Napendekeza kusiwe na wakuu wa wilaya bali wilaya ziongozwe na wakurugenzi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Napendekeza kusiwe na wakuu wa wilaya bali wilaya ziongozwe na wakurugenzi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by baraka moze, May 28, 2012.

 1. b

  baraka moze Member

  #1
  May 28, 2012
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Na pia mkuu wa mkoa achaguliwe kwa kupigiwa kura kipindi cha uchaguzi mkuu
   
 2. K

  Kimbito nyama Senior Member

  #2
  May 28, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 157
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabisa kwani kivitendo kazi za mkuu wa Wilaya ni 1) kumpokea Rais, waziri mkuu au viongozi wa kisiasa wanapofika wilayani kwao kazi inayoweza kufanywa na Meya au Mwenyekiti wa Halmashauri.2) Kusuluisha migoro mbalimbali ya wananchi pindi inapotokea kama ya wafugaji na wakulima- jukumu ambalo OCD akishirikiana na mkurugenziwa Halmashauri anaweza kulifanya 3) kusimamia ulinzi na usalama wa wilaya(kisiasa zaidi)- jukumu ambalo OCD anaweza kulifanya bila siasa. Ukipiga mahesabu ya matumizi kwa Landcruiser 133, maderereva 133, secretary 133, wahumudumu wa ofisi 266, na Ma-DC 133 ukilinganisha na tija haviewezi kuendana kabisa. Hata wakuu wa Mikoa nao ni kuangalia sana kama wanahitajika kwani kuna RAS n.k
   
 3. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #3
  May 28, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,085
  Trophy Points: 280
  hili pendekezo lako ni sawa na kusema "napendekeza serikali ipunguze anasa (V8)"!
  Kila aliyemo anajua kuwa hawa jamaa hawapaswi kuwepo na hawatakiwi ila ni area ya 'tuzo' za washirika na washikaji.
  Cha msingi hapa ni kutekeleza na waliopo serikalini hawawezi kufanya hivyo
   
 4. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #4
  May 28, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Sio tu ma-DC hata Ma-RC hawatakiwa kuwepo mda wa kupeana ulaji at the expense of common mwananchi umepita. DCs and RCs hawana kazi.
   
 5. Jiwe Linaloishi

  Jiwe Linaloishi JF-Expert Member

  #5
  May 29, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 3,736
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  siyo DC na RC tu ambao hawatakiwi hata manaibu mawaziri na makamu wa rais hawana kazi wanayofanya, pili mawaziri wasiwe wabunge ili bunge liweze kuiwajibisha serikali vizuri na hili tulivalie njuga hasa kwenye hii katiba mpya.
   
 6. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #6
  May 29, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Ingekuwa poa sana, Maana hawa wakuu wilaya ni mzigo tu kwa mlipa kodi.

  Sijawahi kusikia kitu chochote kizuri kutoka kwa wakuu wa wilaya zaidi ni ma gharama kwetu!
   
 7. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #7
  May 29, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Hawa ma naibu waziri kwakweli ndio buree kabisa, maana hata hatujui kama wanakuwaga na kazi.

  Huko Kenya miaka 3 iliyopita ma naibu waziri walilalamika kwamba hawapewi kazi za kufanya.
   
 8. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #8
  May 29, 2012
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Ushauri Mzuri: Ila naomba nikuelimishe kisha nikuache na swali.

  1.Elimu
  Mkurugenzi anawajibika kwa Halmashauri (Serikali za Mitaa)
  Mkuu wa wilaya ni mwakilishi na anawajibika kwa (Serikali Kuu);
  2. Swali
  Kwa kuwa Serikali kuu na Serikali za Mitaa zimewekwa wazi kwenye katiba... Je ni nani atakayekuwa mwakilishi wa Serikali kuu katika ngazi ya wilaya? Na je kama mwakilishi wa serikali hatakuwepo kwenye ngazi ya wilaya... si ndio kwamba taifa linakuwa vipande vipande vinavyojitegemea?

  Asante.
   
 9. B

  BigMan JF-Expert Member

  #9
  May 29, 2012
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,097
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Mimi navyoona tatizo kubwa humu ni kwamba idadi kubwa ya watu hawana uelewa wa elimu ya uraia kama vile zamani tulivyokuwa tunasoma somo la siasa kuanzia darasa la kwanza,kila mtu anafahamu jinsi wakurugenzi wa halmashauri za wilaya ya wataalamu wao wanavyokula fedha za walipa kodi bila ya huruma kwa kuidhinisha fedha za miradi hewa na iliyoko chini ya viwango,miongoni mwa majukumu ya wakuu wa wilaya ni kupata orodha ya miradi hiyo,kiasi cha fedha na kuikagua kama wanahofu nayo ni jukumu lao kumfahamisha cag ili kutuma wakaguzi ama kuagiza takukuru kuingilia kazi.

  Ok wengi wenu hasa cdm mnapendekeza kuondolewa kwa nafasi hii lakini lazima mjue kuwa miaka kichache ijayo mtaingia madarakani hali itakayokuwepo itawatesa na mara nyingi uzoefu unaonyesha kuwa kutaka sheria fulani kwa ajili ya kumkomoa fulani mwisho wa siku umkomoa yule aliyefanya fitina.

  Nafasi hizo ni muhimu kwa chama chochote kinachotawala kwanza katika kuhakikisha kinafanikisha malengo na sera ikiwemo ilani ya uchaguzi lakini pili kuwa wawakilishi wa rais aliyeko madarakani ambaye hawezi kwa wakati mmoja kuwa katika wilaya zote 133.wakurugenzi ni waajiriwa hawana uchungu na serikali inayotawala huu ndiyo umuhimu wa dc toka utwala wa kikoloni mpaka serikali huru za kiafrika
   
 10. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #10
  May 29, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kama wawepo wachaguliwe na Wananchi toka Vyama Vya Upinzani na Walipwe na Kodi za Wananchi za Wilaya hizo na Sio Serikali kuu; Kwahiyo hao wakuu wa Wilaya watahamasisha Ulipwaji wa Kodi; Utengenezaji wa Barabara za Wilaya, Usafi wa Wilaya, Utoaji wa Kazi Wilayani kuondoa Watoto Wazururaji.

  Hiyo itahamasisha kazi na uhamasishaji wa Vijana toka wilayani na Uwajibikaji wa hao waliochaguliwa Wilayani kuliko kupeana kwasababu ni Marafiki pale kijiweni au Baba anamujua baba yangu; na sie ambao hatuna baba Je?
   
 11. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #11
  May 29, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Mkurugenzi wa wilaya chini yake kuna watumishi zaidi ya 200. Mkuu wa wilaya ana watumishi 4 tu. Ila we sema nafasi za u dc ni kwa wale walioshindwa kwenye majimbo, na wale waliosaidia kufanikisha wizi wa kura chini ya utawala wa ccm.
   
 12. S

  Sting007 JF-Expert Member

  #12
  May 29, 2012
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 275
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Naunga mkono hoja.....!
   
 13. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #13
  May 29, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,072
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  mawazo yote yanayo husu tanzania yapelekwe kwenye tume ya katiba ya mh. warioba.
   
 14. Kiatu cheusi

  Kiatu cheusi Member

  #14
  May 29, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 35
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Nakuja tena kwa wana JF: Ndugu wana jf hivi huyu jamaa analengo gani na wa TZ kupitia hawa wakuu wa wilaya? Maana sioni kazi ambayo wanakuja kufanya maana kazi hizo tayari zina watu wa kuzifanya na watu hawa wamewekwa ili kuongeza umasikini kwa wa TZ maana bajeti watayotumia ilitakiwa kwenda sehemu zingine kama upande wa Afya.
   
Loading...