Napendekeza TCRA wapige marufuku matangazo ya BBC nchini Tanzania. Wameitukana kumbukumbu ya Mwl. Nyerere

Dunyua,

Kipindi cha jaribio la kwanza la kumpindua Nyerere mbona Muingereza aliingilia kati kumnusuru Nyerere?

Mkuu Coscated
Wakati naandika Kuchangia uzi huu nilikumbuka hilo la Waingereza kumsaidia Mwl wakati wa Uasi ule wa wanajeshi wetu. Si rahisi kusema kwanini Waingereza walimsaidia wakati ule lakini nikiangalia juu juu naweza sema miaka ile ambayo ilikuwa mwanzoni mwa 1960, haikuwa rahisi kumtambua Mwl na misimamo yake. Nafikiri sijui ingekuwaje kama mapinduzi yale yangekuja baada ya Azimio la Arusha au hata baada ya miaka ya kati ya 70 wakati mapambano ya Kusini mwa Afrika yamepamba moto.

Naweza sema baadae sidhani kama Waingereza waliendelea kuwa na mapenzi na Mwl ingawa mahusiano ya kibalozi yaliendelea. Mwl alikuwa mwiba kwenye makalio ya Mwingereza kwa muda mrefu sana.
 
Sifa upewe siyo ujipe. Nimegundua tulifungiwa kwenye box kwa muda mrefu na mi FISI M, tukiwa kwenye box tuliaminishwa hayo, ya Nyerere, Nyerere, Nyerere.

Sasa ukitoka nje masikioni unasikia Nyerere, Nyerere, Nyerere. Akili ikikukaa sawa sauti zile zinapotea, ukiona husikii Nyerere, jua sasa akili iko sawa. Yani yale maluweluwe hayapo tena.

Wale walijikomboa wenyewe sio kwamba Nyerere aliwakomboa.

Nchi imekuwa ya chama kimoja muda mrefu, na stori zilikuwa hizo za ma FISI M, sasa kuna masauti mengi.

Hizo habari za Nyerere zinakosa muelekeo na support.

Tusilazimishe sifa, kama zipo zetu tutapewa, lakini tusiwalazimishe kutoa sifa kwetu, pengine hatustahili.

Ukitaka sifa za Nyerere mtafute Kabudi, mtakesha akikutajia Nyerere.
Kuna kujisifu na pia wananchi tuliyoyashuhudia kwa macho. Kulikuwa na makambi ya nchi ngapi hapa Tz zilizokuwa zikipigania uhuru wao? Hiyo nayo ni uongo?
 
Hilo si la kustaajabisha kuhusu BBC inapokuja kwa Mwl Nyerere hata matangazo wakati wa kifo chake yalijaa kejeli na lawama, Mwl hakuwahi kuwaramba miguu hawa wajinga.

Kinachotushangaza wengi ilikuwaje wakati wa kuumwa kwake akakubali kwenda kutibiwa kwenye hospitali ya adui wake??!! Hii ilishangaza sana!!! Najaribu kupata picha Mwl kalazwa kwenye hospital Uingereza kwa mbaya wake. Mwl alijua mtizamo wa Mwingereza kwake sijui kama alikuwa naïve kudhani akiwa taabani basi mahala pa kukimbilia ingekuwa Uingereza!!!

Lakini hii yote mitazamo tu, tunasema kwa kutumia akili ya kuzaliwa tu na mtizamo wa haraka haraka. Ingawa ukweli unabaki Mwingereza hakuwahi kuwa Rafiki wa Mwl Nyerere kivileee...
Mwenye hii kesi ameshaenda kuijibu mkuu
 
Kuna kujisifu na pia wananchi tuliyoyashuhudia kwa macho. Kulikuwa na makambi ya nchi ngapi hapa Tz zilizokuwa zikipigania uhuru wao? Hiyo nayo ni uongo?
Ungezitaja sio uniulize mimi, nyie ndio mnatafuta sifa.

Hivyo yale makambi kigoma na ngara nayo utasema ni ya wapigania uhuru?!

Wakimbizi sio wapigania uhuru, mkikataliwa msilazimishe.
 
Babu mchonga meno aliwabania rasilimali za nchi hajawah wasujudia mabeberu viva forever mwl Nyerere continue to rest in eternal peace
 
Dunyua,

Tambua, aliyempeleka London ni yule aliesaini mikataba ya madini mwaka 1999 punde tu baada ya kifo cha Baba wa Taifa

Francis Da Don

Kabisa Aisee yaani ilikuwa kama kusema "mi naweza saini mikataba hiyo lakini kuna kizingiti, tukitoa hicho itakuwa poa sana"
Na baada ya kizingiti kutoka, kweli ikawa!!! Kutoka hapo Shamba la Bibi.
Tanzania itakuja siku watu watabidi wajibu maswali magumu sana hata kama watakuwa wametangulia mbele za haki.

Tunafahamu kuwa hawa Wakuu wengine wa nchi zetu hizi Afrika huwa wako kwenye orodha za malipo (pay roll) za mashirika ya nje ya kijasusi. Wananchi wanaweza kudhani kiongozi fisadi tu au mwenye tamaa ya kujilimbikizia mali kumbe kwa upande wa pili yuko kwa manufaa mapana ya nchi Fulani kupitia mashirika nguli ya kijasusi. Ipo siku mengi yanaweza kufukuliwa kwenye hili.

Na iwe kama alivyojibu rais wa USSR wakati ule Nikita Khruschev kwenye miaka ya 1960 akitoka kuonana na Fidel Castro alipoulizwa kama anajua Castro ni Mkomunisti Nikita alijibu " Sijui kama Castro ni Mkomunisti lakini najua kuwa mimi ni Fidelista"

Na tuombee WaTanzania wote na vizazi vijavyo wote tuwe Nyereresta, kwa maana kuzienzi fikira na msimamo na ndoto nzuri za Baba wetu wa Taifa wa Taifa lenye kujitegemea.
 
Hilo si la kustaajabisha kuhusu BBC inapokuja kwa Mwl Nyerere hata matangazo wakati wa kifo chake yalijaa kejeli na lawama, Mwl hakuwahi kuwaramba miguu hawa wajinga.

Kinachotushangaza wengi ilikuwaje wakati wa kuumwa kwake akakubali kwenda kutibiwa kwenye hospitali ya adui wake??!! Hii ilishangaza sana!!! Najaribu kupata picha Mwl kalazwa kwenye hospital Uingereza kwa mbaya wake. Mwl alijua mtizamo wa Mwingereza kwake sijui kama alikuwa naïve kudhani akiwa taabani basi mahala pa kukimbilia ingekuwa Uingereza!

Lakini hii yote mitazamo tu, tunasema kwa kutumia akili ya kuzaliwa tu na mtizamo wa haraka haraka. Ingawa ukweli unabaki Mwingereza hakuwahi kuwa Rafiki wa Mwl Nyerere kivileee.
Usisahau na misaada pia hua mnaomba na kupokea kutoka kwake
 
Kunywa maji mtoto na uende shule. Achana na mambo yasiyokuhusu. Utasubiri sana BBC wafungiwe.
 
Unamtetea Nyerere huyuhuyu aliyetuachia katiba hii na sheria ya kumpa authority DC ya kumweka lockdown mbunge wa upinzani?
 
Mwenye hii kesi ameshaenda kuijibu mkuu
Inavyoonekana mwaka 1999 kulikuwa na mkakati kabambe ulishaandaliwa, maana mzee alivyong’ata shuka tu, mwaka huo huo ilisainiwa mikataba kichaa ya madini mfululizo, hadi Lissu akawa anaipigia kelele, JPM ndio akaja kuifumua
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom