Napinga Serikali kutoa elimu ya msingi na Sekondari bure

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,975
48,843
Elimu imekuwa ya mateso kwa wanafunzi, walimu na serikali kwa ujumla. wazazi wamekuwa walevi wamedumaa hawafikirii tena kupambana hata kupata ile elfu 20 tatu vitu vya bure havina uchungu hata kidogo wazazi sasa wamewatelekeza watoto na kuacha majukumu yao nashauri serikali warudishe karo shuleni.

Elimu ya bure iwe ya chuo kikuu na vyuo vya ufundi stadi sio unamsomesha mtu bure anamaliza form four anapata zero anao, anaolewa. Tuache siasa toka elimu bure ianze wazazi wamejisahau sana hawana kabisa uchungu na watoto wao.

kama ni watoto yatima mfumo ulikuwepo toka zamani wa kuwasomesha serikali inaujua lakini ili la kusomesha watoto halafu baba zao wanashinda kulewa halikubaliki hata kidogo.

Kwa mzazi anayejitambua hawezi kumpeleka mtoto wake akakae chini kisa shule ya bure.
 
Sent using Jamii Forums mobile app[/QUOTE]Mkuu, hili suala la elimu kutolewa kwa kisingizio cha bure ulikuwa ni uamuzi wa kukurupuka. Ulikuja kutokana na kudandia treni kwa mbele hoja ambayo ilikuwa imetolewa na kusisitizwa na CDM na wala si vinginenevyo.

Hakukuwa na matayarisho ya kutosha katika kuipokea hoja hii. Ilikuwa ni uamuzi wa kushangaza, kwa kuwa kutokana na Structural Adjustment Programs (SAPs) za miaka ya 1980s kutokana na masharti ya IMF yalilazimisha serikali ya awamu ya kwanza kuachana na utoaji wa elimu bure.

Chama kile kile kilichowahi kuwahi kushindwa kuendesha mpango huu, kingepaswa kujiuliza kama sababu na changamoto za kuachana nao kama bado zilikuwapo, ama uwezo wa serikali ktk kugharimia elimu hii kwa ubora unaokubalika kama ulikuwepo na pia kama kungekuwa na mpango endelevu unaoendana na mahitaji halisi ya kifedha ktk kusukuma mbele kwa tija elimu ya msingi.

Tatizo ni siasa siasa siasa tu hata ktk mambo ya msingi kama yahusuyo elimu kwa watoto na wajukuu zetu. Watu wengi hupenda vya bure ndiyo maana hawapendi ama wanapenda kubebwa tu ktk majukumu yao kama wazazi. Wewe kama unapenda kuzaana bila ya utaratibu, basi tambua ni jukumu lako kuwalea watoto zako na kuwapa huduma muhimu ikiwamo suala la kugharamia elimu.

Mimi ningeshauri serikali ingeweka sheria mathubuti za ustawi wa jamii, ili kila mtu ambaye itathibitika ana mtoto ama ametelekeza mtoto awajibishwe kisheria ktk kumgharamia ktk huduma zote muhimu ikiwemo elimu ya msingi. Ni vyema sasa serikali ikalitua zigo hili ambalo kwa vigezo vyote inaonyesha kuelemewa nalo.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Elimu imekuwa ya mateso kwa wanafunzi, walimu na serikali kwa ujumla. wazazi wamekuwa walevi wamedumaa hawafikirii tena kupambana hata kupata ile elfu 20 tatu vitu vya bure havina uchungu hata kidogo wazazi sasa wamewatelekeza watoto na kuacha majukumu yao nashauri serikali warudishe karo shuleni.

Elimu ya bure iwe ya chuo kikuu na vyuo vya ufundi stadi sio unamsomesha mtu bure anamaliza form four anapata zero anao, anaolewa. Tuache siasa toka elimu bure ianze wawazi wamejisahau sana hawana kabisa uchungu na watoto wao.

Mimi binafsi nalisema ili kwa mzazi anayejitambua hawezi kumpeleka mtoto wake akakae chini.
Elimu ya ufundi ndio itolewe bure
 
Mfikrie Yohana wa Simiyu aliyesoma kwa tabu na dhiki na pengine bila elimu bure asingesoma kabisa kabla ya kuandika kumfurahisha mbowe
Mfikirie baba yake Yohana, mtu ambaye hatajwi sana, ila bayana kuwa alimtelekeza kijana wake aliyekuja kubainika kuwa ni kipanga hata akakosa fursa muhimu ya kupata elimu ikiwa ni jukumu lake kubwa kama mzazi mwenye kuwajibika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom