Napendekeza liandaliwe tamasha la kuchangia matibabu ya Professor Jay

sinza pazuri

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
2,521
7,368
Napendekeza wadau wa sanaa pamoja na familia ya Professor Jay wakae chini waandae tamasha la kukusanya pesa za kusaidia matibabu ya Professor.

Jay sio tu ni msanii mkali lakini pia anaishi vizuri sana na jamii yake...Ni yule brother fulani hanaga noma hana makuu anaishi vizuri na wadau wote kwenye sanaa na nje ya sanaa.

Lakini pia Jay kachora ramani ya huu muziki wa Bongo Fleva, bado tuna deni la kumlipa Jay kwenye muziki kaitoa sanaa mbali sana.

So, lipigwe bash fulan la kilijendi mimi kwa uzoefu wangu wa hii industry inaweza patikana pesa ya kumuuguza hata mwaka mzima.

Milioni 4 kila wiki kiukweli familia haiwezi kumudu hiyo gharama hata kama wana akiba kiasi gani.

Kama Ruge alichemka akapitisha bakuli, why not Prof?

jaytunakuzimia@yahoo.com

20220209_175734.jpg
 
Nimemchangia kwa kweli ila MACHADEMA ni hovyo sana yaan iwamentelekeza kabisa huyu Mbunge aliewapa ruzuku zote hizo. Hata kutoa taarifa yake kimya.

Mpaka mke wake anasema eti wanaopiga tu simu kweli kweli hovyo sana Halafu hii michango wasisogeze pua hasa Mnyika na genge lake.
 
Nimemchangia kwa kweli ila MACHADEMA ni hovyo sana yaan iwamentelekeza kabisa huyu Mbunge aliewapa ruzuku zote hizo. Hata kutoa taarifa yake kimya. Mpaka mke wake anasema eti wanaopiga tu simu kweli kweli hovyo sana Halafu hii michango wasisogeze pua hasa Mnyika na genge lake.
Politics haina nafasi kwenye ugonjwa wa Prof. Hii ni family issue.
 
Hiyo show iwahusu wasanii woteeeee,tena ifanyike mikoa 5 Dar, Arusha,Mbeya,Mwanza na kigoma.

Itapatikana fedha ya kutosha sanaaaa
 
Kama Kaka yangu professor jay anatembezewa bakuli hivi,nawaza walalahoi wa nchi hii wana hali gani kwenye masuala ya matibabu.
Kama ni mlalahoi unaumwa figo wasaidie ndugu zako waambie wakuache upumzike.
Matibabu ya figo mpaka Ruge alichangiwa na nyumba aliuza.
 
Kama familia imeomba kuchangia tuchangie lakini kama wahuni tu acheni isije ikawa mtu anakwenda kuoa
 
Back
Top Bottom