FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 36,052
- 40,715
==========================
Badala ya mfumo wa sasa wa ‘TxxxAyy> TxxxByy > TxxxCyy > TxxxDyy , na sasa karibia tunaingia namba ‘E’ , ambapo mtu anakuwa anajua kabisa kwamba gari hii imesajili ya zamani au ni mpya.
Napendekeza namba zinazofuata baada ya kuisha kwa namba ‘D’ ziwe katika mfumo wa ku-‘Randomize’ ambapo panakuwa hakuna mtitiririko maalum katika usajili wa namba za magari, hii itasaidia mtu kuuza gari lake kulingana na hali iliyonayo, na sio kuangalia namba, unakuta gari zuri lina hali nzuri ila linakosa soko kisa ni namba A.
=================================
Watu wengi hununua gari toka Japan ili tu aweze kupata usajili mpya kwenye gari lake, na hivyo tunatumia pesa nyingi mno za kigeni kuagiza magari kama taifa, wakati huo huo kuna gari nyingi nchini zina hali nzuri kuliko hata hizo za kutoka japan (imefungwa engine mpya, gearbox mpya, matairi mapya, body halina accident damage, low mileage); ila linakosa soko kisa ni namba C, au B au A, ila kuna watu wanaagiza mikangafu toka Japan kisa tu itapata usajili mpya.
Hii itatoa fursa ya kuanzishwa kwa ‘Car restoration facilities’ ambazo zinalorudisha gari katika hali ya upya kama ilivyokuwa kiwandani, hata hao Japan ndivyo wanavofanya kiasi wakituuzia mkangafu sisi tunaona kama jipya, hii itatengeneza ajira nyingi sana!!!!
Pia itaokoa fedha nyingi tunazotumia kuagiza magari toka Japan, maana mtu ataona anunue hapa hapa nchini restored car ambayo haitamwaibisha barabarani kwa kuwa na plate number ya zamani...
===========================
Update: 08/09/2022
Ajira nje nje
==========================
Update: 25/10/2022
Kwa jinsi namba E inavyokimbiza kuna kitu hakipo sawa mahali
Kwa takwimu rasmi za Benki Kuu.. Kipindi cha miezi nane pekee Januari mpaka Agosti 2022 Watanzania wamenunua/wameagiza magari nje ya nchi yenye thamani ya mamilioni ya dola, hii tafsiri yake ni nini kuna kitu hakipo sawa ama kwa uzuri au kwa ubaya. Inawezekana kabisa nchi imefunguka na pesa...
www.jamiiforums.com
===========================Update: 14/05/2023