Napendekeza Mdahalo wa ana kwa ana kati ya Wasomi wa Kiislamu na Kikristo Waliomo na Wasiokuwamo JF | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Napendekeza Mdahalo wa ana kwa ana kati ya Wasomi wa Kiislamu na Kikristo Waliomo na Wasiokuwamo JF

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rapture Man, Oct 14, 2012.

 1. R

  Rapture Man JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Wana JF,
  Nina rafiki zangu kadhaa wa kiislamu. Tunapendana na kuheshimiana licha ya tofauti ya ki-imani. Muislamu mmoja alikuwa 'group study' moja na mimi. Rafiki yangu tangu Form I hadi Form IV na room mate wangu University. Huyu ndugu alikuwa mtaratibu na mpole sana. Enzi hizo pale UDSM mlimani kulikuwa na muungano wa wanafunzi wa kiislamu ulioitwa MSAUD. Na itikadi za MSAUD na za huyu rafiki yangu zilikuwa hazipishani sana (at least theoretically) na misimamo ya waislamu wa 'itikadi' kali. Kwa kuwa tulikuwa marafiki tulioshibana nilimuuliza kuhusu usahihi wa misimamo yake ya kidini, ya ki-MSAUD, ya kiislamu (itikadi kali). Rafiki yangu, kwa utaratibu kabisa, kwa ukweli wa moyoni, akaniambia chanzo cha msimamo wake ni KORAN yenyewe. Kwamba yeye anashikilia misimamo yake kwa sababu KORAN inamtaka afanye hivyo. Kama isingekuwa KORAN asingekuwa na misimamo hiyo.

  Sasa mimi sijasoma KORAN hata kidogo. Natamani kupatikane wasomi wa kiislamu wenye nia ya kutuelimisha kuhusu KORAN, kama misimamo ya itikadi kali ni ya ki_KORAN au ni uzushi. Na pia wapatikane wasomi wa ki-kristo wenye nia ya dhati ya kuelimisha wasioufahamu ukristo. Haya makundi mawili yakutanishwe ktk mdahalo wa ana kwa ana, wenye nia ya kujenga, lakini wenye nia ya kufahamishana ukweli toka mioyoni mwetu. Tufanye hivyo huku tukitarajia kwamba hoja zikipishana sana TUTAKUBALIANA KUTOKUKUBALIANA.

  Napendekeza mdahalo huu uandaliwe kinamna fulani na wazito wa JF. Kwa baadae utaweza kurushwa hewani, sote tuone na tusikie. JF itaweza ku-raise fund kwa mtindo huu toka kwa wadhamini wa kipindi maana ni wazi kipindi hiki kitakuwa hot-cake.

  Bado naamini kuna waislamu wengi hawana misimamo ya kiitikadi kali. Lakini tunataka wao kwa wao pia wasimame na watoe maoni kuhusu KORAN yao kama inafagilia itikadi kali au la. Na kama ni ndiyo basi tutafute namna ya kudumu ya kuishi huku waislamu wakitimiza KORAN na wakristo wakitimiza BIBLIA.

  Rafiki yangu huyu alinieleza kuwa KORAN inadai nchi itawaliwe na sharia.

  Sasa wasomi wengine wa kiislamu mnasemaje? Tukutane tutafakari mambo haya kwa uwazi na ukweli wa moyo. Inawezekana KORAN inadai hivyo na tunaposhindana na 'itikadi kali' tunapoteza muda. Tukiamua tunaweza kuleta kitu tofauti cha kuigwa duniani.

  Humu JF naona hoja kadhaa kuhusu suala hili nyeti zinakuja kimzahamzaha, utani, na matukano fulani. Tukiwa ana kwa ana tutakuwa serious zaidi. Mnaonaje?

  PENYE WENGI HAPAHARIBIKI NENO.

  NAWAKILISHA.
   
 2. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Mambo ya udini hayo,Ngoja nipite ka mshale
   
 3. R

  Rapture Man JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Perfect. Ni kweli kabisa ni udini. Asante kwa kuliona hilo. Ila nadhani ni bora tukalijadili kwa mtindo niliopendekeza maana 'udini' huu unatufuata mpaka vyumbani kwetu mkuu.
   
 4. peri

  peri JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kama unataka kuufahamu uislam unaweza tembelea Alhidaaya.com.

  Kwa mijadala ya masuala mbalimbali juu ya uislam na tafiti mbalimbali tembelea
  International Rectifier Home Page - Flash Detection au tafuta mijadala ya dr zakir naik.

  Moja ya mijadala mizuri kati ya waislam na wakristo na uliofanyika marekani mwanzoni mwa mwaka 2000, kati ya dr zakir naik na dr wilia campbel.

  Ulichoshauri ni kizuri ila ni kigumu sana kwa mazingira ya tanzania yetu.
   
 5. M

  Magwero JF-Expert Member

  #5
  Oct 14, 2012
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 243
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Ni wazo zuri sana,,,ila utekelezaji wake ni mgumu kidogo...
  Imani hizi mbili ya Islam na Kristo zimesimamishwa na watu wawili tafauti na waliokuwa na approach tofauti kabisa katika mafundisho na uenezaji wa imani..!!

  YESU ambaye yeye ni kiongozi wa kundi letu...aliongeza kundi na wafuasi wake kwa njia za kidemokrasia(majadiliano na mahubiri)kila aliyeamini na kukubali alipata kibali kufanyika kuwa mwana wa aliye Juu...
  Akiondoka ulimwengini akiubiri habari ya kusameeana na Kupendana pasi na mipaka uku akituamrisha kuwapenda Adui zetu zaidi...
  Akiwaacha mitume na wanafunzi wake akisema "tazameni nawatuma kama kondoo kati ya kundi la Mbwa mwitu"
  ni lugha ya picha hii, nani kondoo? ni wale waliotumwa na nan Mbwa mwitu..? unaweza ukajazilizia hapo...
  Tena iweni wapole kama kondoo na waelevu kama nyoka...

  Nageukia upande wa pili wa sarafu...

  Muhamadi ndiye kiongozi wa waislamu,mtume wa mwisho na kipenzi cha mungu wao(allaah...)

  Alieneza imani islam kwa njia ya Vita(jihadi),,kila aliyempinga na kuupinga uislamu aliuwawa(dictorship)....
  Akiondoka ulimwenguni aliwataka waislamu kuilingania imani yao...kuipigania kwa Ajili ya allah...!!

  Sasa unaweza kuona,,nyumba hzi mbili zimejengwa kwa misingi tofauti...
  Natamani endelea ila ngoja niachie hapa..
  Ntarudi..
  Asalaam aleikumu..
   
 6. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #6
  Oct 14, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hiyo kazi tuwaachie kile kikundi chetu cha "Biblia Inajibu"
   
 7. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #7
  Oct 14, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  siungi mkono hoja hawa wenzetu wajua reaction zao? Hawatak kuheshimu iman za wengine na ni watu wa kuover-react,refer incident ya mbagala sasa wa2 kama hao mtajadil nn nao?
   
 8. M

  Magwero JF-Expert Member

  #8
  Oct 14, 2012
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 243
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  U dnt nid 2b afraid abt ths...
  We need 2 educate ths warmans...
  Kama unaimani ya Kikristo kupita hapa kama mshale ni sawa na kukata tiketi ya kuingia kwny ziwa la moto lisilo zimika..
  Kwani yeye mwenyewe anasema "atakaye nikana mbele ya wanadamu nitamkana Mbele ya Baba yangu" unaweza juu anamanisha nin kwa atakaye mkiri...!!
  Hata ukinyamaza hawatakuacha hawa wavaa vipedo wakianzisha balaa..
  Stand up tall and say "Jesus is the world Greatest.."
   
 9. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #9
  Oct 14, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hamna haja ya kuwa na kitu kama hicho na wala hakina manufaa yoyote. Hapa JF tayari kuna jukwaa la dini. Nafikiri kule iman zote zimechambuliwa kiundani kwenye thread mbali mbali. Kama upo nterested kufahamu, usiwe mvivu, tembelea tu jukwaa la imani!!
   
 10. M

  Magwero JF-Expert Member

  #10
  Oct 14, 2012
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 243
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Wew utakuwa unafanya nin..?!
  Ukae tu,,,Yesu kasikitishwa na kauli yako...its ur right and obligation in everywhre,in nomatta situation, no post kuitangaza injiri kwa maneno na kwa vitendo...
   
 11. s

  sally21 Member

  #11
  Oct 14, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wameshaireport sasa hivi inakuja kufutwa hii thread yako
  wapunguzieni kazi za zisizozalazima mamods
   
 12. R

  Rapture Man JF-Expert Member

  #12
  Oct 14, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Active ni super moderator na ame-like!
   
 13. R

  Rapture Man JF-Expert Member

  #13
  Oct 14, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Kamanda peri, kwa jinsi ulivyoteremsha points hizo, hata kama una itikadi kali, naona unaweza kabisa ku-present issues katika mdahalo kwa style itakayokubalika kabisa kwa wakristo. Mawazo yangu ni kwamba waislaimu wa mind-set kama yako watakuwa wa kwanza kushiriki, then kwa baadaye hata type ya Ponda wakaribishwe.

  Sasa mie ni mkristo na kwa mtizamo wangu nimeenda mbali sana ktk ukristo na haiwezekani kugeuka. I have reached an irreversible state. Sasa kunaweza kuwa na muislamu ambaye ktk uislamu wake naye kafika irreversible state. Pia kuna kundi hapo katikati la waislamu na wakristo ambao wanaweza kuhama toka upande mmoja kwenda mwingine wakisikiliza nguvu ya hoja toka kwa waliobobea.

  Mimi naamini na nadhani na wewe unaamini kuwa dini inasambazwa na juhudi ya binadamu lakini pia na juhudi ya Mungu Mkuu (ingawa hatuwezi kuona waziwazi role yake). Sasa katika mdahalo ninaoupendekeza nguvu hiyo ya Mungu ndiyo itakuwa determinant ya hili kundi la kati linafuata mwelekeo upi. Upande watakaokwenda wengi ndo tukubali kuwa utakuwa umeshinda. Wakristo wakishindwa warudi darasani wakajifunze upya au wasilimu. Waislamu wakishindwa nao pia warudi darasani au wabatizwe tu. Tuendelee kuboresha hili wazo na kama halifai nalo tutalizima tu. Big Up.
   
 14. R

  Rapture Man JF-Expert Member

  #14
  Oct 14, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Mkuu, nafahamu kabisa nguvu hizo mbili ambazo ziko 'opposite' kabisa. Lakini katika fimbo ya Moses na ya Farao, ni ipi ya wakristo na ipi ya waislamu? Wewe unajua uko upande wa fimbo ipi, lakini huenda wenzio hawajui. Tupange kuzungumza kwa nia njema halafu hizo fimbo mbili (nguvu ya hoja - ambayo iko backed up by the Power of God - Yahweh, Allah - whatever the name) zitakapogeuka nyoka na mmoja kummeza mwingine ndo tutajua nani anafuata njia sahihi.
   
 15. R

  Rapture Man JF-Expert Member

  #15
  Oct 14, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Kamanda peri, kwa jinsi ulivyoteremsha points hizo, hata kama una itikadi kali, naona unaweza kabisa ku-present issues katika mdahalo kwa style itakayokubalika kabisa kwa wakristo. Mawazo yangu ni kwamba waislaimu wa mind-set kama yako watakuwa wa kwanza kushiriki, then kwa baadaye hata type ya Ponda wakaribishwe.

  Sasa mie ni mkristo na kwa mtizamo wangu nimeenda mbali sana ktk ukristo na haiwezekani kugeuka. I have reached an irreversible state. Sasa kunaweza kuwa na muislamu ambaye ktk uislamu wake naye kafika irreversible state. Pia kuna kundi hapo katikati la waislamu na wakristo ambao wanaweza kuhama toka upande mmoja kwenda mwingine wakisikiliza nguvu ya hoja toka kwa waliobobea.

  Mimi naamini na nadhani na wewe unaamini kuwa dini inasambazwa na juhudi ya binadamu lakini pia na juhudi ya Mungu Mkuu (ingawa hatuwezi kuona waziwazi role yake). Sasa katika mdahalo ninaoupendekeza nguvu hiyo ya Mungu ndiyo itakuwa determinant ya hili kundi la kati linafuata mwelekeo upi. Upande watakaokwenda wengi ndo tukubali kuwa utakuwa umeshinda. Wakristo wakishindwa warudi darasani wakajifunze upya au wasilimu. Waislamu wakishindwa nao pia warudi darasani au wabatizwe tu. Tuendelee kuboresha hili wazo na kama halifai nalo tutalizima tu. Big Up.
   
 16. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #16
  Oct 14, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,105
  Likes Received: 7,362
  Trophy Points: 280
 17. R

  Rapture Man JF-Expert Member

  #17
  Oct 14, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Mkuu, nafahamu kabisa nguvu hizo mbili ambazo ziko 'opposite' kabisa. Lakini katika fimbo ya Moses na ya Farao, ni ipi ya wakristo na ipi ya waislamu? Wewe unajua uko upande wa fimbo ipi, lakini huenda wenzio hawajui. Tupange kuzungumza kwa nia njema halafu hizo fimbo mbili (nguvu ya hoja - ambayo iko backed up by the Power of God - Yahweh, Allah - whatever the name) zitakapogeuka nyoka na mmoja kummeza mwingine ndo tutajua nani anafuata njia sahihi.
   
 18. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #18
  Oct 14, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
 19. R

  Rapture Man JF-Expert Member

  #19
  Oct 14, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Shark, kwa maoni yangu tulishachonganishwa tayari. Tunatafuta dawa ya ku-neutralize uchonganishi huu kabla haujafika kiwango kikubwa. Haya great thinkers, christians and muslims, keep talking tuone hili kama linawezekana au la.
   
 20. peri

  peri JF-Expert Member

  #20
  Oct 14, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  mkuu suala la mdahalo linawezekana kama tutakuwa na nia safi ya kutaka kuujua ukweli ili kuufuata bila kumtukana wala kumkashifu yoyote.

  Tatizo kubwa wengi tunachukulia suala la mdahalo kama njia ya kutugawa na kutugombanisha na sio njia ya kuelimishana ili tuijue kweli na kweli ituweke huru.

  Nb: irf niliyokuambia utembelee inasimama kwa niaba ya islamic reserch foundation taasisi inayoongozwa na dr zakir naik. Natumia sim ndiomana nimeshindwa kuiweka vizuri.
   
Loading...