Napendekeza Meya awe mkuu wa mkoa pia,Mwenyekiti wa halmashauri awe mkuu wa wilaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Napendekeza Meya awe mkuu wa mkoa pia,Mwenyekiti wa halmashauri awe mkuu wa wilaya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ng'wanza Madaso, Mar 29, 2010.

 1. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #1
  Mar 29, 2010
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Nimetafakari kwa kina nikaona Mkuu wa mkoa na Meya wanafanya kazi kwa asilimia fulani zinashabihiana, Basi napendekeza Meya ndo afanye kazi za mkuu wa mkoa. Kwani kwa sasa wakuu wa mikoa wengi ni wabunge basi wawatumikie waliomchagua na huyu meya kwa kwa sababu amechaguliwa na Madiwani ni lahisi kwa madiwani kumuwajibisha pia bila kungoja maagizo toka ikulu.

  Mameya wanayajua mapato ya mkoa husika basi ni lahisi kwao kutumia kwa ajili ya mkoa wanaotoka. Kwani kwa mbunge ambaye ni mkuu wa mkoa hawezi kusimamia miradi ya jimboni kwake na mkoani anaouongoza. Na nilishaona meya na mkuu wa mkoa wakihitilafiana.

  Kwa Mwenyekiti wa Halmashauri anapaswa pia kufanya kazi za mkuu wa wilaya pia inakuwa lahisi kwa madiwani wa wilaya husika kumhoji na kumsimamisha Mwenyekiti wao bila kungoja maagizo kutoka Ikulu.

  Wakuu wengi wa mikoa ambao ni Wabunge na wanaotarajiwa kugombea Ubunge wanaviacha vituo vyao vya kazi na kutumia Gari na pesa za mkoa fulani kwenda majimboni mwao kinyemela na kuanza kuomba kura,Kwa upande wa meya yeye ametoka pale pale mkoani hana haja ya kusafili kwenda sehemu nyingine kuomba ama kugombea ubunge kwa sababu yeye ni diwani kutoka pale basi mambo yake anayafanyia palepale.


  Kwa hili litasaidia kubana matumizi na kuwa na vyeo mtililiko kwa kazi ambazo anaweza kufanya mtu mmoja

  Je hili kwa maoni yenu linaewzekana?
   
 2. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #2
  Mar 29, 2010
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Nimetafakari kwa kina nikaona Mkuu wa Mkoa na Meya wanafanya kazi kwa asilimia fulani zinashabihiana, Basi napendekeza Meya ndo afanye kazi za mkuu wa mkoa. Kwani kwa sasa wakuu wa mikoa wengi ni wabunge basi wawatumikie waliomchagua na huyu meya kwa kwa sababu amechaguliwa na Madiwani ni lahisi kwa madiwani kumuwajibisha pia bila kungoja maagizo toka ikulu.

  Mameya wanayajua mapato ya mkoa husika basi ni lahisi kwao kutumia kwa ajili ya mkoa wanaotoka. Kwani kwa mbunge ambaye ni mkuu wa mkoa hawezi kusimamia miradi ya jimboni kwake na mkoani anaouongoza. Na nilishaona meya na mkuu wa mkoa wakihitilafiana.

  Kwa Mwenyekiti wa Halmashauri anapaswa pia kufanya kazi za mkuu wa wilaya pia inakuwa lahisi kwa madiwani wa wilaya husika kumhoji na kumsimamisha Mwenyekiti wao bila kungoja maagizo kutoka Ikulu.

  Wakuu wengi wa mikoa ambao ni Wabunge na wanaotarajiwa kugombea Ubunge wanaviacha vituo vyao vya kazi na kutumia Gari na pesa za mkoa fulani kwenda majimboni mwao kinyemela na kuanza kuomba kura,Kwa upande wa meya yeye ametoka pale pale mkoani hana haja ya kusafili kwenda sehemu nyingine kuomba ama kugombea ubunge kwa sababu yeye ni diwani kutoka pale basi mambo yake anayafanyia palepale.


  Kwa hili litasaidia kubana matumizi na kuwa na vyeo mtililiko kwa kazi ambazo anaweza kufanya mtu mmoja

  Je hili kwa maoni yenu linaewzekana?
   
 3. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #3
  Mar 29, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Hao wakuu wa mikoa nao wawe wanachaguliwa na wananchi pia, na ikitokea mkuu wa mkoa anshindwa kuwajibika basi wananchi wawe huru kuchaguwa mwingine.
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Mar 29, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ni wazo zuri sana...lakini katiba hairuhusu.
   
 5. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #5
  Mar 29, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  hapa nashindwa kusema ngoja nitafakari kwanza
   
 6. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2010
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mkuu japo katiba hairuhusu nina swali dogo tu, kwani mkuu wa mkoa anasimamia nini na meya anasimamia nini?.Kwani mji ukiwa mchafu ninani awajibishwe?.Mapato ya mji husika yakilegalega ni nani alaumiwena mengineyo mengi?.Yote haya Meya huyafanyia kazi na mkuu wa mkoa pia,sasa kwanini asiwepo mmoja tu akayasimamia haya yote?.
   
 7. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #7
  Mar 29, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mzee Madaso hapa unajidanganya tu.System iliyopo ni ya ki CCM ,haiwezi kubadilika.
  Umeshasikia mkuu wa mkoa wa Berlin au London au NewYork?

  Hawa DAO,DED ,DC na wenzi wao mmikoani ni wastage of space,time na resources.
  Chukua Dar Es Salaam kwa mfano:
  Hakuna haja ya kuwa na Mkuu wa Mkoa.Inatakiwa kuwa na strong local council ,ambayo wote watakuwa chini ya Mayor wa jiji.Hapo ndio watakuwepo wachumi,polisi ,afya etc.Wilayani vilevile.


  Lakini survival ya mfumo wa sasa ,ni kuhakikisha ulaji unaendelea kila siku
   
 8. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #8
  Mar 29, 2010
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hii ingekuwa nzuri sana kwani wangeheshimu pesa za wananchi,lakini kwa sasa mkuu wa mkoa hata kama akifanya mabaya wananchi watabaki kushika matama wakisubili huruma ya Rais ya kumuondoa.
   
 9. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #9
  Mar 29, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Tena ingependeza zaidi na kuleta maana pale hao wakuu wa mikoa miongoni mwao ndio angetoka Rais wa nchi...!

  Vyama vya siasa vingeteuwa wagombea wao, na yule anayeshinda ndiye anakuwa mkuu wa mkoa... Kisha hivyo vyama vinachaguwa miongoni mwa watu wao waliochaguliwa kuwa wakuu wa mikoa kugombea nafasi ya urais. Nahisi hii ingepunguza utitiri wa wagombea urais
   
 10. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #10
  Mar 29, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  naunga mkono hoja ....!!!
   
 11. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #11
  Mar 29, 2010
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  badilisheni katiba, kwanini tuwe na katiba kikwazo kwa vitu vizuri???????????
   
 12. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #12
  Mar 29, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160

  Wabadilishe katiba ili waondoke madarakani?
   
 13. R

  Renegade JF-Expert Member

  #13
  Mar 29, 2010
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 3,770
  Likes Received: 1,074
  Trophy Points: 280
  Mkuu point yako sio mbaya,
  Lakini mimi nina mtizamo tofauti na wewe , Ni kweli kwamba kuwa na nafasi nyingi zinazoshabiiana kunaongeza gharama kwa serikali lakini pia Hakuleti tija kwa Taifa, suala la kofia mbili liondolewe kabisa, inapofikia uwezekano wa mtu kuteuliwa nafasi nyingine ile ya mwanzo ikanwe.Mbunge asiteuliwe kuwa waziri, mawaziri wawe watendaji waliobobea toka kwenye wizara husika.Ukiwa mbunge hubaki kuwa mbunge.Tukija kwenye hiyo pointi yako ya msingi meya ni Diwani anayewakilisha kata yake, huyu abaki kuwa diwani.
  ateuliwe mtu ambaye ataweza kusimamia shughuli zote za utendaji katika ngazi ya mkoa na pia kila wilaya.
  Mfano: Katika ngazi ya Mkoa, Meya huwa na ulinganifu na RC, Mkurugenzi wa Manispaa , Pia nafasi kama ya RAS nayo inashabiiana na hizo.
  Mkurugenzi na RC wanashulika na watendaji , japo RC hutanua wigo mpaka Kusimamia vyombo vya usalama lakini ni kitu kinachoweza kufanywa na Mkurugenzi akipewa dhamana.RAS Humsaidia RC Mambo ya utawala, lakini chini ya mkurugenzi kuna afisa utumishi ambaye anafanya kazi kama za RAS, na RC hana watendaji wengi, ukiunganisha unawaunganisha hao wote.Kwa hiyo nafasi moja inawaunganisha wote hao.awepo mwenyekiti wa madiwani kwa ajili ya vikao na kufuatilia watendaji.
  Pia ngazi ya wilaya iwe kama ya mkoa, DC, DED, DAS na mwenyekiti wa Halmashauri abaki mmoja, Japo DAS yuko chini lakini asiwepo awepo mkurugenzi wa wilaya ambaye atasaidiwa na AFISA UTUMISHI, VILE VILE NGAZI YA WILAYA DC hana watu wengi.
  Habari ndo hiyo, wakuu sina ugomvi na nafasi zenu bali maslahi ya nchi.
   
 14. K

  Kimweri JF-Expert Member

  #14
  Mar 30, 2010
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 3,998
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Wishful thinking!

  kuna vitu Tanzania haviwezi kutokea hivi karibuni,hicho ni kimoja wapo,wewe uanataka wapunguziane madaraka,waondoe nafasi za kupeana vyeo,wawe "eficient".

  THAT is so not Tanzanian Government.so it wont happen.
   
 15. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #15
  Mar 4, 2012
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mkuu katiba mpya ndo hiyo yaja je haya tuyatarajie?

   
 16. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #16
  Mar 4, 2012
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Tarajia disappointment. Hakuna katiba mpya itakayotokana na usimamizi wa CCM. Hiki kinachofanyika sasa ni usanii mtupu we subiri utaniambia mwisho wa chakato ni square one.
   
 17. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #17
  Mar 4, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Na ma-RAS na ma-DAS je...

  Au hao unaona wana kazi za maana za kufanya? Ma-Afisa Tawala je...
   
Loading...