Napiga zoezi pamoja na kujinyima kula lakini kitambi hakiishi, ila manyama uzembe Sina kwenye mbavu kushuka chini ya mbavu, ila katumbo haka hakaishi

Unajinyima kula au umepunguza kula carbohydrates?

Punguza Carbohydrates zidisha protein (matunda na mboga mboga), kama ratiba inaruhusu ongeza idadi ya milo kwa kuhakikisha unakula sio kushiba unakula kisela tu, baada ya muda tena unakula kisela hata ukila mara tano kwa siku sio mbaya.
 
Badilisha aina ya mazoezi... zingatia yanayoez kulifanya liwe flati. Ingia you tube utapata aina ya mazoezi yakulifuta
 
Punguza vyakula vya mafuta acha nyama nyama kula samaki ukizingatia mafuta tunayotumia yana koresto
 
Fanya mazoezi kila siku asubuhi na jioni kwa nusu SAA tu
Mlo wako uwe 75% mbogamboga na matunda
Hakikisha ndani ya masaa 24 umekunywa maji angalao lita 3-5
Ndani ya wiki 2 leta mrejesho
N:B DON'T SKIP A MEAL!
 
Tumia hii,sikuhizi wanauza hata wamachinga,ukitumia mwezi mmoja tu kila siku kitambi kinapotea..
Screenshot_20181111-063453.jpeg
 
Hili neno koresto sijawahi kulielewa
Koresto ni Cholesterol kwa neno la kiswahili ni Rehemu, kwa maneno rahisi ni kwamba Koresto ni aina ya mafuta(fats) yanayotengenezwa kwenye miili yetu (kwenye ini) na mengine tunayapata kwa kula vyakula kama nyama nyekundu, vyakula vya viwandani etc.
Sasa mafuta haya sio tatizo endapo yatakua ni kidogo mwilini, yakizidi ndio shida hutokea maana yananenepesha sehemu mbali mbali za mwili ikiwemo mishipa ya damu hivyo mishipa ya damu kupungua kipenyo, yaani kama mshipa wa damu ulikua ni mm 1 basi Koresto inaweza kuujaza ukawa ni chini ya mm1 inamaana damu itaanza kupita kwa kasi zaidi na kiasi kidogo (kwa maana ya blood volume), kama unavyokumbuka the small the area the higher the pressure, kwa mantiki hiyo moyo wako hautapata kiwango sahihi cha damu na oxygen kwa wakati muafaka, ubongo wako pia hautapata mahitaji hayo kwa wakati muafaka, madhara ndio utasikia heart attack, kwenye ubongo ndio utasikia stroke( mshituko, ndio utasikia mtu anakufa ghafla), kufua kuuma n.k

Namna gani utapelekea upate Koresto mbaya ni mtindo wako wa ulaji(chakula ikimaanisha kupenda vyakula vyenye mafuta kama nyama za kukaanga, chips n.k), kwa mfano watu wenye vitambi wana uwezekano wa kua na Koresto nyingi, watu wanene, wavuta sigara sana, watu wenye kisukari n.k

Nini ufanye sasa kuepuka koresto nyingi, kuzingatia ulaji wa vyakula visivyo na mafuta, kufanya mazoezi, kuacha sigara, kupunguza pombe, kula matunda, mboga mboga na nafaka.

Mimi sio daktari naomba niishie hapa, wenye fani zao watakuja kunirekebisha na kujazia palipopungua.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom