Napendekeza kusitishwa au kubadilishwa elimu yetu

MusuKuma

Member
Jan 30, 2021
33
87
Mimi ni mdau wa Elimu, napendekeza Sana tuweze kubadili mfumo mzima wa Elimu kwa kuwa pengine inaweza kutokuwa na faida ya kujinasua na wimbi la umasikini.

Miaka Michache ijayo tutakuwa na ongezeko la watu wengi Sana watakao kuwa wahanga wa ukosefu wa ajira.
Kipi kifanyike.

1: Tufundishwe sitadi za vitendo kuanzia kidato Cha 1-4 baada ya hapo watu watumie hiyo elimu Yao kwa manufaa ya maisha Yao atakaye taka kuelee kusoma asome kwa msingi wa kutoajiliwa yaani asitegemee ajira popote pale Ila akipata Basi ashkru.

2: Tubadili mfumo wote wa Elimu kuanzia vidudu Hadi elimu ya mwisho. Mwanangu akiingia vidudu awe anajua kabisa yeye ni driver au yeye ni mwashi.

Kwa kufanya hivyo tutanusuru Sana kizazi chetu.

Hebu fikilia Kuna watu wangapi waliomaliza four au chuo mwaka Jana vipi mwaka juzi vipi mwaka kesho n.k je wanaenda wapi?

Serikali inamishahara yakuwalipa hao wote? Vipi miradi au maendeleo ya nchi yatafanyika?

Kama itakuwa vizuri na iwe hivyo.
 
Elimu haiwezi kusitishwa. Na kubadili mfumo wa elimu ni suala linalohitaji maandalizi ya kutosha na siyo kukurupuka tu vu bin vu. Ni suala la pole pole hatua kwa hatua.

Hiyo elimu ya vitendo itakuhitaji ubadili mitaala, uandae walimu wa kutosha, ujenge karakana; na mengine mengi.

Kaa ufikirie vizuri, uandike maoni yako yawe katika uhalisia badala ya mihemko tu. Tena ufanye na utafiti kidogo kama mfumo huu unaopendekeza wa mtoto kuingia chekechea akijua kuwa atakuwa dereva upo mahali po pote pale duniani ana sisi ndiyo tutakuwa wa kwanza. Kama upo, zipi changamoto zake?

Wasiliana pia na Mh. Kimei umpe maoni yako haya (baada ya kuyaandika vizuri)

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom