sifa za kinafiki anazopewa Maalim Seif leo na Watu wale wale waliomdhalilisha

Hakuna uadui wa kudumu au urafiki wa kudumu kwenye siasa. Kufikiri otherwise ni kuwa naive.

Unafiki huo huo unaupima vipi kwa Edward Lowassa?Alipokuwa CCM ilidaiwa na Chadema kwamba ni fisadi.Alipoingia Chadema akapewa fursa ya kugombea urais.Fisadi akabadilika kuwa mgombea urais na akasifiwa.

Kabla ya kudai moral authority ya kuita watu wanafiki toa boriti kwenye jicho lako kabla hujaona ubanzi kwenye jicho la mwenzako.
Kwa kumalizia ni utamaduni wetu kutosema ubaya wa marehemu kama anao huo ubaya.

Kama watu wanafuata utamaduni huo au hapana is another case for another day.
Kwahiyo ccm wanafunga urafiki mpya na marehemu?
 
Maalim Seif alifariki akiwa na cheo gani?Au umeanza kumfahamu akiwa marehemu?Kusoma na kuelewa ulichokisoma ndio hitaji la hiyo mada ili uweze kujibu na kushiriki.
 
Wakati Maalim Seif anaporwa ushindi 2015 Rais alikuwa Mwendazake ? kuitenga ccm na unafiki ni ngumu kuliko ngamia kupenya kwenye tundu la sindao
jidanganye nimie nikikuuliza kipindi hiko mlikuwa pamoja mkijiita ukawa je mlisaidiaje baada ya kuona amedhurumiwa haki yake ? Siasa za majungu✖️, siasa za chuki✖️, siasa za ukabila✖️ , siasa za ubabe ✖️,kwa tanzania 🇹🇿 ya sasa hazina nafasi tena chini ya mama yetu kipenzi .muhasisi wa siasa hizo unazotaka ameshaenda zake na kama bado wapo inshaa,allah m/mungu atawashughurikia tu
 
Hakuna uadui wa kudumu au urafiki wa kudumu kwenye siasa. Kufikiri otherwise ni kuwa naive.

Unafiki huo huo unaupima vipi kwa Edward Lowassa?Alipokuwa CCM ilidaiwa na Chadema kwamba ni fisadi.Alipoingia Chadema akapewa fursa ya kugombea urais.Fisadi akabadilika kuwa mgombea urais na akasifiwa.

Kabla ya kudai moral authority ya kuita watu wanafiki toa boriti kwenye jicho lako kabla hujaona ubanzi kwenye jicho la mwenzako.
Kwa kumalizia ni utamaduni wetu kutosema ubaya wa marehemu kama anao huo ubaya.

Kama watu wanafuata utamaduni huo au hapana is another case for another day.

Je, IPO kauli rasmi au azimio la CHADEMA linalodai kuwa Lowassa SI fisadi? Na kumuomba radhi kwa kumchafua hadharani? Naomba kauli/azimio hilo liwekwe wazi hapa JF tuthibitishe unafiki wa chama hicho.

Sioni kama kumpa fursa kuwa mgombea uRais wa CHADEMA 2015 ndio ilikuwa kusema Lowassa SI fisadi. Bali naona ulikuwa ni mkakati wa CHADEMA kushinda uchaguzi (BY ANY MEANS!) kwa kutegemea nguvu na ufuasi mkubwa aliokuwa nao Lowassa ndani ya nchi. Yaani CHADEMA waliamua kutupilia mbali kanuni yao ya uadilifu kwa manufaa ya REALPOLITIK inayodai lengo kubwa la chama cha siasa ni kushika dola hata kwa kanuni ya THE END JUSTIFIES THE MEANS!

Kwetu sisi waumini wa siasa safi - unaweza kutuita IDEALISTS (wadhanifu) - tulisikitika sana kwa CHADEMA kwenda kinyume na msimamo wake na hivyo kujifananisha na CCM. Walipata matokeo makubwa sana kwenye uchaguzi ule (inaaminika walishinda kwa kura) lakini waliumia kwenye MORAL AUTHORITY.

Sasa kama hakuna kauli rasmi ya CHADEMA kudai Lowassa si fisadi, basi hakuna unafiki uliofanyika. Wahukumiwe kwa kukumbatia “siasa chafu” REALPOLITIK baadala ya kukomaa na maadili ya chama.

Leo CCM ambao mara kadhaa wanamtambulisha Lowassa kama fisadi mkuu wamemkumbatia vizuri sana ndani ya chama chao kama mwanachama wao muhimu sana. Kumbuka, Dr. Slaa aliwahi kumfananisha na “choo kuhamishiwa sebuleni”. Je, huu ni unafiki au nayo ni REALPOLITIK?
 
Just curious Dk Slaa aliwahi kumfananisha na choo kuhamishiwa sebuleni akiwa chama kipi?Ni nani hao waliokihamishia choo sebuleni?
Huna uwezo wa uchambuzi kabisa , mada ni Maalim Seif , Wafuasi wake kwa mamia wameuawa na ushahidi upo , leo waliosababisha mauaji ya watu wake wanamsifia , Je kuna mfuasi yeyote wa Lowassa aliuawa na CHADEMA ?
 
Pambana na mwenyekiti wako atoke jela ishu ya maalim seif waachie act na CCM wanaounda serikali ya umoja na ndio maana wakashirikiana kwenye hilo tukio/uzinduzi nyie CDM mnakereka nini kama sio wivu wa kike tu
 
Tena cha kushangaza kumbukumbu imeandaliwa na ccm kaalikwa na mke wa maalim
Kumbukumbu ya Maalim Seif Foundation haijaandaliwa na CCM.Mama Samia kaitwa afungue uanzishaji wa foundation hiyo.
Kwa mujibu wa Ismail Jussa mjumbe wa kamati ya muda ya Maalim Seif Foundation,dhumuni ikiwa ni kuenzi kazi nzuri iliyofanywa na Maalim Seif.
Mada ya mwaka huu ni dhana ya maridhiano na umoja wa kitaifa.
 
Tafsiri yako siipingi , bali tunapoandika ukweli hapa jf hatushindani na mtu yeyote
Ni kweli kabisa, ila kumbuka huo "ukweli" unatakiwa uwe na nguvu na pasiwepo na hoja za kuukosoa. Vinginevyo yale tunayoyaandika yasichukuliwe kuwa ni ukweli bali ni "dhana" zinazotokana na fikra zetu.
 
Back
Top Bottom