Napendekeza Mdahalo wa ana kwa ana kati ya Wasomi wa Kiislamu na Kikristo Waliomo na Wasiokuwamo JF

Mkuu,
Mi naonaga hakuna haja ya kushindana wala kutoleana kwa maneno meengi kwa ajili ya hizi dini zilizokuja na meli.

Wewe leo unaweza ukakomaa kabisa Yesu ndio mwenyewe, hakuna mwengine zaidi yake, na bila yeye basi mtu ahera inamuhusu.

Shark

Lakini je ungekua umezaliwa Uislamuni ungetetea hayo?

So kigezo ni familia ulipozaliwa, au reality?

Shark, huu ndio ukweli ambao waafrica tulio wengi hatuzitumi akili zetu kufikiri... tumepokea hizi dini na wachache sana wanazisoma na kuzifuata kutokana na kuzielewa bali wengi tuma tu kwa vile tumezaliwa na kukuta wazazi wetu wamo humo. matokeo yake tumebaki kuwa "fanatics" na inakuwa kigezo cha kutugawa na kubaguana.


Utaona hata comments za wachangiaji wengine hapo juu, ndio maana hata haya yanayotokea mbagala na kwingineko africa yanatokea... poor african, we don't use our brains!
 
Mh mtawaweza hao masela wa vipedo,wanabishana na ubwabwa na wanashina,sembuse mambo ya maana,inabidi siku hiyo muwe na bunduki kabisa maana tukiwasihnda watakimbilia bakora!
 
shika sana ulicho nacho asije shetani akakitwaa binafsi sina haja ya kuelewa tofauti zaidi ya kwamba upande huo siyo wa kufuata WameshaProve Itikadi yao halisi. Haiwezekani mtu utoke Ibadani ukitafuta pa kwenda kufanya Uhalifu kwa jina la Mungu

If the Lord Himself came down today, will He not talk with or teach them? Will He not listen to their questions and arguments and give them answers as He did to the Pharisees of His time?
 
shika sana ulicho nacho asije shetani akakitwaa binafsi sina haja ya kuelewa tofauti zaidi ya kwamba upande huo siyo wa kufuata WameshaProve Itikadi yao halisi. Haiwezekani mtu utoke Ibadani ukitafuta pa kwenda kufanya Uhalifu kwa jina la Mungu

If the Lord Himself came down today, will He not talk with or teach them? Will He not listen to their questions and arguments and give them answers as He did to the Pharisees of His time?
 
Nafikiri hilo lisiwe hapa tu bali liwe mjadala wa Kitaifa huko Tanganyika. Suala hili liliwahi kuongelewa Bungeni kwenu na Zitto kabwe na wengi walilipuuza.

Kumbukeni suala la UDINI ni suala la kihistoria sana huko Tanganyika kwani hilo ni kovu lililoachwa na wakoloni wa Kiingareza katika kuitawala tanganyika. Walitumia Ukabila katika Kenya na Uganda.

Nafikiri sasa ni kipindi muafaka kuandaa MJADALA huo wa kitaifa kuona kiini, ukubwa wa tatizo na suluhisho. Kwani bila kufanya hivyo basi nje ya Muungano wenu tanganyika lazima itagawanyika katika mapande mawili yaani UISLAM na Ukristo.
 
Mdahalo wa nini? Kama ulisoma hadi Chuo Kikuu, huhitaji Padre and Mchingaji kuja kukuelimisha juu ya Ukristo. Nunua Biblia tena linapatikana kwa lugha zote. Soma mafundisho ya Yesu, halafu ugeukie msaafu na utaona tofauti kadi ya mafundisho ya dini hizi mbili. Yesu alifundisha saana kuhusu umoja na uvumilivu. sijui kama SAW alifundisha hayo maana kitabu chenyewe kimeandikwa kwa kiarabu...
 
Kujadiliana kuhusu dini bila kuwa na Terms of Reference ni ngumu sana, maana kila dini ina marefu na mapana yake. Ili mjadala uwe na tija lazima tukubaliane na mambo gani maalumu tutajadili.
Hata hivyo, uzoefu unaonyesha tutaishia kama yale ya juzi Mbagala ingawa tofauti itakuwa hakuna kurushiana ngumi na kuvamiana physically maana hatuonani, ila wengine watapasua key boards za kompyuta au simu zao.
 
Ni hatari kufanya hivyo hasa kwa sisi tulio wengi ambao uvumilivu si wa kidini tu bali hata wa kisiasa umeanza kupungua kwa kasi, jiulize, kama mtoto amekojolea msahafu na watu wazima wakafanya uharibifu mkubwa kiasi kile na serikali ikachelewa kiasi kile, itakuwaje?

Wazo zuri sana pia don12.
 
Mdahalo wa nini? Kama ulisoma hadi Chuo Kikuu, huhitaji Padre and Mchingaji kuja kukuelimisha juu ya Ukristo. Nunua Biblia tena linapatikana kwa lugha zote. Soma mafundisho ya Yesu, halafu ugeukie msaafu na utaona tofauti kadi ya mafundisho ya dini hizi mbili. Yesu alifundisha saana kuhusu umoja na uvumilivu. sijui kama SAW alifundisha hayo maana kitabu chenyewe kimeandikwa kwa kiarabu...

Yesu alipofundisha hakutumia biblia. Aliongea maneno yaliyokuwa ktk biblia (agano la kale); Hata Paulo na Peter na wahubiri wa agano jipya hawakutumia agano jipya kuhubiri. Walitumia midomo. Biblia ni muhtasari wa baadhi ya maneno waliyosema kaka. Unajua? Most of the time there is bigger power in talking than reading. Ingawa tukienda deep sana ktk hili inabidi tuhamie ktk JUKWAA la dini.
 
Ni wazo zuri sana,,,ila utekelezaji wake ni mgumu kidogo...
Imani hizi mbili ya Islam na Kristo zimesimamishwa na watu wawili tafauti na waliokuwa na approach tofauti kabisa katika mafundisho na uenezaji wa imani..!!

YESU ambaye yeye ni kiongozi wa kundi letu...aliongeza kundi na wafuasi wake kwa njia za kidemokrasia(majadiliano na mahubiri)kila aliyeamini na kukubali alipata kibali kufanyika kuwa mwana wa aliye Juu...
Akiondoka ulimwengini akiubiri habari ya kusameeana na Kupendana pasi na mipaka uku akituamrisha kuwapenda Adui zetu zaidi...
Akiwaacha mitume na wanafunzi wake akisema "tazameni nawatuma kama kondoo kati ya kundi la Mbwa mwitu"
ni lugha ya picha hii, nani kondoo? ni wale waliotumwa na nan Mbwa mwitu..? unaweza ukajazilizia hapo...
Tena iweni wapole kama kondoo na waelevu kama nyoka...

Nageukia upande wa pili wa sarafu...

Muhamadi ndiye kiongozi wa waislamu,mtume wa mwisho na kipenzi cha mungu wao(allaah...)

Alieneza imani islam kwa njia ya Vita(jihadi),,kila aliyempinga na kuupinga uislamu aliuwawa(dictorship)....
Akiondoka ulimwenguni aliwataka waislamu kuilingania imani yao...kuipigania kwa Ajili ya allah...!!

Sasa unaweza kuona,,nyumba hzi mbili zimejengwa kwa misingi tofauti...
Natamani endelea ila ngoja niachie hapa..
Ntarudi..
Asalaam aleikumu..

JIHAD KATIKA BIBLIA Wakristo wamefanya kampeni
za makusudi kwa muda mrefu
sana, ili kutoa picha kuwa
Jihad yaani vita vitakatifu,
vimeamuriwa na Allah (s.w.)
katika Qur’an na kuwa katika Biblia hakuna sehemu yoyote
iliyohalalisha vita hivyo. Na
Jihad inaambatana na Uislamu
tu. Na kwenye vitabu vingine
vya dini kitendo cha kupigana
kwa jina la dini au Mungu inapigiwa debe kuwa hakuna.
Hii inadhihirisha kwa ufupi vipi
wasomaji, hususani wa biblia
kuwa hawafahamu kilicho
andikwa ndani ya bibilia. Basi
Insha’Allah ungana nami tuangalie maandiko ya bibilia ni
vipi wamepigana vita hivi
vitakatifu na walikuwa
"wakatili" au "wapole" kiasi
gani. Katika kuwaandaa watu
kwa vita, Mungu (Yehova) aliweka sheria ifuatayo: "Utokapo kwenda vitani
kupigana na adui zako, na
kuona farasi na magari, na
watu wengi kuliko wewe,
usiwaogope, kwa kuwa BWANA
Mungu wako yu pamoja nawe, aliyekukweza katika nchi ya
Misri. Na iwe msongeapo
mapiganoni, Kuhani na kusema
na watu, awaambie, sikizeni,
enyi Israili, hivi leo mwasongea
mapiganoni juu ya adui zenu; mioyo yenu isizime, msiache
wala msitetemeke, wala
msiingiwe na hofu kwa ajili ya
wao. Kwa maana BWANA,
Mungu wenu, ndiye
awaandamaye kwenda kuwapigania juu ya adui zenu,
ili kuwaokoa ninyi".
(Kumb. 20:1-4) Jihadi rasmi ya kwanza kabisa
iliongozwa naNabii Yoshua mwana wa Nuni, ili kuwaingiza Waisraeli katika
nchi ya ahadi (Kaanani)
wakitokea Misri. Mji wa kwanza
kushambuliwa ulikuwa wa
Yeriko. Kwanza Yoshua (a.s.)
alipeleka wapelelezi wawili ambao walijificha katika
nyumba ya kahaba Rahabu
(Yoshua 2:1-24). Kisha
waliuvamia mji na kuuweka
"Wakfu" kwa kuua kile chenye
uhai isipokuwa kahaba Rahabu na familia yake.
"...Basi wakaangamiza kabisa
vitu vyote vilivyokuwa ndani
ya mji, wanaume na
wanawake, watoto na wazee
na ng’ombe, na kondoo, na punda kwa makali ya upanga".
(Yoshua 6:21)
Na Yoshua 6:24 inasema;
…Kisha wakauteketeza mji kwa
moto, na vitu vyote
vilivyokuwa ndani yake… Utaratibu wa "kufyagia" miji
uliendelea hadi Yoshua mwana
wa Nuni alipotawala miji yote
aliyoitaka. (Yoshua 10:28;
11:16-23). Wakuu wa nchi (wafalme)
wao walikumbana na vifo
vya aina yake; "Kisha ikawa hapo walipomletea
Yoshua hao wafalme watano
hapo nje, Yoshua akawaita
wanaume wote wa Israeli,
akawaambia majemedari wa
vita waliokwenda naye, haya jongeeni karibu, mweke nyayo
za miguu yenu katika shingo za
wafalme hawa. Nao
wakajongea karibu, wakatia
nyayo zao katika shingo zao.
Yoshua akawaambia., msiache wala msifadhaike, iweni hodari,
na mioyo ya ushujaa, kwa
kuwa ndivyo BWANA
atakavyowafanyia adui zenu
wote, ambao mwapigana nao.
Baada ya Yoshua akawapiga na kuwaua, akawatundika
katika miti mitano, nao
wakawa wakitundikwa katika
miti hiyo hata jioni".
(Yoshua 10:24-26). Aidha, wakati mwingine Yehova, alishiriki yeye binafsi "kuua" watu wengi
zaidi kuliko "walivyouawa" kwa mikono ya watu wake. "Kisha ikawa hapo walipokuwa
wakikimbia mbele ya Israeli,
hapo walipokuwa katika
kutelemkia Beth-horoni, ndipo
BWANA alipowatupia mawe
makubwa kutoka mbinguni juu yao hata kufikilia Azeka, nao
wakafa, hao waliokufa kwa
kuuawa na hayo mawe ya
barafu walikuwa ni wengi
kuliko waliouliwa na wana wa
Israeli kwa upanga". (Yoshua 10:11) Na Yuda walipo tazama nyuma,
angalia, vita vikawa mbele na
nyuma; wakamlilia BWANA na
makuhani wakapiga mapanda.
Ndipo wakapiga kelele na watu
wa Yuda; ikawa. Watu wa Yuda walipopiga kelele, Mungu
akampiga Yeroboamu na Israeli
wote mbele ya Abiya na Yuda.
wana wa Israeli wakakimbia
mbele ya Yuda; naye Mungu
akawaua mikononi mwao. Abiya na watu wake wakapiga
mapigo makuu; hata
wakaanguka wameuawa wa
Israeli mia tano elfu, watu
wateule. Ndivyo walivyo tiishwa
watu wa Israeli wakati ule, wakashindwa wana wa Yuda,
kwa kuwa walimtegemea
BWANA, Mungu wa baba zao.
Abiya akamfuata yeroboamu,
akamnyang'anya miji, betheli
na miji yake, na Yeshana na miji yake, Efroni na miji yake.
wala Yeroboamu hakupata
nguvu tena siku za Abiya;
kisha BWANA akampiga akafa.
ila Abiya akapata nguvu
akapata nguvu akaoa wake kumi na wanne, akazaa wana
ishirini na wawili binti kumi na
sita.
2 Nyak, 13:14-21 Jihadi ya kuikomboa nchi ilianza
mwaka 1220 KK na kuendelea
hadi mwaka 1010 KK ambapo
Nabii Daud (a.s.) aliutwaa mji
wa Yerusalem na kuwa makao
makuu ya dola yake. Dola hii ilidumu kwa muda wa miaka
290 kwa dola ya Kaskazini
(Samaria) na miaka 423 kwa
dola ya kusini (Yuda). Dola hizi
zilianguka na kutawaliwa na
mapagani baada ya kumwasi Yehova, kwa kufuata sheria
zisizo za Mungu. Baada ya
kuteswa sana na mapagani
walianzisha tena jihadi ili
kujikomboa wakati wa mfalme
Mgiriki Antioko Epifani (175 – 163 KK). Vita hivi vilianzishwa
rasmi na Matathia mwaka 166
KK. Sababu ya kuanzishwa kwa
jihad hii ilikuwa kurejesha
sheria za Torati zilizofutwa na
Antioko Epifani ili kuleta "Umoja na mshikamano wa kidola
(Empire)". "Mfalme Antioko akaziandikia
milki zake zote, kwamba wote
wawe taifa moja, kila mtu
aache sheria zake za asili.
Watu wote wa mataifa
wakaikubali amri ya mfalme, hata wengi katika Israel
(Waislamu) walifuata ibada
yake, wakitoa dhabihu kwa
miungu ya uongo na kutia
najisi sabato. Mfalme akapeleka
barua Yerusalemu na kwenye miji ya Uyahudi (dola ya
Kiislamu) kwamba wazifuate
desturi zilizo za kigeni kwao,
waache kutoa sadaka za
kutetekezwa a dhabihu na
sadaka ya kinywaji hekaluni, wazinajisi sabato na sikukuu,
na kulitia unajisi hekalu na
waliotakasika. Tena, wajenge
madhabahu na mahekalu na
viwanja vitakatifu vya miungu
ya uwongo, na kutoa dhabihu za nguruwe na wanyama
wachafu, waache wana wao
bila kutahiriwa, na kujitia nafsi
zao unajisi kwa uchafu na
ukafiri wa kila namna, kusudi
waisahau sheria (Torati) na kuzibadili kawaida zao. Naye
asiyelitii neno la mfalme
atakufa".
(1 Makabayo 1:41-50) Kuhani Matathia hakuvumilia
kuendelea kuona fedheha hiyo
dhidi ya waumini na akasema: "(Mathathia) akayaona mambo
ya ukufuru yaliyotendeka
katika Uyahudi na Yerusalemu,
akasema, ole wangu! Kwa nini
nalizaliwa kuuona uharibifu wa
watu wangu na maangamizo ya mji mtakatifu, hata kukaa
kimya unapotiwa katika mikono
ya adui zake, na patakatifu
pake (Msikiti mkuu - Hekalu)
katika mikono ya wageni
(Antioko aliteka hekalu na kulinajisi kwa kuingiza
madhabahu yake ya
kutambikia maarufu "chukizo la
uharibifu"). Nyumba yake
imekuwa kama ya mtu asiye na
heshima vyombo vyake vya fahari vimetekwa na
kuchukuliwa; watoto wake
wameuwawa njiani, na vijana
wake kwa upanga wa adui
taifa lipi lisiloyashiriki mateka
yake? Ufalme upi usioziteka mali zake? Mapambo yake yote
yameondolewa naye aliyekuwa
muungwana amekuwa mtumwa!
Naaam, vyombo vitakatifu
vyetu na fahari yetu na
utukufu wetu vimefanywa ukiwa; vimetiwa unajisi na
watu wa mataifa. Mbona, basi,
tuzidi kuishi? Matathia na
wanawe wakararua nguo zao,
wakajivika gunia, wakalia kwa
majonzi (toba ya kweli) (1 Makabayo 2:6-14). "Baada ya toba hiyo ya kweli
akatangaza jihadi "kisha,
Matathia alipiga mbiu mjini kwa
sauti kuu, akisema, kila aliye
na juhudi (mujahid) kwa ajili ya
sheria (Torati) na kutaka kulitetea agano, na ANIFUATE!
Naye na wanawe wakakimbilia,
wakaviacha vyote walivyokuwa
navyo mjini"
(1 Mak. 2:27-28). Kisha kazi ikaanza. Baadhi ya
Wayahudi wapatao 1000
walienda kujificha jangwani.
Askari wa mfalme waliwafuata
katika siku ya sabato kwa
kuogopa "kuinajisi" sabato walisita kupigana na wote
wakachinjwa kama mbuzi
(tazama 1Mak 2:29-38). Lakini kuhani Matathia
akaamua hivi: "Matathia na rafiki zake
walipopata habari waliambana,
kama sisi sote tutafanya kama
walivyofanya ndugu zetu,
tusipigane na watu wa mataifa
kwa ajili ya nafsi zetu na amri (sheria) zetu, watatufata
upesi katika nchi. Wakafanya
shauri siku ile ya kuwa; kama
mtu yeyote akituletea vita
siku ya sabato TUPIGANE NAYE,
tusife wote kama ndugu zetu waliokufa katika vificho vyao.
Wakati huo kundi la Wahasidimu
(mujahidina) walijiunga nao,
Waisraeli hodari wa vita
waliojitoa kwa hiyari kuitetea
sheria. Na wote (wasio waumini) waliyakimbia maovu
walikuja kwao na kuwaongezea
nguvu. Wakakusanya jeshi
kubwa, wakawapiga wenye
dhambi (makafiri) katika hasira
yao na, (waumini) walioasi (wanafiki) katika ghadhabu
yao; na (wanafiki) waliobaki
waliwakimbilia mataifa
(makafiri) wajisalimishe kwao.
Matathia na rafiki zake
wakazunguka zunguka wakizivunja madhabhu za
miungu na kutahiri kwa shuruti
watoto wote wasiotahiriwa
katika mipaka ya Israeli;
wakawafuata wana wa uovu
na kazi ilifanikiwa mikononi mwao. Wakaiokoa sheria katika
mikono ya mataifa na wafalme,
wasikubali wenye dhambi
wainue pembe zao".
(1Mak. 2:39-48) Kuhani Matathia
alipokaribia kufa aliwausia
wanawe yafuatayo: "Msiyaogope maneno ya mtu
mwenye dhambi, maana fahari
yake itakuwa samadi na funza.
Leo atainuka na kesho
hataonekana kamwe, amerudia
udongo wake na mawazo yake yamepotea. Basi ninyi
wanangu, muwe hodari,
mfanye kwa kiume kwa ajili ya
sheria (Torati), maana kwa
hiyo mtatukuzwa. Tazama,
Simon ndugu yenu, najua ya kuwa ya mtu wa shauri;
msikilizeni siku zote; atakuwa
baba kwenu. Yuda Makabayo,
shujaa tangu ujana wake,
atakuwa jemadari wenu na
kuwapigania watu wenu. Nanyi, wapokeeni wote wanaoishika
sheria, mkatoze kisasi cha
maovu waliyotendewa watu
wenu. Wapatilizeni mataifa na
kuyaangalia (kuyafuata)
maneno ya sheria. Akawabariki, akakusanyika kwa baba zake
(akafa)"
(1Mak. 2:64-69) Yuda Makabayo
akakumbana na mtihani: "Apolonio akakusanya mataifa
pamoja na watu wengi kutoka
Samaria, ili apigane na Israeli.
Yuda akapata habari, akaenda
kukutana naye, akampiga
akamuua. Watu wengi wakanguka wametiwa jereha
za mauti na wengine
wakakimbia. Wakateka nyara,
naye Yuda aliutwaa upanga wa
Apolonio, akautumia siku zote.
Seroni, jemadari wa jeshi la Shamu, alisikia ya kuwa Yuda
amekutanisha mkutano, jeshi la
watu waaminifu (wacha Mungu)
na walio hodari wa vita,
akasema, nitalitukuza jina
langu na kujipatia heshima katika ufalme kwa kupigana na
Yuda na wale walioko kwake
wanaoidharau amri ya mfalme.
Na pamoja naye walikwenda
jeshi kubwa la watu waovu ili
wamsaidie kuwatoza kisasi wana wa Israeli. Akaja karibu
na mipando ya Beth-horoni,
Yuda akamwendea na kikosi
kidogo. Nao walipoliona lile jeshi
kubwa likija juu yao
walimwambia Yuda, Je! Sisi kundi dogo tutaweza kupigana
na umati huu mkubwa wa
nguvu? Nasi tumedhoofu kwa
sababu hatujaonja kitu leo.
Yuda akasema, ni jambo rahisi
watu wengi wazingiwe kwa mikono ya wachache. Kwa
mbingu (Mwenyezi Mungu s.w.)
ni mmoja tu, kuokoa kwa
wengi au kwa wachache,
maana kushinda vitani
hakupatikani kwa wingi wa watu, ila kwa nguvu itokayo
mbinguni. Wao wanatujia kwa
wingi ni jeuri na udhalimu ili
kutuharibu sisi na wake zetu
na watoto wetu na kututeka.
Lakini sisi tunazipigania maisha na amri zetu . Yeye (Yehova
s.w.) atawafadhaisha usoni
petu,basi msiwaogope. Akisha
kusema hayo, aliwashambulia
kwa ghafula, Seroni na jeshi
lake wakapondwa mbele yake. Wakawafuatia katika
mitelemko ya Beth-horoni hata
uwandani chini wakaanguka
watu kama mia nane na
waliosalia walikimbilia nchi ya
Wafilisti. Basi hofu na woga uliwaangukia mataifa ya jirani
kwa sababu ya Yuda na ndugu
zake, jina lake likajulikana hata
kwa mfalme na mataifa yote
walisimulia habari za vita
vyake" (1Mak. 3:10-26). Jihadi hii iliendelea hadi dola
yote ya kiyahudi
ilipokombolewa na amani
kurejea. Katika kuthibitisha
kuwa Mungu, yuko pamoja na
mujahidina katika vita vyao, mujahidina watatu (3)
walilishinda jeshi la makafiri
zaidi ya elfu kumi. (Mujahid)
Yonathan na jeshi lake
wakapiga kambi penye ziwa la
Genesareti hata asubuhi na mapema wakaondoka kwenda
uwanda wa Hazori. Jeshi la
mataifa lilikutana naye
uwandani. Wengine wao
walikuwa wakimwotea milimani,
hali jeshi lenyewe lilipambana naye uso kwa uso Nao
waliomwotea wakaondoka
wakajitia katika vita, na wote
wa upande wa Yonathani
walikimbilia, asibaki hata mmoja
ila Matathia bin Absolomu na Yuda bin Kalfi, wakuu wa vikosi.
Yonathani akararua nguo zake
akajitia mchanga kichwani
(toba ya kweli) akasali. Akajitia
tena vitani, akawarudisha
nyuma, hata wakakimbia, watu wake walipoona hivi walimrudia
wakafuatana naye
wakiwakimbiza mpaka Kadeshi
kwenye kambi lao, wakatua.
Siku ile katika wageni
walianguka (walikufa) watu kama tatu elfu. Yonathani
akarudi Yerusalem".
(1Mak 11:67-74) 1samweli 15:3 inasema:
Basi sasa enda ukawapige
Amaleki, na kuviharibu kabisa
vitu vyote walivyo navyo, wala
msiwaachilie; bali waueni
mwanaume na mwanamke, mtoto naye anyonyae,
ng’ombe na kondoo ngamia na
punda. Basi ajili hiyo mwueni kila mume
katika hao watoto, na kila
mwanamke aliye mjua mume
kwa kulala pamoja naye, lakini
hao watoto wote wa kike
ambao hawakumjua mume kwa kulala pamoja naye
mtawaweka hai kwa ajili yenu.
Hesabu 31:17 Kumb 20:16-20
But of the cities of these
people, which the LORD thy
God doth give thee for an
inheritance, thou shalt save
alive nothing that breatheth: But thou shalt utterly destroy
them; namely, the Hittites, and
the Amorites, the Canaanites,
and the Perizzites, the Hivites,
and the Jebusites; as the LORD
thy God hath commanded thee: That they teach you not to do
after all their abominations,
which they have done unto
their gods; so should ye sin
against the LORD your God.
When thou shalt besiege a city a long time, in making war
against it to take it, thou
shalt not destroy the trees
thereof by forcing an axe
against them: for thou mayest
eat of them, and thou shalt not cut them down (for the
tree of the field is man's life)
to employ them in the siege:
Only the trees which thou
knowest that they be not
trees for meat, thou shalt destroy and cut them down;
and thou shalt build bulwarks
against the city that maketh
war with thee, until it be
subdued. Hapa hapa lazima tujiulize kwa
nini kila chenye kupumuwa
kiuliwe…? Ina maana hakuna
huruma hata kwa wanyama
sembuse watoto na vikongwe!?
Haya ndo tunayo yaona leo Iraq, Afghanistan, Chechnya na
kwengineko... Vita na maandalio ya vita
yalikuwa mengi sana angalia
pia 2nyaka 32:2-9 uone jinsi
Hezekia alivyo funga
chemchemu za maji ili mfalme
wa Ashura aitwae Senakeribu ashindwe vita kwa kiu na njaa. Isa 31:4 ...ndivyo bwana wa
majeshi ataposhuka ili kufanya
vita juu ya mlima sayuni, na
juu ya kilima chake... Kumb, 3:22 msimwache, kwa
kuwa bwana, mungu wenu,
ndiye awapiganiaye. Inajulikana kuwa Mungu wa
kwenye bibilia kesha weka
ahadi yake kwa kusema; …Mungu si mtu, aseme uongo;
wala si mwanadamu ajute;
iwapo amelisema, hatalitenda?
iwapo amenena, hatalifikiliza?
Hes, 23:19 Huyu ndie Mungu wa kwenye
biblia, na hayo nilio yanukuu ni
kutoka kwenye biblia. Si ajabu
kuona ivi leo mataifa ya
kimagharibi yakifuata mfumo
huu wa kivita toka kwenye biblia. Tuna shuhudi mengi sana
toka kwenye vyombo vya
habari na kuona jinsi nchi
amabazo zinashambuliwa
zikiangamizwa kwa mabomu na
maroketi, toka nchi za kimagharibi. Watoto, wanawake
wajawazito, wazee na
vikongwe, wanyama na mimea
hakuna kinacho salimika… yaani
ni mauwaji kwenda mbele…!! Basi kama aliahidi kuangamiza
miji ataiangamiza tu,
atushangahi George W. Bush
kututangazia kuwa ametumwa
na mungu kufanya vita na
mataifa ya kiislam… atushangai kuomuona Bush akimwambia
James Robison (a prominent
minister) kuwa... 'I've heard the
call. I believe God wants me to
run for President.'
Wamarekani hawakuwa nyuma kumuunga mkono rais wao kwa
kusema, ...it must have been
God who selected Bush, since a
plurality of voters hadn't. "Why
is this man in the White House?
The majority of America did not vote for him. He's in the
White House because God put
him there for a time such as
this." (William "Jerry" Boykin.) hata magazeti yao hakubaki
nyuma Time magazine gazeti la
marekani likaandika,
"Privately, Bush talked of
being chosen by the grace of
God to lead at that moment." World Magazine, a
conservative Christian
publication, quoted White
House official Tim Goeglein as
saying, "I think President Bush
is God's man at this hour, and I say this with a great sense of
humility." Even former President George
H.W. Bush speculated that
perhaps he needed to be
defeated so that his son could
become president: "If I'd won
that election in 1992, my oldest son would not be
president of the United States
of America," he said. "I think
the Lord works in mysterious
ways."
 
Huo mdahalo hautasaidia. Kuna mahubiri mengi sana ampayo unaweza kuhudhuria iwapo unataka ya midomo. Ni suala ya kuvua kwa muda imani yako na ukaenda hapo ukasikiliza. sasa hapo unaposema mara biblia ya kale au mpya, tayali ushaanza malumbano na mjadala bado, si kasheshe hiyo?
 
hapana mimi ninaomba kusiwe na mjadala kwani mpaka sasa kunambasuko wa kidini nchini ila haujaonekana wazi so kuandaa mjadala kutachochea mambo tofauti maana kumbuka sio kila mtu atachukulia suala hilo na hoja za wachangiaji kilahisi kama tunavyochukulia. Kwan wapo ambao watachukulia kihasira na wapo ambao watapuudhia suala hili je ni wangap watachukulia tofauti hatujui na kumbuka tukio lililotokea juzi tu hapa tayari nimeanzakututenga miongoni mwetu maana wapo waliokuwa wanahasira ndio wakaenda kuvunja makanisa je leo ni watu mia na kenda je ukitokea huo mjadala sindio kuingiza nchi kwenye vita za kidini. Jamani watanzania ninajua kila mmoja inamuuma kwa kilichotokea kwa pande zote mbili za dini kilichobaki tujalibu kufikiri mambo mengine maana tukiendelea hivi ninahuakika hatutaowana wala kusaidiana
 
Nyinyi munaojita wakristo biblia munaisoma tu lakini hamuijui ama hamuifanyii kazi!

Na wewe waisoma na kuifanyia kazi kwa manufaa yako binafsi ambapo shetani mapepo yake huwa yanaisoma yanaisoma sana kwa ajili ya kuipotosha na kuwapotosha wanadamu ili waiache kweli. Mfano mzuri ni wa Nyoka na mama yetu Hawa pale bustanini, na shetano na Yesu pale jangwani na mingineyo mingi ifananayo na hiyo.

Biblia ina siri moja ambayo ni kuionesha njia ya ukombozi kwa mwanadamu tangu mwanzo wa kuingia kwa dhambi ulimwinguni.

Kwa anaye okolewa ni nguvu ya Mungu lakini kwa wanaopotea ni upuuzi. Kwa hiyo upuuzi huo unaweza kuitafsri bibili unavotaka kwa kuwa unaeelekea upotevuni haikusaidii bali kwa wale wanaokusudia kumtafuta Mungu kwa bidii, biblia inasema kwao Mungu ataonekana.
 
Mdahalo siyo ishu sema waislam wawe na mfumo mzuli wa kupata viongozi wao .
Kama kiongozi msomi na anajua kazi yake ni ya mungu hawezi kuwa mchochezi.
Mimi najua kazi ya dini ni kuleta watu wote pamoja waishi kwa amani.
Tofauti na hapo jua ume feli!!!!!
 
Back
Top Bottom