Napendekeza TCRA wapige marufuku matangazo ya BBC nchini Tanzania. Wameitukana kumbukumbu ya Mwl. Nyerere

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
35,835
40,431
Eti wameonyesha kipindi cha historia ya ukombozi wa Afrika, ambapo wametaja wapambania uhuru kama akina Kwame Nkrumah, Patrice Lumumba na Nelson Mandela, Jomo Kenyatta miongoni mwa wengi.

Lakini cha ajabu walipofika kwenye ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika wameishia kumtaja Mandela tu na kuishia hapo. Yaani Julius Kambarage Nyerere, pamoja na mchango wake mkubwa katika ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika, hajatajwa hata kwa bahati mbaya, hii maana yake nini??!

Wanasema ‘A TRUTH HALF TOLD IS A LIE’, kwa kukaa kimya ni kukubali matusi ya nguoni juu ya baba wa taifa letu. Ngoja nipunguze jazba kwanza..., daah!!!
 
Hilo si la kustaajabisha kuhusu BBC inapokuja kwa Mwl Nyerere hata matangazo wakati wa kifo chake yalijaa kejeli na lawama, Mwl hakuwahi kuwaramba miguu hawa wajinga.

Kinachotushangaza wengi ilikuwaje wakati wa kuumwa kwake akakubali kwenda kutibiwa kwenye hospitali ya adui wake??!! Hii ilishangaza sana!!! Najaribu kupata picha Mwl kalazwa kwenye hospital Uingereza kwa mbaya wake. Mwl alijua mtizamo wa Mwingereza kwake sijui kama alikuwa naïve kudhani akiwa taabani basi mahala pa kukimbilia ingekuwa Uingereza!

Lakini hii yote mitazamo tu, tunasema kwa kutumia akili ya kuzaliwa tu na mtizamo wa haraka haraka. Ingawa ukweli unabaki Mwingereza hakuwahi kuwa Rafiki wa Mwl Nyerere kivileee.
 
Habari ni sawa na chakula mezani.

Mtazamaji/mskilizaji ataamua kuikubali au kuikataa na kukipongeza au kukidharau chanzo/chombo cha hiyo habari.

Kuwafungia hakutawazuia kuendelea kututangaza vibaya endapo wamedhamiria kufanya hivyo.
 
Sijui kuna shida gani kuhusu recognition kwa Mwl. Nyerere.

Wewe unashangaa kuhusu BBC wakati AU yenyewe walikua hawana chochote kinachomtambulisha kama aliwahi kua kiongozi wa mstari wa mbele katika ukombozi wa Afrika hadi pale Robert Mugabe alipowasuta wenzake kwa kuwaambia sio fair kumsahau Nyerere ndio angalau wakajitoa na kuupa ukumbi mpya jina lake!
 
si hilo tu huku Tanzania utakuta kuna barabara ya sam Nojuma sijui shule Mugabe sijui chuo cha Mandela sijui barabara ya Kwame Nkurumah sasa nenda huko walikosaidiwa kupata uhuru na Tanzania hata mtaa wa Kambarage hakuna 🤣 tatizo sisi kiherehere,kimbelembele chetu muda wa kuijenga nchi yetu eti tunawasaidia wasio na shukrani wapate uhuru na tulikuwa tunawasongea hata ugali washibe
 
Dunyua,

Kipindi cha jaribio la kwanza la kumpindua Nyerere mbona Muingereza aliingilia kati kumnusuru Nyerere?
 
Sifa upewe siyo ujipe. Nimegundua tulifungiwa kwenye box kwa muda mrefu na mi FISI M, tukiwa kwenye box tuliaminishwa hayo, ya Nyerere, Nyerere, Nyerere.

Sasa ukitoka nje masikioni unasikia Nyerere, Nyerere, Nyerere. Akili ikikukaa sawa sauti zile zinapotea, ukiona husikii Nyerere, jua sasa akili iko sawa. Yani yale maluweluwe hayapo tena.

Wale walijikomboa wenyewe sio kwamba Nyerere aliwakomboa.

Nchi imekuwa ya chama kimoja muda mrefu, na stori zilikuwa hizo za ma FISI M, sasa kuna masauti mengi.

Hizo habari za Nyerere zinakosa muelekeo na support.

Tusilazimishe sifa, kama zipo zetu tutapewa, lakini tusiwalazimishe kutoa sifa kwetu, pengine hatustahili.

Ukitaka sifa za Nyerere mtafute Kabudi, mtakesha akikutajia Nyerere.
 
si hilo tu huku Tanzania utakuta kuna barabara ya sam Nojuma sijui shule Mugabe sijui chuo cha Mandela sijui barabara ya Kwame Nkurumah sasa nenda huko walikosaidiwa kupata uhuru na Tanzania hata mtaa wa Kambarage hakuna 🤣 tatizo sisi kiherehere,kimbelembele chetu muda wa kuijenga nchi yetu eti tunawasaidia wasio na shukrani wapate uhuru na tulikuwa tunawasongea hata ugali washibe
Nasikia kweli tulikuwa tunawapikia ugali kule morogoro, wanakula wanashiba na mapmbano tunaendelea nao bega kwa bega, leo wanajidai hawamjui Nyerere??!!
 
Soma kwanza 1964 mutiny kisha uongee hizo pumba. Bila huyo muingereza, nyerere si angekaa madarakani miaka 3 tu na kung'olewa.
 
Habari ni sawa na chakula mezani.

Mtazamaji/mskilizaji ataamua kuikubali au kuikataa na kukipongeza au kukidharau chanzo/chombo cha hiyo habari.

Kuwafungia hakutawazuia kuendelea kututangaza vibaya endapo wamedhamiria kufanya hivyo.
Hivi fungafunga ya vyombo vya habari haitatuacha salama.
 
Nimetoka kushuhudia ushenzi wa hali ya ya juu toka kwa hawa muda huu. Eti wameonyesha kipindi cha historia ya ukombozi wa Afrika, ambapo wametaja wapambania uhuru kama akina Kwame Nkrumah, Patrice Lumumba na Nelson Mandela, Jomo Kenyatta miongoni mwa wengi.

Lakini cha ajabu walipofika kwenye ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika wameishia kumtaja Mandela tu na kuishia hapo. Yaani Julius Kambarage Nyerere, pamoja na mchango wake mkubwa katika ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika, hajatajwa hata kwa bahati mbaya, hii maana yake nini??!

Wanasema ‘A TRUTH HALF TOLD IS A LIE’, kwa kukaa kimya ni kukubali matusi ya nguoni juu ya baba wa taifa letu. Ngoja nipunguze jazba kwanza..., daah!!!
Pia nashauri TCRA waifungie TBC na Channel 10 kwa kuonyeha habari kwa upendeleo
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom