Napendekeza kodi ya uzalendo kwenye tiketi za mabasi ili tukamilishe SGR haraka zaidi

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Naona serikali siku hizi imekuwa hodari sana wa kupokea ushauri wa tozo za serikali kwa kisingizio cha uzalendo bila hata kuzifanyia utafiti wa kina kuona kama kuna socioeconomic impacts za tozo hizo. Serikali sasa inaendeshwa kwa njia ya "hapendwi mwananchi bali kodi yake"

Mwigulu amekuwa mbunifu hadi amegundua kodi mpya inaitwa Covid-19 import duty, inayotozwa mtu anapoingia nchini kutoka nje.

Basi na mie napendekeza serikali ianzishe tozo kwenye ticket za mabasi ili tukamilishe haraka ujenzi wa SGR. Zungu na Nchemba mpo, mnasemaje kuhusu kodi hii nyingine ya uzalendo? Kwanza nyie hampandi mabasi kwa hiyo haitawasumbua, hivyo ipite tu.

Hebu tuangalie hadi sasa tuna tozo za kishikaji ngapi ndani ya miezi sita tu
  • Tozo la kuuza samaki kwenye viwanda vya minofu
  • Tozo la kutuma muamala
  • Tozo la kupokea muamala
  • Tozo la wakala wa simu kukupa muamala wako
  • Tozo la kununua mafuta ya kupata hela ya barabara vijijini
  • Tozo la kununua vocha ya simu
  • Tozo la mwenye nyumba kupitia luku
  • Tozo ya kukupima kama umeleta Covid-19 nchini (Covid-19 import duty)
 
Back
Top Bottom