Napinga Makamu Mwenyekiti wa CCM Abdulrahman Kinana kuwa mgeni rasmi kwenye game ya Simba vs Orlando Pirates

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,373
217,435
Klabu_ya_Simba_SC_imemtangaza%2C_Abdulrahman_Kinana%2C_Makamu_Mwenyekiti_wa_Chama_cha_Mapinduz...jpg

Ni lazima waandaaji wa mechi za soka watambue kwamba , soka ndio mchezo pekee unaounganisha watu wote bila kujali itikadi za kisiasa , Umri , Jinsia , dini , rangi wala makabila yao .

Kuweka kiongozi wa CCM kuwa mgeni rasmi wa mechi ya kimataifa ya CAF ni kitendo ambacho lengo lake ni kumtambulisha Kinana mbele ya Watazamaji , Jambo hili la kutumia soka kupata Ahueni ya kisiasa halikubaliki na tutalipinga kwa nguvu zote , LIWALO NA LIWE !

Kwani ni nani Hamjui Kinana mpaka muanze kuvunja protokali kwa kumpachika asipostahili , Waziri wa Michezo au viongozi wengine wa serikali wako wapi ? Halafu Kinana na Soka wapi na wapi jamani ?

Huyu Rais wa TFF wa sasa Karia ndio kiongozi wa soka wa Tanzania anayejiingiza mno kwenye siasa , jambo hili likiachwa liendelee litavuruga soka na kusababisha Fujo , iko siku tutaleta viongozi wa Chama Chetu ili wawe Wageni Rasmi bila hata kualikwa .

Majuto ni Mjukuu .
 
basi isomeke Mgeni wa Heshma ni Waziri wa zamani wa Ulinzi na jeshi la kujenga Taifa, Kanali mstaafu, Spika mstaafu wa Bunge la Afrika mashariki na Mbunge wa zamani wa Arusha mjini

kama yote hutaki basi isomeke Mgeni wa heshma ni Mmiliki na mfanyabiashara maarufu wa usafirishaji na Mmiliki wa meli za usafurishaji na Uvuvi hapa nchini
 
wanaharibu mchezo sasa, kuweka wazee wa chama cha mapinduzi wanakosea. Simba wanakosea sana kwa hili
 
View attachment 2190571

Ni lazima waandaaji wa mechi za soka watambue kwamba , soka ndio mchezo pekee unaounganisha watu wote bila kujali itikadi za kisiasa , Umri , Jinsia , dini , rangi wala makabila yao .

Kuweka kiongozi wa CCM kuwa mgeni rasmi wa mechi ya kimataifa ya CAF ni kitendo ambacho lengo lake ni kumtambulisha Kinana mbele ya Watazamaji , Jambo hili la kutumia soka kupata Ahueni ya kisiasa halikubaliki na tutalipinga kwa nguvu zote , LIWALO NA LIWE !

Kwani ni nani Hamjui Kinana mpaka muanze kuvunja protokali kwa kumpachika asipostahili , Waziri wa Michezo au viongozi wengine wa serikali wako wapi ? Halafu Kinana na Soka wapi na wapi jamani ?

Huyu Rais wa TFF wa sasa Karia ndio kiongozi wa soka wa Tanzania anayejiingiza mno kwenye siasa , jambo hili likiachwa liendelee litavuruga soka na kusababisha Fujo , iko siku tutaleta viongozi wa Chama Chetu ili wawe Wageni Rasmi bila hata kualikwa .

Majuto ni Mjukuu .
Yaaan mechi ni ya kimataifa alafu tunaalika kiongozi wa chama kama vile washibiki wa simba wote sisim
 
Kuna siku Tena Hawa hawasimba wakamleta ndugai kuja kuwa mgen rasm sielewi wanamaana gani haswa lzm niwaandikie caf au FIFA barua kulikaripia hili
 
Back
Top Bottom