Napendekeza uchaguzi mkuu usifanyike mwaka huu, pesa zielekezwe kuimarisha demokrasia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Napendekeza uchaguzi mkuu usifanyike mwaka huu, pesa zielekezwe kuimarisha demokrasia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mag3, Mar 15, 2010.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Napendekeza uchaguzi mkuu usifanyike mwaka huu na badala yake pesa zilizotengwa zitumike kuimarisha misingi muhimu ya demokrasia kama kuwekeza zaidi katika elimu ya Uraia na kuandika katiba mpya. Ingawa ni miaka karibu ishirini tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi, serikali yetu na bunge letu bado vimeendelea kuendeshwa kama vitengo maalum vya chama tawala. Kwa maneno mengine CCM imeendelea kuwa mchezaji, mshika kibendera na mwamuzi ndani na nje ya uwanja wa siasa.
  Kwa hali hii uchaguzi hauna maana, ni kupoteza hela kwani mshindi wa kuchongwa ni a gone conclusion.
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Mar 15, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Uchaguzi usipofanyika wale wote waliokuwa madarakani kwa kuchaguliwa wanapoteza haki ya kuwepo madarakani sasa nani ataongoza hizo juhudi za kuimarisha demokrasia? Unless tupige kura kuwaongezea muda...
   
 3. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Best hizi pesa zikiwekwa elewa kuwa mafisadi watazitia kwapani na kutimka nazo. Best kuhusu demekrasia hata uchaguzi ukiahirishwa itakuwa bado tu. Jiandikisheni kwenye daftari la kudumu na mwezi wa kumi wapigeni chini mafisadi.
   
 4. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2010
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Wakenya naona wako kwa process ya kuibadili katiba yao. Sisi yetu inawekwa viraka kila kukicha, a hivyo viraka ni vile tu vinavyoiwezesha CCM kuzidi kuwepo madarakani.
   
 5. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #5
  Mar 15, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  naombeni kuuliza wakuu wakuu wangu mnieleweshe.
  siku zote tunasisitiziwa kupiga kura ili kuwachagua viongozi tunaowataka,lkn mie mwenzenu naomba nikiri kuwa huwa siamni kabisa kuwa kiongozi wa upinzani anaweza kumng'oa mgombea wa ccm kwa kumzidi kura.
  huwa naamni kuwa tunapiga kura tu kama wajibu lkn hazina nguvu yeyote.
  huwa naamini kuwa ccm ndio wenye nguvu za kuamua nani awe kiongozi lkn sio mpiga kura.
  je nina kosea kuamni hivi?
  kama ninakosea naomba mnieleweshe ni nani anayehakikisha kuwa CCM hawaadili matokeo ya kura.
  maana hata nikipiga kura huwa napiga kiunyoonge nikiwa naona nachafua dole gumba langu tu na wino wa mhuri.
   
 6. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #6
  Mar 15, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Waliopo madarakani wameonyesha kuwa hawana nia kabisa ya kuimarisha demokrasia, sana sana wangependa wazibe kabisa hata hako kadirisha kanakopitisha hako kahewa ka vyama vingi, hivyo hawatufai.
  Mwanakijiji, provisional government hapa ndipo mahali pake - utawala unapokwama na mabadiliko ya msingi lazima yafanyike. Tungeweza kufanya hivyo mwaka 1992 wakati tunaingia kwenye mfumo mpya lakini hatukufanya hivyo na matokeo yake pamoja na athari za kutofanya hivyo sasa zote zinatutafuna. Namna ya kuiunda hii provisional government ? - that is open to debate lakini hatutakuwa taifa la kwanza kufanya hivyo.
   
 7. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #7
  Mar 16, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Uchaguzi ni lazima ufanyike sio kosa la CCM kwamba tuliingia vyama vingi bila kubadilisha katiba ya chama kimoja, yalikuwa ni makosa ya waasisi wa vyama vya upinzani, wafadhili waliwalazimisha CCM kukubali vyama vingi, sasa ulikuwa ni wajibu wa wapinzani kulilia kubadilishwa katiba, they never did haya ndio matokeo!

  - Walipo kwenye power hawana ni ya kubadili anything kwa sababu wananchi hatujawaonyesha in a serious tone kwamba tunataka mabadiliko!


  FMEs!
   
 8. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #8
  Mar 16, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  uchaguzi ndio demokrasia yenyewe
  sasa usipofanyika,ndo demokrasia ipi hiyo????????
   
 9. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #9
  Mar 16, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Na hayo yote yata tekelezwa na serikali ya chama gani?
   
 10. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #10
  Mar 16, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  FMES CCM hawakulazimishwa na wafadhili kukubali vyama vingi walilazimishwa na vuguvugu la mabadiliko ya mfumo wa demokrasia na utawala mwishoni mwa miaka ya 80 kwa hiyo CCM isingeweza kubaki pekee kuendelea na mfumo wa chama kimoja wakati karibia nchi zote duniani zilikuwa kwenye mabadiliko hayo

  naomba nikusahihishe kidogo hayakuwa makosa ya waasisi wa vyama vya upinzani kukubali bila kubadili katiba bali yalikuwa ni makosa ya waasisi wa vyama vingi maana hata Nyerere pia ni mmoja wa waasisi wa vyama vingi na hakuwa chama cha upinzani, waasisi wa vyama vya upinzani walikuja baada ya CCM kuyakubali mageuzi kwa wakati huo usingetegemea mtu nje ya CCM kudai mabadiliko ya katiba bila kuitwa mhaini
   
 11. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #11
  Mar 16, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu CCM haikutaka vyama vingi, na mpaka sasa inaonesha hivyo. Vyama vingi lilikuwa ni wimbi ambalo liliikumba karibu kila nchi ya Afrika. CCM ilikataa kwa kuwa kura za maoni zilionesha asilimia 80 ya watanzania hawataki vyama vingi, lakini heababu za kisiasa za Nyerere zikawahimiza wakubali. Hata vyama vya upinzani kama NCCR mageuzi vilianzishwa na usalama wa taifa kucontain opposition, mpaka sasa kazi hiyo inaendelea kwa viwango tofauti. George Liundi alijaribu kusema lakini akanayamazishwa.

  Mentality ya CCM ni kuendela kutawala tu na kuhakikisha hakuna genuine opposition, na sio kuendeleza nchi. Having said that, ni lazima tukubali kuwa wananchi bado tuko kwenye mind set ya chama kimoja japo kuwa kisheria tuko kwenye vyama vingi, viongozi wa oppositin hawajakuwa serious kuhimiza mabadiliko ya katiba ili iwe ya kweli inayoendana na plural politics.
   
 12. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #12
  Mar 16, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ivi kwa nini tunawalaumu CCM kwa kutotaka vyama vingi? They are just responding to nature. Kumbuka siku zote kuwa power is corruptive. CCM imekaa madarakani, na kuona nguvu na uwezo unaokuja na hayo madaraka. Hivyo it's natural kwa CCM (kama chama) kupinga kwa nguvu zake zote mabadiliko yeyote yatakayo punguza na hatimaye kuondoa nguvu zake. Ndo maana nasema hichi ni kitu natural. Ni kama wanyama (hasa madume) wanavyochunga boma zao!! As long as they are the alpha-male (i.e.: they have the power)...they will use and do all means to resist any changes to maintain the dominant position!! Angalia nature documentary. We can actually learn a lot from animals...hasa in regards to our behavior and actions.
  Kwa hiyo CCM is doing what any other political party would do. (angalia kwingine kote duniani Russia included). Uzuri means wanazotumia ku-resist haya mabadiliko tunazifahamu:

  1. UJINGA
  kila siku ni zogo kuhusu malipo ya waalimu, alafu compare na malipo ya wabunge katika kikao kimoja bungeni. Angalia zile picha za shule (madarasa) Tz alafu compare na cost ya nyumba ya govenor wa benki kuu. Elimu ya juu bongo ni mapambano. Wanafunzi wanatoka chuo kikuu DSM hawana uwezo wa kufikiri nje ya box. They are trained to remain in the same system of thought.

  2. WIZI
  Wizi wa kura, Wizi wa mali za umma....

  3. RUSHWA
  Bunge lilikaa chini na kuidhinisha rushwa kwa kuipa jina tofauti - sijui takrimu!!!!!!

  4. VITISHO
  Nenda Tarime, kumbuka Znz 2000 na 2005.
   
 13. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #13
  Mar 16, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,890
  Trophy Points: 280
  Umemaliza kaka tatizo ni upinzani, hata mimi ningekuwa CCM nisingetaka kuondoka! CCM haitaondoka kwa maombi! kwa kujitoa na kugharamia

  Nchi hii siyo ya CCM! wala sio ya chadema, NCCR n.k ni ya wote watanzania!

  hakuna upigaji wakura wowote nchi hii utakaomake sense kama

  1. Hakuna mabadiliko ya katiba, katiba itakayo accomodate vyama vyote( serikali ya mseto) , serikali ya mseto inaamsha vyama na vyote vinakuwa active, sijui nani anakataa hili na sijui Zanzibar wameweza vipi

  2. Rais lazima apunguziwe madaraka, haiwezekani, jaji mkuu uteue wewe, mkuu wa polisi, jeshi, PCCB, n.k!!

  3. Tume ya uchaguzi iwe tume huru

  Tukifanya hayo tutakuwa tunajenga msingi mpya wa taifa jipya.

  Nashukuru umesema vyama vya siasa vimelala! sasa vyama vya siasa kama vinaingia kwenye chaguzi ili hali wakijua hayo hapo juu yanatakiwa, tuwaeleweje??

  Opportunity:

  Mwaka huu vyama vyote vya upinzani visusie uchaguzi kwa kulazimisha hayo mabadiliko. Tena tunawapa ushauri wakati mzuri kabisa, maana inaonekana mwaka huu mnajua kabisa mtashindwa, hata sisi mmetuaminisha hivyo. Hivyo basi, ili mwaka 2010 usipotee bure, na muwe na uzito sawa na CCM katika chaguzi zote zijazo, katiba lazima ipiganiwe.

  CCM kwa sababu wanawaza kuombaomba nje, nyie nanyi utangazieni ulimwengu kuwa hamtafanya uchaguzi mpaka katiba ibadilike! kimoyo moyo mnajua kabisa mkiingia kwenye uchaguzi mtashindwa! so why dont you think of taking this peace of advice?? kumbukeni dunia itawasupport kwa hili.

  we will be behind you!
   
Loading...