Napendekeza mishahara ya Mawaziri ipunguzwe

Civilian Coin

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
2,305
4,379
KUNA HAJA YA MISHAHARA YA MAWAZIRI KUPUNGUZWA nakuwa ANGALAU 1.5M

Kimsingi Kiongozi Mzalendo lazima aangalie maslahi ya Taifa na wananchi wake. Kitendo cha kiongozi kujiangalia mwenyewe huku akitumia mamlaka yake kuhukumu ni majanga kwa kizazi chetu.

Kama tu mwalimu mwenye Digrii mshahara wake anaoshika mkononi(take home) ni takribani laki 5. Hana posho, hana nauli ya usafiri, hana posho ya chakula, hana posho ya NYUMBA, hana posho ya dreva lakini waziri anapokea mshahara takribani 3.5m na mahitaji yote anapata. Hapa nchi inakuwa haina usawa Bali inakuwa na upendeleo. Ndio maana wanalipana mapesa manono halafu wanatengeneza kanuni za kuwabana wasio na maposho.

Nchi bado iko changamotoni kwenye swala la maslahi kwa umma. Tatizo sio kuongeza mshahara kwa watumishi WA Umma na kuwaboreshea maslahi Bali tatizo ni "Standardization" ya maslahi. Kwangu Mimi Deogratius Kisandu naona Nchi hii si ya Kidemokrasia katika maslahi Bali ni ya ukandamizaji WA maslahi.

Tunahitaji kufika Tanzania ya Kileo tukiwa salama na sio tukiwa tumetishiwa kwa kuhoji ukweli wa maslahi.

Usiku mwema.

Deogratius Nalimi Kisandu

MALIPO NI HAPA HAPA DUNIANI.
 
Mwezi(moon) tayari ni mkubwa naona maneno yanaeleweka.
 
Hili wazo lako hata ashuke malaika mlinzi aende pale mjengoni kuwaomba hawawezi kukubali kwanza wenyewe wanasema haziwatoshi alafu wakipunguza nyama ya mbuzi,bia na totozi itakuaje tena.
 
Mshahara wa waziri ukishushwa kwa hicho kiasi unachotaka wewe, nahisi itaharibu mpka scale za mishahara kwa watu wa kada za chini kama walimu hao ambao unawatetea. Wataanza kuishi kama mashetani.,"Najaribu kuwaza tu nje ya box".
 
We Kisandu VP mkuu wa idara au Kitengo Halmashauri anakula 3m. na ushee ijekuwa waziri. Mi naona ndogo waongezewe..
 
Aliyekuambia waziri anakipwa iyo 3.5 nani? yani kukimbizana na makamera uku mara kule alipwe hela ya dagaa iyo..? Lala tu kisandu
 
Kweli unausingizi lala tu..Aliyekuambia waziri anapokea ela ya dagaa iyo ni nani? na makamera yote anayokimbizana nayo mara uku mara kule kisa iyo ela ya dagaa pale feri?
 
Naomba majaliwa amoe jina faru mmoja kule mbugani aitwe faru kisandu
 
Ukitaka kuamini kwamba hakuna bifu kati ya CCM na UKAWA basi gusia suala la kupunguza mishahara na posho za wabunge.
Ha...ha......, uko sawa mpaka unakeraaa. Hapo kama ni mtihani ni 100%. Hivi hayo mahela yao watazikwanayo????
 
Back
Top Bottom