Napendekeza TZS 1000 kwa mtu mmoja ili Kivuko Cha Kigamboni kijiendeshe kwa faida! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Napendekeza TZS 1000 kwa mtu mmoja ili Kivuko Cha Kigamboni kijiendeshe kwa faida!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rich Dad, Jan 1, 2012.

 1. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #1
  Jan 1, 2012
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 742
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Watu wanalishana upumbafu humu JF! hivi mnajua gharama za kuendesha kile kivuko kwa siku ni kiasi gani? kuna mafuta, kuwalipa walinzi wa aina tatu ( Security Guards, Suma JKT, Polisi wa Kawaida), wafanyakazi wa dirishani na wale wanaochana ticket. Hapo bado hujawalipa madereva, hujapitisha askari na wanajeshi bure, wachilia mbali ticket fake zinazoingizwa pale na wakubwa.
  Sasa yote hayo ukiyaangalia inatoa picha ya kwamba TZS 200 haitoshi kabisa, napendekeza mtu mmoja bila kujali umri alipie TZS 1000. Kwa upande wa vyombo vyote vya moto viwango vianzie TZS5000 - TZ10,0000 ili kuisaidia serikali na wafanyakazi kuongeza mapato.
   
 2. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #2
  Jan 1, 2012
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  Mkuu ni maoni mazuri. Lakini mimi ningependekeza watu wasilipe kabisa, kusiwe na suala la biashara, sababu watanzania bado hatuna uwezo wa kuendesha public property. Dawa ni kujenga barabara tu pale, ikijengwa hakutakuwa na la kubabaisha. Ni ujinga hata kusikia waziri anakwenda kuzuia kupandishwa bei, as if hana kazi ofisini. kama kungekuwa na vivuko 1000 na vyote vingepandisha bei sijui kama angekwenda kwenye kila kivuko kusimamisha kupandisha bei.
   
 3. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #3
  Jan 1, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 12,747
  Likes Received: 1,515
  Trophy Points: 280
  Mkuu wangu mawazo mazuri lakini kumbuka hiyo ni huduma na si mradi wa kutoa faida. Pia mkuu hizo ticket fake unataka wananchi wazilipie? Huoni hapo kuna mwanya wa kuvujisha mapato?
   
 4. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #4
  Jan 1, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 29,251
  Likes Received: 4,239
  Trophy Points: 280
  hata mlipe 10,000 kama uthibiti wa mapato ni mbovu haitosaidia.
   
 5. Lasikoki

  Lasikoki JF-Expert Member

  #5
  Jan 1, 2012
  Joined: Jan 10, 2010
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Duh! Mtoa mada mbona hueleweki? Yaani wewe jawabu la kukabiliana na tiketi feki ni kupandisha nauli, au kuajiri wana-usalama/askari wa aina 3 tofauti ambao pengine hawahitajiki ni kupandisha nauli mpaka 1,000/..........je wafahamu idadi ya watanzania wanaoishi chini ya dola moja na kwamba usafiri wa kuvuka upande mmoja kwa kivuko kwa sh 1,000 ni anasa and almost impossible. I thought ungekuja na idea ya kutolipia kabisa

  Unatuachia maswali mengi kuliko majibu NA pengine tuanze kuja na theory mbalimbali ili kujaribu kujibu baadhi ya maswali. One of the theory ni kwamba WEWE MWENYEWE INAWEZEKANA NDIE MLETA/MKATA TIKETI FEKI sasa unataka bei ipandishwe ufaidi vizuri.

  Hakika ninyi na ufisjdi wenu iko siku laana zetu zitawakuta
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Jan 1, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,014
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Kwa nini tunalipa kodi? Nilidhani kuwa kodi zetu ndizo zilipaswa kushughulikia haya mambo unayoyaorodhesha hapa. Basi kama ni hivyop serikali ifute kodi halafu tulipe hiyo nauli wanayoitaka. haiwezekani tulipe kodi kwa ajili ya kuiwezesha serikali kugharamia huduma za jamii, halafu huduma hizo hizo zitolewe kwa bei ya juu
   
 7. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #7
  Jan 1, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,134
  Likes Received: 1,450
  Trophy Points: 280
  Asanteee!
  Heri ya mwaka mpya, hongera kwa kugoma kulishwa pumba na mtoa mada
   
 8. Mr Suggestion

  Mr Suggestion JF-Expert Member

  #8
  Jan 1, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 605
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 60
  Suluhisho la kigamboni ni electronic gates tu, Uwanja wa ndege getini yupo mtu mmoja tu tena wakati wa kutoka, hakuna sababu ya kuwa na watumishi wengi kwenye kile kivuko, hasa yule mdada wa matangazo kwani hawawezi kurecord sauti ya mtu kisha wakawa wanaplay kila wanapofika upande wa pili. Kimsingi mtanzania kila kitu kwa vitendo ni 0% ila theory 100%
   
 9. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #9
  Jan 1, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,163
  Likes Received: 466
  Trophy Points: 180
  hivi we mleta thread unakatisha ticket nini na wewe kwa hiyo unataka mshahara wako upande eh wewe ukiwa pale unalipwa na nani na serikali au na kivuko? Hata hiyo nauli ingetolewa watu wapande bure
   
 10. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #10
  Jan 1, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 12,747
  Likes Received: 1,515
  Trophy Points: 280
  Mkuu unaweza kutuambia kwa siku kivuko kinavuna shilingi ngapi na matumizi ni kiasi gani? Hao wakubwa wanaoleta ticket fake kwa nini wasiripotiwe kwenye vyombo vya ulinzi na usalama. Kama kun ticket fake toka kwa wakubwa ni hakika pia kuwa kuna ticket fake toka kwa wadogo; kwa maana hiyo asilimia zaidi ya hamsini ya ticket zinazotolewa ni fake na hivyo mapato kuingia mifukoni mwa wajanja.

  Hayo makundi yote ya walinzi ya nini? Polisi si wanalinda mali ya serikali wanalipwa nini kama wako kazini kama kawaida? Au ni posho?
   
 11. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #11
  Jan 1, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 12,747
  Likes Received: 1,515
  Trophy Points: 280
  Tunatengeneza ajira mkuu!
   
 12. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #12
  Jan 1, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,895
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kijana hujui unachoandika.
  Ni vizuri ukafanya research kwanza kabla hujaandika.
   
 13. u

  utantambua JF-Expert Member

  #13
  Jan 1, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Rich Dad unatoka katika Rich Family kwa sababu wewe ni wa Rich Clan na una Rich Kids so Una Rich Money unaweza kulipa Rich Fare na kuishi Rich Life. Mnataka kutukomoa tuishio Kigamboni?
   
 14. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #14
  Jan 1, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,800
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  hebu tuwekee mahesabu sahihi, KUNA JUMLA YA WAFANYAKAZI WANGAPI? MATUMIZ MENGINE YANAGHARIM SH. NGAPI? KUNAVUKA WASTANI WA BINADAMU WANGAPI KWA SIKU? MAGARI MAKUBWA NA MADOGO YANAVUSHWA MANGAPI KWASIKU?
   
 15. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #15
  Jan 1, 2012
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 792
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Eleza kuendesha kivuko gharama yake ni kiasi gani kwa siku? Na mapato yanayokusanywa ni kiasi gani? Siyo kusema tunalishana upumbavu toa figure tuanze kujadili ongezeko lenye tija ni kiasi gani?
   
 16. aikaruwa1983

  aikaruwa1983 JF-Expert Member

  #16
  Jan 1, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 1,272
  Likes Received: 1,024
  Trophy Points: 280
  maadam lengo ni kukusanya mapato sawa buku tutoe ila mimi mkazi wa mbutu pantoni linipeleke mpaka home.....
   
 17. K

  Kubingwa JF-Expert Member

  #17
  Jan 1, 2012
  Joined: Apr 23, 2010
  Messages: 502
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Vyombo vyote vya moto,hata mabasi ya mikoani,teh teh teh.Kweli wewe unatupenda watz
   
 18. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #18
  Jan 1, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 55,309
  Likes Received: 16,702
  Trophy Points: 280
  Unafikiri daraja ndio litakuwa la bure?? wa Mombasa hunena "unlala".
   
 19. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #19
  Jan 1, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,007
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 160
  hivi mtoa mada unakaa kigamboni?
  kama sivo unajua ugumu wa maaisha kwa mwananchi wa kawaida? mfano mwl alipe 1000 asbh na jioni jumla kwa mezi sh 60,000 kwa mwezi,mshahara wake 120,000
  'je nauli ya daladala? kodi,matumizi ya ndani atajimuduje?
  hicho kivuko ni huduma tu kwa wananchi sawa na ilivo umeme tunalipa bil lakini hazitoshi kukidhi uendeshaji wa tanesco ndio maana
  serikali inagharamia ili ijiendeshe
  unapotoa pendekezo kama hivo wazia mwananchi wa kawaida atajimuduje
  bila shaka ww ni mmoja wa wanaofaidikia na hicho kivuko.
  suluhisho ni daraja peke yake,
   
 20. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #20
  Jan 1, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 7,410
  Likes Received: 212
  Trophy Points: 160
  ukitaka kumchanganya muongo mwambie akupe hizo data!
   
Loading...