Napendekeza Mdahalo wa ana kwa ana kati ya Wasomi wa Kiislamu na Kikristo Waliomo na Wasiokuwamo JF

Hicho kitu maaskofu hawakipendi kwasababu katika miaka ya 1980 midahalo hiyo ilipoanza wakristo wengi walisilimu. Ikabidi TEC waiamuru serikali yule muhadhiri wa kiislamu afukuzwe nchini wakaiomba BAKWATA ijitoe katika ule mdahalo ili polisi wafanye kazi yao.

Wana JF,
Nina rafiki zangu kadhaa wa kiislamu. Tunapendana na kuheshimiana licha ya tofauti ya ki-imani. Muislamu mmoja alikuwa 'group study' moja na mimi. Rafiki yangu tangu Form I hadi Form IV na room mate wangu University. Huyu ndugu alikuwa mtaratibu na mpole sana. Enzi hizo pale UDSM mlimani kulikuwa na muungano wa wanafunzi wa kiislamu ulioitwa MSAUD. Na itikadi za MSAUD na za huyu rafiki yangu zilikuwa hazipishani sana (at least theoretically) na misimamo ya waislamu wa 'itikadi' kali. Kwa kuwa tulikuwa marafiki tulioshibana nilimuuliza kuhusu usahihi wa misimamo yake ya kidini, ya ki-MSAUD, ya kiislamu (itikadi kali). Rafiki yangu, kwa utaratibu kabisa, kwa ukweli wa moyoni, akaniambia chanzo cha msimamo wake ni KORAN yenyewe. Kwamba yeye anashikilia misimamo yake kwa sababu KORAN inamtaka afanye hivyo. Kama isingekuwa KORAN asingekuwa na misimamo hiyo.

Sasa mimi sijasoma KORAN hata kidogo. Natamani kupatikane wasomi wa kiislamu wenye nia ya kutuelimisha kuhusu KORAN, kama misimamo ya itikadi kali ni ya ki_KORAN au ni uzushi. Na pia wapatikane wasomi wa ki-kristo wenye nia ya dhati ya kuelimisha wasioufahamu ukristo. Haya makundi mawili yakutanishwe ktk mdahalo wa ana kwa ana, wenye nia ya kujenga, lakini wenye nia ya kufahamishana ukweli toka mioyoni mwetu. Tufanye hivyo huku tukitarajia kwamba hoja zikipishana sana TUTAKUBALIANA KUTOKUKUBALIANA.

Napendekeza mdahalo huu uandaliwe kinamna fulani na wazito wa JF. Kwa baadae utaweza kurushwa hewani, sote tuone na tusikie. JF itaweza ku-raise fund kwa mtindo huu toka kwa wadhamini wa kipindi maana ni wazi kipindi hiki kitakuwa hot-cake.

Bado naamini kuna waislamu wengi hawana misimamo ya kiitikadi kali. Lakini tunataka wao kwa wao pia wasimame na watoe maoni kuhusu KORAN yao kama inafagilia itikadi kali au la. Na kama ni ndiyo basi tutafute namna ya kudumu ya kuishi huku waislamu wakitimiza KORAN na wakristo wakitimiza BIBLIA.

Rafiki yangu huyu alinieleza kuwa KORAN inadai nchi itawaliwe na sharia.

Sasa wasomi wengine wa kiislamu mnasemaje? Tukutane tutafakari mambo haya kwa uwazi na ukweli wa moyo. Inawezekana KORAN inadai hivyo na tunaposhindana na 'itikadi kali' tunapoteza muda. Tukiamua tunaweza kuleta kitu tofauti cha kuigwa duniani.

Humu JF naona hoja kadhaa kuhusu suala hili nyeti zinakuja kimzahamzaha, utani, na matukano fulani. Tukiwa ana kwa ana tutakuwa serious zaidi. Mnaonaje?

PENYE WENGI HAPAHARIBIKI NENO.

NAWAKILISHA.
 
Kama kweli unataka kujua kuhusu Quran shule zipo. Ulivyosoma mpaka chuo kikuu uliwahi kuwaambia maprofesa waje ufanye nao mdahalo?
 
Kama kweli unataka kujua kuhusu Quran shule zipo. Ulivyosoma mpaka chuo kikuu uliwahi kuwaambia maprofesa waje ufanye nao mdahalo?
Mkuu, lengo la hoja hii ni kwamba wewe unifahamishe uzuri wa kile unachokijua na mimi nikufahamishe uzuri wa kile nikijuacho. Baada ya hapo unabaki na uhuru wa kufanya informed decision.
 
Hicho kitu maaskofu hawakipendi kwasababu katika miaka ya 1980 midahalo hiyo ilipoanza wakristo wengi walisilimu. Ikabidi TEC waiamuru serikali yule muhadhiri wa kiislamu afukuzwe nchini wakaiomba BAKWATA ijitoe katika ule mdahalo ili polisi wafanye kazi yao.
Francis, ninachopendekeza hapa sio mihadhara ni mdahalo. Wasomi wa elimu dunia na elimu ya dini tukutane katika hali iliyojaa maarifa, ustaarabu na ikibidi kukubali kushindwa. Watakaotusikiliza huenda wakapata elimu ya nyongeza kutokana na hoja zetu. Style ya mihadhara, iwe ya Mzee Ponda au Biblia ni Jibu naona kama imekaa ki-ugomvi zaidi.
 
mkuu suala la mdahalo linawezekana kama tutakuwa na nia safi ya kutaka kuujua ukweli ili kuufuata bila kumtukana wala kumkashifu yoyote.

Tatizo kubwa wengi tunachukulia suala la mdahalo kama njia ya kutugawa na kutugombanisha na sio njia ya kuelimishana ili tuijue kweli na kweli ituweke huru.

Nb: irf niliyokuambia utembelee inasimama kwa niaba ya islamic reserch foundation taasisi inayoongozwa na dr zakir naik. Natumia sim ndiomana nimeshindwa kuiweka vizuri.

Peri unafaa ku-represent waislamu katika mdahalo. Nikifanikiwa kuandaa chochote cha aina ya mdahalo utakuwa wa kwanza kualikwa.
 
But do these Moslem radicals really want dialogue with Christians?
A very good question. Kama wamo humu watujibu. Nimeona baadhi hapo juu kama mkuu 'peri' wanaweza kujadili kwa points na kukubali nguvu ya hoja.
 
siungi mkono hoja, sihitaji kufahamu kitu chochote kinacho husu uislam kiwe kizuri ama kibaya. Mungu wangu sio Mungu wa kumpigania, yaani mimi kujitoa kimwili kumtetea, simuabudu Mungu wa jinsi hiyo. Mungu wangu anajitetea mwenyewe ninapo mwabudu katika roho na kweli.
 
Nadhani unajua wazi kabisa matokeo yake. mi naomba kusiwe na kitu kama hiki.
 
siungi mkono hoja, sihitaji kufahamu kitu chochote kinacho husu uislam kiwe kizuri ama kibaya. Mungu wangu sio Mungu wa kumpigania, yaani mimi kujitoa kimwili kumtetea, simuabudu Mungu wa jinsi hiyo. Mungu wangu anajitetea mwenyewe ninapo mwabudu katika roho na kweli.
Tuendelee kusahihishana. Kumbuka, 'imani huja kwa kusikia...'.
 
Hicho kitu maaskofu
hawakipendi kwasababu katika miaka ya 1980 midahalo hiyo ilipoanza
wakristo wengi walisilimu. Ikabidi TEC waiamuru serikali yule muhadhiri
wa kiislamu afukuzwe nchini wakaiomba BAKWATA ijitoe katika ule mdahalo
ili polisi wafanye kazi yao.

Ningekujibu kwa kutumia kitabu chako, na kwa kutumia vitabu vya imani yako ..lkn naogopa(sio kuheshimu) bana, maana mods wana tu ban hata tukinukuu quran!
 
shika sana ulicho nacho asije shetani akakitwaa binafsi sina haja ya kuelewa tofauti zaidi ya kwamba upande huo siyo wa kufuata WameshaProve Itikadi yao halisi. Haiwezekani mtu utoke Ibadani ukitafuta pa kwenda kufanya Uhalifu kwa jina la Mungu
 
Shark, kwa maoni yangu tulishachonganishwa tayari. Tunatafuta dawa ya ku-neutralize uchonganishi huu kabla haujafika kiwango kikubwa. Haya great thinkers, christians and muslims, keep talking tuone hili kama linawezekana au la.

Mkuu,
Mi naonaga hakuna haja ya kushindana wala kutoleana kwa maneno meengi kwa ajili ya hizi dini zilizokuja na meli.

Wewe leo unaweza ukakomaa kabisa Yesu ndio mwenyewe, hakuna mwengine zaidi yake, na bila yeye basi mtu ahera inamuhusu.

Lakini je ungekua umezaliwa Uislamuni ungetetea hayo?

So kigezo ni familia ulipozaliwa, au reality?
 
Ni hatari kufanya hivyo hasa kwa sisi tulio wengi ambao uvumilivu si wa kidini tu bali hata wa kisiasa umeanza kupungua kwa kasi, jiulize, kama mtoto amekojolea msahafu na watu wazima wakafanya uharibifu mkubwa kiasi kile na serikali ikachelewa kiasi kile, itakuwaje?
 
Back
Top Bottom