FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 37,898
- 43,802
Kumbe toka 2004 tulikuwa tuna haki ya kimkataba ya kuachana na hili jinamizi, lakini mtu anapendekeza kutuhonga punguzo la Capacity Charges toka billioni 5.2 mpaka billioni 2.6 ili tusiitumie ile haki yetu ya kimkataba ya kuachana nao, kwakuwa mpaka leo hawa IPTL wapo, inamaana huyo alieombwa alikubali kwa maslahi yake binafsi badala ya kuangalia utaifa. Sasa huyo alieomba na huyo alieombwa, wanyongwe wote kwa presidential decree.
=====================================
UPDATE: Rais JPM ameagiza mawaziri waliohusika na utiaji saini mikataba ya kinyonyaji ya madini na ACACIA iliyopelekea upotevu wa matrillioni washughulikiwe kwa mujibu wa sheria. Waziri mwenyewe ndio huyo Daniel Yona anaetajwa kwenye hiyo document. Kwakuwa pia amehusika kulitia hasara taifa kupitia IPTL, nazidi kutilia mkazo anyongwe kwa makosa yote mawili
=======================================
UPDATE: (19/06/2017)
Baada ya kutoa malalamiko haya dhidi ya VIP engineering na IPTL, TAKUKURU wameanza kuchukua hatua.Nazidi kutilia mkazo wanyongwe kwa presidential decree
TAKUKURU yawafikisha mahakamani Harbinder Sethi na James Rugemalira kwa kosa la Uhujumu uchumi
======================================
UPDATE: 17/07/2017
Mitambo IPTL yazimwa, wakwama kufanya biashara ya umeme
Hatua hiyo imekuja baada ya kukwama kwa maombi ya kuongezewa muda wa miezi 55 ya leseni yake ya uzalishaji umeme kutokana na kusubiri uamuzi wa Ikulu.
Hali hiyo inajitokeza wakati mmiliki wa Kampuni ya Pan Africa Power (PAP) Harbinder Singh Sethi na Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering, James Rugemalira wakiwa tayari wamefikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya uhujumu uchumi, kutakatisha fedha na kusababisha hasara Serikali.
Hali za uhakika zilizolifikia gazeti hili jana zilisema mitambo hiyo kwa sasa haizalishi umeme.
MTANZANIA lilitembelea mitambo hiyo iliyoko Tegeta na kukuta wafanyakazi wachacheambao walikiri mitambo hiyo kutofanya kazi.
"Mitambo ilizimwa tangu siku ile walipomkamata Sethi", alisema mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo ambaye hakuwa tayari kutajwa jina lake gazetini.
Pamoja na hatua hiyo inaelezwa kuwa kuna hatari ya kuitaifishwa kwa mitambo hiyo hasa baada ya Serikali kuweka ngumu katika utoaji wa leseni mpya ya biashara ya kuzalisha umeme kwa kampuni hiyo.
Licha ya hali hiyo leseni ya kampuni hiyo ilimalizika muda wake Julai 15, mwaka huu ambapo hadi sasa uamuzi wa kuitaifisha mitambo hiyo kurudi kuwa mali ya TANESCO ama laa ukisubiri uamuzi wa Ikulu.
Kwa sababu hiyo, kama Serikali itaendelea na msimamo wake dhidi ya IPTL ndiyo utakuwa mwisho wa miaka 23 ya IPTL.
Kampuni hiyo au IPTL iliingia nchini tangu mwaka 1994 na kila mwezi imekuwa ikilipwa Sh. bilioni 5.943 na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ikiwa ni gharama za uwekezaji mbali na gharama za umeme inaoliuzia shirika hilo.
Novemba 2014, baada ya Bunge kujadili Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu Akaunti ya Tegeta Escrow, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), ilitoa maazimio manane ikiwa ni pamoja na kuangaliauwezekano wa kuichukua mitambo ya IPTL na kuimilikisha kwa TANESCO.
Siku chache baada ya Bunge kupitisha uamuzi huo ambao ulifanyiwa kazi kwa haraka kwa Profesa Sospeter Muhongo kujiuzulu nafasi yake.