Napendekeza rasmi jina la ufupisho la mama liwe SASHA

safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
11,161
15,836
Wakuu napendekeza jina rasmi la mama yetu mpendwa Samia Suluhu Hassan liwe SASHA kama ambavyo watangulizi walikuwa na ufupisho.

Hayati Magufuli aliitwa kwa kifupi JPM yaani John Pombe Magufuli.

Mzee Kikwete aliitwa JK yaani Jakaya Kikwete.

Sasa na mama naomba Tumuite SASHA ikimaanisha
SA = Samia
S = Suluhu
HA = Hassan.

Hii SASHA ni rahisi kuitamka na kuiandika kulika SSH ambayo ni ngumu kuitamka na haileti utamu ule wa uwepesi kama Jeikei ama Jeipiem.

mama SASHA oyeeeee.
 
Kama hatojali, napendekeza Rais wetu akubali tutumie jina lake la kwanza "Samia"....ni fupi, rahisi na zuri pia.
 
Unataka kumpa mama jina la kutunga!!!?
wacha zako mama ni SSH
Inaonekana unaamini sana katika majina kumcontrol mtu.

Nipende kukupa maneno ambayo ndugu Obama aliyasema katika moja ya hotuba zake kali sana.

Alisema ya kuwa "your name is not a barrier to success"
 
Kwa JPM tulipaswa kumwita JOPOMA au sio?
JO: John
PO: Pombe
MA: Magufuli
Kwa sababu kifupi cha magufuli kilifiti na kuwa rahisi hata kutamkwa yaani jpm ndio maana haikutumiwa jopoma hahahah
 
Back
Top Bottom