Napendekeza kwenu kuwa Ridhiwani Kikwete atatufaa sana Urais baada ya Magufuli

Amefanya kitu gani cha maana.

Kwenye urais huko mbali hebu tumkague kwenye nafasi yake ya ubunge tu amefanya nini cha maana,kuna ushujaa gani wa maana alioufanya hadi wewe ushawishike kwamba anafaa urais...
Makonda tena! Yani unaruka mavi unakanyaga mkojo, hawa wachunga ng'ombe hatuwataki tena.
 
Hukunielewa maana yangu sikusema Makonda anafaa kuwa Rais soma kwa umakini.

Nimemaanisha hivi pamoja na madhaifu aliyokuwa nayo Makonda lakini ni mchapakazi kumzidi huyo Ridhiwani Kikwete ambaye yupo yupo tu, jina la baba yake tu limembeba
Makonda tena!,Yani unaruka mavi unakanyaga mkojo,hawa wachunga ng'ombe hatuwataki tena.
 
Mambo mengine kabla ya kupost uwe unashaurisha watu wanaokuzunguka.

Umeandika pumba tu hapa, Huyu hata ukatibu wa wizara hafai.
Wizara mbali sana, wa Kata wenyewe hastahili asubiri kubebwa kwenye ubunge basi
 
We Ridhiwani unajiharibia mwenyewe hapa kwa kuji mwambafai unafaa. Kaa kimya jiwe ana jina lake tayari na hapangiwi. Inamaana hili hulijui?!
Majaliwa anaandaliwa na form ya kugombea ita printiwa moja tu.
 
Sisi tuko bize na kubadilisha katiba, ili sisi wa Chato tutawale hadi milele.
 
Baada ya kuifanya Zanzibar nchi ya kifalme mnataka na huku pia mtuletee hizo habari.
 
Sema umekataa wewe usiwasemee wengine. Sioni kijana wa kushindana na Ridhiwani katika medani ya uongozi. #RK2025
Naona Ridhiwani kakutuma uje umpigie kampeni. Ila ni kwambie si kwa serikali hii. Hatopewa nafasi
 
Back
Top Bottom