Napendekeza Mkoa Mpya wa Butiama

LENDEYSON

JF-Expert Member
Sep 27, 2013
2,996
2,659
Ndiyo! Namaanisha mkoa mpya wa Butiama.

Hivi hakuna Wazalendo wa kuomba kuanzishwa huu mkoa kama kielelezo cha kumuenzi Baba wa Taifa hili?

Twajua hakuwa Mbinafsi, na hakutaka kujipendelea licha ya kuwa na uwezo huo! Leo tunaona uzalendo sehemu fulani kuwa mkoa kutokana na mihemko sijui ni ya msiba ama ubinafsi ulioasisiwa na mtu fulani?

Kwa dhati kabisa, naomba nipendekeze Mkoa Mpya huu wa Butiama kwani una kila sifa ya kuwa Mkoa. Naomba hata mkuu wa mkoa wa Manyara uunge mkono Hoja hii. Naomba wakaazi wa maeneo hayo mjitokeze na kupeleka maombi haya serikalini.

Mkoa huu uundwe na Musoma Vijijini yote, Serengeti, Bunda, sehemu ya Wilaya ya Meatu, na hadi sehemu ya Wilaya ya Mbulu!

Naomba kuwasilisha!
 
Ivi juu una jua ya kuwa iyo ni miongon mwa halmashauri ambayo makusanyo yake ya ndani duni sanaa
 
Napendekeza mkoa mpya wa Nzega. Pia Tabora boys alikosoma baba wa Taifa kiwe chuo kikuu.
 
Back
Top Bottom