FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 36,023
- 40,693
Huu hautakuwa mkopo wa kwanza kwa NSSF kuutoa kwa Serikali, Mabibo hostel, General Tyres upgrading, Machinga Complex na miradi mingine mingi isiyo na tija imepata mikopo toka NSSF, iweje kwa daraja la Kigamboni isiwe tu mkopo na ukalipwa taratibu na serikali kwa riba?
Hii itapanua wigo wa biashara kwa kuruhusu usafirishaji wa abiria na mizigo bila vinzingiti hivyo kuchagiza kasi ya maendeleo kwa ujumla.
Pia wale watumishi wenye degree na masters wanaokaa kaa kihasara hasara pale kwenye vibanda wakikusanya mia mbili mia mbili kama makonda wa daladala watapangiwa kazi zingine zenye tija zaidi.
Vinginevyo hata daraja la Kigongo busisi nao walipishwe? Hii ni haki? Na ukizingatia tayari tunakamuliwa tozo kama zote?
Tujadili.