Napigilia Msumari: Kuna mambo ya Ovyo Ovyo na ya Kipambavu Ndani ya Serikali...

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndugu zangu,

Kauli ya Rais John Pombe Magufuli akiwa Tanga juzi hapa ni ya kijasiri na yenye kumpambanua kama Kiongozi Mkuu wa Nchi.

Rais Magufuli amesikika akisema hivi;

" Kuna mambo ya ovyo ovyo na ya kipumbavu ndani ya Serikali."

Ni kauli ya kijasiri kwa Kiongozi Mkuu wa Nchi kuyasema hayo hadharani. Inahusu Serikali yake. Amefanya hivyo katika mantiki ile ya mficha maradhi kifo humuumbua.

Ukweli Rais amewasemea wengi anaowaongoza. Ni ukweli, kuwa Serikalini kuna watendaji wazuri wengi wenye mioyo ya uzalendo, lakini, wapo wachache wenye kufanya ya ovyo ovyo na ya kipumbavu mpaka mtu unajiuliza walipataje ajira.

Yaani, unamkuta mtumishi anahujumu wazo jema kwa maendeleo ya nchi kwa kutanguliza, ama maslahi binafsi, au kuwa na chuki binafsi tu na mwenye wazo la maendeleo. Ni aina hii ya watumishi wenye kufanya kazi kwa misingi ya majungu na fitina tu, basi.

Ni imani yetu, Awamu hii ya Magufuli watumishi wa aina hii watapukutika kwa wingi waiache nchi yetu isonge mbele.

Maggid Mjengwa.

Iringa.
 
Ila naona bora angewatumbua tu kuliko kuwaita wapumbavu huku umewaacha kwenye madaraka yao. Kwanini aunde serikali ya wapumbavu?

Aweke utaifa mbele, ateue watu bila kujali itikadi zao mradi wana qualify na ni wazalendo.

Kazi ya kusema ni wapumbavu ni yetu wananchi na ndiyo uhuru wa kukosoa unapopata mantiki. Kazi ya kwake ni kutenda, maana kila mmoja akilalamika nani atatenda?
 
Hivi wewe ulihitaji mpaka Magufuli aseme ndiyo ujue kama kuna upumbavu?

Aliyeondoa kwenye mzunguko wa pesa nchini nusu trilioni ni Waziri yupi!? Huyu aliyefanya uamuzi huo bila ya kuwashirikisha wataalamu wa mambo ya uchumi tumwiteje? Na mnunuzi wa kivuko uchwara cha bilioni 8 je!? Tafakari kwa kina acha kukurupuka ili kujikomba kwenye vyeo.

Ndugu zangu,

Kauli ya Rais John Pombe Magufuli akiwa Tanga juzi hapa ni ya kijasiri na yenye kumpambanua kama Kiongozi Mkuu wa Nchi.

Rais Magufuli amesikika akisema hivi;

" Kuna mambo ya ovyo ovyo na ya kipumbavu ndani ya Serikali."

Ni kauli ya kijasiri kwa Kiongozi Mkuu wa Nchi kuyasema hayo hadharani. Inahusu Serikali yake. Amefanya hivyo katika mantiki ile ya mficha maradhi kifo humuumbua.

Ukweli Rais amewasemea wengi anaowaongoza. Ni ukweli, kuwa Serikalini kuna watendaji wazuri wengi wenye mioyo ya uzalendo, lakini, wapo wachache wenye kufanya ya ovyo ovyo na ya kipumbavu mpaka mtu unajiuliza walipataje ajira.

Yaani, unamkuta mtumishi anahujumu wazo jema kwa maendeleo ya nchi kwa kutanguliza, ama maslahi binafsi, au kuwa na chuki binafsi tu na mwenye wazo la maendeleo. Ni aina hii ya watumishi wenye kufanya kazi kwa misingi ya majungu na fitina tu, basi.

Ni imani yetu, Awamu hii ya Magufuli watumishi wa aina hii watapukutika kwa wingi waiache nchi yetu isonge mbele.

Maggid Mjengwa.

Iringa.
 
Ndugu zangu,

Kauli ya Rais John Pombe Magufuli akiwa Tanga juzi hapa ni ya kijasiri na yenye kumpambanua kama Kiongozi Mkuu wa Nchi.

Rais Magufuli amesikika akisema hivi;

" Kuna mambo ya ovyo ovyo na ya kipumbavu ndani ya Serikali."

Ni kauli ya kijasiri kwa Kiongozi Mkuu wa Nchi kuyasema hayo hadharani. Inahusu Serikali yake. Amefanya hivyo katika mantiki ile ya mficha maradhi kifo humuumbua.

Ukweli Rais amewasemea wengi anaowaongoza. Ni ukweli, kuwa Serikalini kuna watendaji wazuri wengi wenye mioyo ya uzalendo, lakini, wapo wachache wenye kufanya ya ovyo ovyo na ya kipumbavu mpaka mtu unajiuliza walipataje ajira.

Yaani, unamkuta mtumishi anahujumu wazo jema kwa maendeleo ya nchi kwa kutanguliza, ama maslahi binafsi, au kuwa na chuki binafsi tu na mwenye wazo la maendeleo. Ni aina hii ya watumishi wenye kufanya kazi kwa misingi ya majungu na fitina tu, basi.

Ni imani yetu, Awamu hii ya Magufuli watumishi wa aina hii watapukutika kwa wingi waiache nchi yetu isonge mbele.

Maggid Mjengwa.

Iringa.

Hapo kwenye red yaani unataka kutuaminishia kuwa wachache ndo wanojenga taswira ya mambo ya hovyo? Kwanini kama wanaofanya mambo ya hovyo ni wachache wasiondolewe tu(ye sio ndo mtaalamu wa kutumbua). Si pendi tumpe Rais vijisifa vya uwongo. Ukweli ni kuwa wanaofanya mambo ya hovyo wapo wengi(si wachache) tena sana ndo maana tunapata taswira ya serikali ya mambo ya hovyo.
 
Katika nchi yenye wapumbavu hutaweza kukosa wapumbavu walioweza kupanda na kushika hatamu za uongozi.

Bila shaka mheshimiwa Rais atawatumbua viongozi hao kadri wanavyoonesha upumbavu wao.
 
Ukitoa seasonal experienced kama Dr Mahiga na natural born leaders kama Selemani Jaffo (if you ask me seriously inabidi waanze kumuangalia baada ya Magufuli) waliobaki ni watu WA ovyo tu kwa namna moja ama nyingine ambapo utarajii miujiza yoyote kutoka kwao.
 
Wewe acha kubwabwaja tu na kuleta ushapiki wa kubiga debe,,hapo hajafika hata robo ya miaka miwili ushaanza kujikuna kuna je miaka mi5????kuweni na subra jamaa anajituma haasa
Ni kweli hakuna binaadam asie na kasoro lkn tuangalie kwanza na kuzipima kasoro zake,,
 
Jaffo bado sana.
 
Kiongozi anayewaongoza viongozi wapumbavu huku akiwa anawajua na yeye tumuiteje???
Na wanainchi wanaoongozwa na viongozi wapumbavu je na wao???
 
Ovyo ovyo ndio kiswahili cha wapi?

Sitegemei kuona mwandishi mkongwe kama wewe na msomi ambae umesoma enzi hizo elimu ikiwa elimu uandike kiswahili cha watoto wa divisheni faivu.
 
Ukitoa seasonal experienced kama Dr Mahiga na natural born leaders kama Selemani Jaffo (if you ask me seriously inabidi waanze kumuangalia baada ya Magufuli) waliobaki ni watu WA ovyo tu kwa namna moja ama nyingine ambapo utarajii miujiza yoyote kutoka kwao.

Umenigusa.Ninamtazama SULEIMAN JAFO kwa jicho la tatu.Huyu Bw. mdogo ni muda ndio utakaoongea. Namuomba Mungu anipe umri ili nimshuhudie.
 
Mm naona kulalamika haisaidii cha msingi ni Raisi kuchukua hatua. Wananchi Ndiyo tunaopaswa kumlalamikia yeye na sio yeye kulalamika
Kwa mfano baba analalamika kwa Watoto wake mambo mabovu anayoyafanya mama yao itasaidia nn? Na wakijua halafu inakuwaje? Chamsingi Mkuu Hao wameshindwa Kazi na kwa kuwa aliwateua yeye Basi awatengue DAWA si kulalamika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe acha kubwabwaja tu na kuleta ushapiki wa kubiga debe,,hapo hajafika hata robo ya miaka miwili ushaanza kujikuna kuna je miaka mi5????kuweni na subra jamaa anajituma haasa
Ni kweli hakuna binaadam asie na kasoro lkn tuangalie kwanza na kuzipima kasoro zake,,
Ushapiki, kubiga debe na subra we ni mtanzania kweli? Uhamiaji kamata huyu mtu
 
Ila naona bora angewatumbua tu kuliko kuwaita wapumbavu huku umewaacha kwenye madaraka yao. Kwanini aunde serikali ya wapumbavu?

Aweke utaifa mbele, ateue watu bila kujali itikadi zao mradi wana qualify na ni wazalendo.

Kazi ya kusema ni wapumbavu ni yetu wananchi na ndiyo uhuru wa kukosoa unapopata mantiki. Kazi ya kwake ni kutenda, maana kila mmoja akilalamika nani atatenda?
Mkuu afadhali umeweka sawa!! Bahati mbaya Mjengwa ni wa upande ule wa wapaka rangi!!hata kinyesi atakipaka chokaa kionekane ni jiwe la urembo.
 
Katika nchi yenye wapumbavu hutaweza kukosa wapumbavu walioweza kupanda na kushika hatamu za uongozi.

Bila shaka mheshimiwa Rais atawatumbua viongozi hao kadri wanavyoonesha upumbavu wao.
Fata upepo!cheering leader!
 
Kwa mfano yule Mhongo alishaonekana tangu enzi ya Kikwete hafai lakini alimteua! Hapo si haki kumuita Mhongo mpumbavu wakati alishafahamika alivyo na alishazembea katika awamu iliyopita. Vile ndivyo alivyo na wewe uliyemteua pia ulijua ni mzembe! Bado wapo watu wenye uwezo kama inawezekana mkuu awatumbue na kisha ateue wengine lakini awape nafasi ya kujipangia na kufanya mambo yao kwa Uhuru! Kwa sasa kuna aina fulani ya woga kwa kuwa mkuu anaonekana ndiye mpangaji na mwamuzi wa mambo mengi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom