Napendekeza taa za kuongozea magari ziunganishwe na mifumo ya ‘Google maps’

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,059
40,722
Huwa inashangaza sana katika zama hizi za kukua mno kwa teknolojia kukuta taa za barabarani zinaita upande usio na magari kabisa hata dakika 2, wakati huo huo upande mwingine wenye msururu mrefu wa magari ukiwa umezuiwa kwa taa nyekundu, huwa nacheka sana.

Ninachojiuliza, kama simu yangu ya mkononi kupitia app kama ‘google map’ inaweza kuniambia ni barabara ipi ina foleni muda huu na nikaweza kuikwepa hiyo barabara, iweje taa za kuongozea magari zishindwe kutambua ni upande upi una magari mengi hivyo uitwe zaidi kuliko upande mwingine?

Kipindi cha nyuma hata kabla ya kukua kwa teknolojia ya Satellite navigation, bado hizo taa zingeweza kufungwa cameras na motion sensors (tochi) ili kujua upande upi uitwe na uoande upi uzuiwe, ila kwa sasa tuna faida ya ziada, kuna teknolojia ya ‘live map’ kama ‘google maps’ ambayo inakupa live feed ya upande gani una magari kiasi gani, hizi teknolojia zote zikiwa ‘integrated’ kwenye mfumo wa kuongozea magari nadhani tutaoiga hatua kubwa sana.

Faida nyingine kubwa ni uwezo wa taa za Junction ‘A’ kuwasiliana na taa za Junction ‘B’ ili kupitia a logical ‘Algorithm’ ziweze kuita magari kwa ‘Coordination’, haileti maana kwamba taa za makutano ‘A’ zimeruhusu wakati less than 100 meters Kuna junction ‘B’ imezuia magari, utaahira wa wapi huu?

Naomba niishie hapa, mbona hata UBER car service wanatumia ‘google maps’ kwenye mifumo yao? Nyinyi mnashindwa nini, mnakwama wapi?

==========================
Update: 04/04/2024

Kibongo bongo bado sana. Acha matrafiki wwendelee kudeal na foleni za hapa jijini.

Maana kama ingekuwa kulitatua tatizo basi ingeshaweka centralized system ya kuruhusu uongozaji wa magari kama ulivyoainisha kisha kugawa hiyo feed kwa live map systems kama za google.

Kama inawezekana kutrack magari yanayodaiwa faini wanashindwa nini kuimplement hili suala?
 
Mkuu nimewahi pia kuwaza kama wewe siku moja foleni ilipokua kali sana pale mataa ya Kamata kutokea mjini

Wazo mbadala, hivi App developers hawawezi kutengeneza app itakayotoa live feed ya foleni barabaran ili kama barabara A iko overloaded basi watu watumie barabara B

Kwamfano kwa siku za karibuni Barabara ya Kawawa (Morroco to Ilala Boma) imekua nyeupe sana wakati wa jioni, muda huo huo Barabara ya Nyerere kuna kamba balaa ikihusisha magari kutoka maeneo ya Mikocheni, kama App ingekuwepo hawa wangepitia Kawawa na kupunguza foleni pale mataa ya Kamata
 
Utakuta traffic wa mataa ya Kamata karuhusu gari zinazotoka mjini kuelekea Mfugale kupita kisha yule wa mataa ya Changombe kazuia anaruhusu gari zinazotoka Ilala kwnd temeke
Vurugu tupu asee
Yaani hakuna coordination kabisa, hata radio call tu wanashindwa kutumia kwa ajili hiyo?
 
Badala ya tambo na kujichekesha fanya wewe hiyo teknolojia Kama unaona ni rahisi Kama theory zako ,peleka wazo kwenye tume ya sayansi na teknolojia utapewa fedha za mradi.
 
Badala ya tambo na kujichekesha fanya wewe hiyo teknolojia Kama unaona ni rahisi Kama theory zako ,peleka wazo kwenye tume ya sayansi na teknolojia utapewa fedha za mradi.
Mimi ndie namiliki barabara za Tanzania? Wapo watu wanalipwa kila siku kwa ajili ya kazi hii, wameajiriwa kabisa. Halafu urahisi au ugumu ni relative, ila relatively ni rahisi.
 
Ni rahisi kwa nani? Kwangu mimi si rahisi
Hapo uliposema wanatumia kilevi gani,nikwambie kitu bloo,hizi foleni ni dill za watu wanaomba dua ziendelee,kuna trafic wanazuia magari buguruni mandela road,magari ya kuyoka ubungo yanazuiwa kijanjsc ili itokee foleni utsnue wakukamate wakutoe upepo
 
Sawa, kilevi kinaitwa Rushwa, wahusika wafanyie kazi
 
Back
Top Bottom