Napendekeza viti vyote kwenye mabasi ya mwendokasi ving'olewe ili kuongeza tija kwenye uendeshaji

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,009
40,680
Zibakishwe siti tatu tu kwa ajili ya wazee, wajawazito na wenye ulemavu, wengine wote wawekewe zile kamba na mabomba kwa ajili ya kujishika. Hii itaongeza mapato kwa kiasi kikubwa sana.
 
Zibakishwe siti tatu tu kwa ajili ya wazee, wajawazito na wenye ulemavu, wengine wote wawekewe zile kamba na mabomba kwa ajili ya kujishika. Hii itaongeza mapato kwa kiasi kikubwa sana.
WaTz kwa uharibifu, hatujambo. Je linatengenezwa kubeba uzito wa halaiki ya watu?
 
Jana nimetoka zangu kariakoo kama saa kumi hivi nikasema ngoja nikamate zangu mwendokasi (niunge juhudi na kulipa kodi)niwahi ubungo lengo niwahi basi la kwenda Tanga saa kumi na moja..wakati tunapandisha mlima wa magomeni pale karibu na kwa macheni (zamani) basi likaanza kufuka moshi kwenye engene.
Ilikua balaa..mbaya zaidi gari imejaa balaaa na milango ikajam ikawa haifunguki..watu wakaanza kuruka madirishani...nikasema oooh..ikabidi nijiongeze kwa namna nyingine niwahi safari yangu..btw sijaona unafuu wa ule mradi zaidi ya adhabu..aisee bora huku mkoani..
 
Back
Top Bottom