FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 36,052
- 40,715
Huwa inashangaza sana katika zama hizi za kukua mno kwa teknolojia kukuta taa za barabarani zinaita upande usio na magari kabisa hata dakika 2, wakati huo huo upande mwingine wenye msururu mrefu wa magari ukiwa umezuiwa kwa taa nyekundu, huwa nacheka sana.
Ninachojiuliza, kama simu yangu ya mkononi kupitia app kama ‘google map’ inaweza kuniambia ni barabara ipi ina foleni muda huu na nikaweza kuikwepa hiyo barabara, iweje taa za kuongozea magari zishindwe kutambua ni upande upi una magari mengi hivyo uitwe zaidi kuliko upande mwingine?
Kipindi cha nyuma hata kabla ya kukua kwa teknolojia ya Satellite navigation, bado hizo taa zingeweza kufungwa cameras na motion sensors (tochi) ili kujua upande upi uitwe na uoande upi uzuiwe, ila kwa sasa tuna faida ya ziada, kuna teknolojia ya ‘live map’ kama ‘google maps’ ambayo inakupa live feed ya upande gani una magari kiasi gani, hizi teknolojia zote zikiwa ‘integrated’ kwenye mfumo wa kuongozea magari nadhani tutaoiga hatua kubwa sana.
Faida nyingine kubwa ni uwezo wa taa za Junction ‘A’ kuwasiliana na taa za Junction ‘B’ ili kupitia a logical ‘Algorithm’ ziweze kuita magari kwa ‘Coordination’, haileti maana kwamba taa za makutano ‘A’ zimeruhusu wakati less than 100 meters Kuna junction ‘B’ imezuia magari, utaahira wa wapi huu?
Naomba niishie hapa, mbona hata UBER car service wanatumia ‘google maps’ kwenye mifumo yao? Nyinyi mnashindwa nini, mnakwama wapi?
==========================
Update: 04/04/2024

Rais Samia: Ili kudhibiti rushwa barabarani, trafiki waondoke barabarani, kamera na taa ndio zifanye kazi
Rais Samia ameagiza kuanza kuondolewa Kwa Matrafiki ambao walijigeuza Wala Rushwa Barabarani badala yake ametaka zifungwe Kamera na Taa Ili Kuongoza magari. --- Rais Samia Suluhu Hassan amesema katika kukabiliana na rushwa nchini, trafiki barabarani wanapaswa kuondolewa badala yake taa na...
www.jamiiforums.com