Napendekeza siku ya kumbukumbu ya Hayati Jemedari Dkt. Magufuli iadhimishwe sambamba na mashujaa hawa wa kizalendo nchini

Generalist

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
4,327
2,000
Kama kuna Maamuzi ambayo Generalist Mimi nitayafurahia na nitazidi Kumpenda (Kumkubali) Rais wangu Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan, Serikali yake na Chama chake (changu) cha CCM ni kama akiliamua hili lifuatalo.

Kwamba tarehe ya Kumbukumbu (Kumbukizi) ya Kifo cha Rais Hayati Dkt. Magufuli iendane pia na Kuwakumbuka 'Wazalendo' wa 'Wanyonge' akina Ben Saanane, Azory Gwanda, Akwilina Akwilina, Alphonce Mawazo na Kupigwa Risasi za Kuuwawa kwa Tundu Lissu.

Rais Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan najua (tena kwa Kujiamini kabisa) kuwa Wewe binafsi, Gerson Msigwa, Dkt. Abbas na Hamphrey Polepole huwa 'mnanisoma' mno (24/7) Generalist hapa JamiiForums hivyo Ombi langu hili mtalipokea, mtalifanyia Kazi na huenda mkalikubali pia na Mwakani likaanza.
 
petro matei

JF-Expert Member
May 11, 2014
640
1,000
Kwa ninavyofahamu sikukuu ya kitaifa ni nyerere day na karume day kwa sababu ni wahasisi wa taifa.

Viongozi wengine wanakumbukwa kama karume day bila mapumziko.

Ila kama itapendeza naye Hayati magufuli siku kumbukumbu yake kukawa na mapumziko ni jambo jema kwa Shujaa wetu
 
Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
6,423

Huu ni wehu ujue 😀😀😀
 
Miss Madeko

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
4,036
2,000
Kwa ninavyofahamu sikukuu ya kitaifa ni nyerere day na karume day kwa sababu ni wahasisi wa taifa.

Viongozi wengine wanakumbukwa kama karume day bila mapumziko.

Ila kama itapendeza naye Hayati magufuli siku kumbukumbu yake kukawa na mapumziko ni jambo jema kwa Shujaa wetu

Shujaa wako na nani? Si bora tumpe hiyo heshima hayati Benjamen William Mkapa. Magufuli hana anachoweza kupewa hiyo heshima kamwe
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom