Napendekeza JULIO APEWE MKATABA RASMI KUINOA TIMU YA VIJANA

commonmwananchi

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,377
1,952
kwa mafanikio yaliyofikiwa na timu yetu ya taifa vijana kwa kuitoa CAMEROON.na kuweka historia mpya ya soka nchini,kocha mzawa JAMHURI KIHWELU apewe mkataba rasmi na TFF na hii itawapa motisha zaidi wengne wenye uwezo na vipaji nchini..kuliko kuendelea kuwathamini makocha wa kigeni pekee,huku tukiwaacha wazawa wenye kuonyesha uwezo kama hao wgeni.
 
Big up sana hiyo!! tunahitaji watu wenye vipaji kila idara siyo kwenye michezo tu!!
 
Tena na mshahara wake na marupurupu uwe kama hao wawili wa kigeni waliotangulia au zaidi...nyie TFF msianze kuleta za kuleta...tunataka reform ya ajira na mishahara asap nyanga zote tz..
 
Tena na mshahara wake na marupurupu uwe kama hao wawili wa kigeni waliotangulia au zaidi...nyie TFF msianze kuleta za kuleta...tunataka reform ya ajira na mishahara asap nyanga zote tz..
Tuko pamoja. Baada ya hapa tutacheza na timu gani?
 
Africa Men's 2012 Olympic Qualifier draw set for 13th April 2011 in Cairo

The draw for the second round of the London 2012 Olympic qualifiers for Africa will be conducted at CAF HQ in Cairo, Egypt on the 13th April at 10am. Sixteen (16) teams will enter the draw with home and away matches to be played on 3, 4, 5 June 2011 for first legs and the return legs on 17, 18, 19 June 2011. The next and final stage will see the introduction of a new qualifying system that is to be further communicated but three teams are going through to represent CAF at the London 2012 Olympics with a fourth African team going to meet a team from Asia in a play-off match to be held on 12th April 2012 in London, UK.

Source: CAF website
 
Africa Men’s 2012 Olympic Qualifier draw set for 13th April 2011 in Cairo

The draw for the second round of the London 2012 Olympic qualifiers for Africa will be conducted at CAF HQ in Cairo, Egypt on the 13th April at 10am. Sixteen (16) teams will enter the draw with home and away matches to be played on 3, 4, 5 June 2011 for first legs and the return legs on 17, 18, 19 June 2011. The next and final stage will see the introduction of a new qualifying system that is to be further communicated but three teams are going through to represent CAF at the London 2012 Olympics with a fourth African team going to meet a team from Asia in a play-off match to be held on 12th April 2012 in London, UK.

Source: CAF website
 
Ni wazo zuri sana, ila mimi najiuliza hivi tuna timu za vijana ngapi zilizo hai?
Serengeti Boyz iliishia wapi?
Kakakuona pia iliishia wapi?
Under 20 ile iliyoundwa baada ya Coca Cola Cup final iliyojumuisha mikoa yote ipo wapi? na timu nyingi nyingi tu za vijana ambazo baada ya mashindano kuisha basi vijana wanapoteana.

Sishangai hata hii timu ikapotea baada tu ya mashindano hayo. Mikakati mingi utekelezaji hafifu hivi kweli tutasogea tunapotaka tufike? Bila kuwekeza kwenye Kandanda tusahau kufikia level ya nchi kama Cameroon, Misri, Tunisia, Ghana, Nigeria.

Kuwafunga Cameroon si kigezo kwamba tunaweza, cha msingi ni kuifanya timu hii itake over in next two years by then watakuwa na miaka 25 average.

Natoa Pongezi zangu za dhati kwa Julio, ni kocha mzalendo na anakipaji cha kupandisha mori na ari ya ushindi kwa timu anayofundisha, ni kweli style yake ni sawa na Jose wa Madrid, anacheza na saikologia na wachezaji na hii ipo katika makocha wachache duniani.

Bravo naunga mkono akabidhiwe timu - na hii timu iwe ya kundumu.
 
kwa mafanikio yaliyofikiwa na timu yetu ya taifa vijana kwa kuitoa CAMEROON.na kuweka historia mpya ya soka nchini,kocha mzawa JAMHURI KIHWELU apewe mkataba rasmi na TFF na hii itawapa motisha zaidi wengne wenye uwezo na vipaji nchini..kuliko kuendelea kuwathamini makocha wa kigeni pekee,huku tukiwaacha wazawa wenye kuonyesha uwezo kama hao wgeni.
Julio ni kama Morinho anajua sana kuhamasisha sijapa kuona kocha mhamamishaji kama Julio kwa hapa bongo,mungu alimpa kipaji cha kuongea pia
 
:yield:

Me nadhani Julio angepewa timu za vijana...

Huyu ni mhamasishaji mzuri na atawajenga mapema kuwa vifaa vizuri kuja kutumiwa huko baadae...

Wachezaji hujengwa katika hatua za umri wa chini, hivyo ni bora awajenge mapema kwa kipaji chake kuliko kupewa timu ya taifa ya wakubwa halafu aje apokee mibwanyenye ambayo haijafunzwa mapema toka udogononi

Si unajua tena, samaki mkunje...

Pia cha muhimu kuanzia sasa TFF wampe posho la kutosha ili awe na morale ya hali ya juu kufundisha vijana hawa na kutuandalia timu bora ya taifa hapo baadae

Nawasilisha
 
Kwa mafanikiwa haya Julio anastahili kukabidhiwa timu kimkataba hili litampa hamasa katika utendaji wake na pia iwekwe mikakati ya kumuendeleza kimasomo katika nchi zilizo piga hatua mbele kimaendeleo ya soko
 
Hongera Julio na Manyara starz. Tunaelekea kuukimbia ukichwa wa mwendawazimu
 
Big up Julio aendelee moyo wa kuhamasisha timu, TFF wampe mkataba na marupurupu stahili
 
hivi, hii timu (Manyara Stars) ndiyo ile ilikuwa ikiitwa Ngorongoro au ni timu tofauti? Kama kuna anayefahamu naomba ufafanuzi!
 
hivi, hii timu (Manyara Stars) ndiyo ile ilikuwa ikiitwa Ngorongoro au ni timu tofauti? Kama kuna anayefahamu naomba ufafanuzi!

Mkuu,

Serengeti Boyz=Under 17
Ngorongoro=Under 20
Manyara Stars=Under 23
Kakakuona=Bara siku hizi ikijlikana kama Kilimanjaro Stars
Taifa Stars=Kili Stars+Mapinduzi Stars(hata km Unguja hawatakuwa na mchezaji)

Hii ni kadri nielewavyo.
 
Back
Top Bottom