Napendekeza jengo la Machinga Complex libadilishwe matumizi, liwe hospitali

Twinawe

JF-Expert Member
Oct 3, 2016
2,363
5,108
Habari za uzima Ndugu zangu poleni na pilika za hapa na pale katika kutafuta riziki hasa katika kipindi hiki tunakabikiwa na changamoto kubwa za kiuchumi.

Kwanza nipende kuishukuru serikali kupitia wizara husika kuwajali wafanya biashara wadogo hadi likapatikana wazo la kuwajengea jengo la kisasa la Machinga Complex.

Tangu jengo hilo lizinduliwe nadhani halijawai kutumika sawasawa na ilivyokua kusudio zaidi limekua sehemu ya watu wasio na pa kwenda mjini kukaa, kuvuta bangi godown nk.

Kutokana na changamoto ya Huduma za afya hapa jijini dar es salaam naiomba serikali kupitia mamlaka husika ikiwemo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Tamisemi, Wizara ya Viwanda na Biashara, hilo jengo mlibadilishie matumizi liwe tu hospitali na iitwe Jakaya Mrisho Kikwete, nadhani itafaa saana.

Nawasilisha
 
Kwamba tumezoea biashara za kutandaza chini au zile za ground floor, kupandisha kule juu shida?
 
Kwa hospital mazingira sio rafiki sahihi litumike Kama hostel za Wana vyuo vya cbe, DIT, IFM, mzumbe, UD, Ustawi, nk linaweza beba jumla ya wanachuo 5000 Mara laki mbili kwa chumba kimoja chenye vitanda 4 ni sh bilion moja litaingiza Mara miezi 12 ndani ya miaka 2 tu pesa za ujenzi zimerudi, huku likiwa limetatua shida za upangaji kwa wanafunzi
 
Machinga complex ni moja ya miradi mweupe isiyoshirikisha watumiaji, Kama ilivo shida ya watawala kuamini ukiwa kiongozi unajua kila kitu na kupelekea watumiaji kutoshirikishwa.
Huwezi tenganisha machinga na stand,
Stand ya gerezani inatakiwa izungushiwe uzio pande zote na ziwe frem ndani kwa nje pande zote hapa jiji alikosi si chini ya maduka 2000 mara laki 3 kwa mwezi ni sh milioni 600 kwa mwezi kwa mwaka ni bilion 7.2 achilia ushuru wa daladala kwa siku.
 
Habari za uzima Ndugu zangu poleni na pilika za hapa na pale katika kutafuta riziki hasa katika kipindi hiki tunakabikiwa na changamoto kubwa za kiuchumi.

Kwanza nipende kuishukuru serikali kupitia wizara husika kuwajali wafanya biashara wadogo hadi likapatikana wazo la kuwajengea jengo la kisasa la Machinga Complex.

Tangu jengo hilo lizinduliwe nadhani halijawai kutumika sawasawa na ilivyokua kusudio zaidi limekua sehemu ya watu wasio na pa kwenda mjini kukaa, kuvuta bangi godown nk.

Kutokana na changamoto ya Huduma za afya hapa jijini dar es salaam naiomba serikali kupitia mamlaka husika ikiwemo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Tamisemi, Wizara ya Viwanda na Biashara, hilo jengo mlibadilishie matumizi liwe tu hospitali na iitwe Jakaya Mrisho Kikwete, nadhani itafaa saana.

Nawasilisha

Bange / Bangi uliyoijaribu 'Kuivuta' leo nakushauri usiirudie tena kwani imeshatuonyesha kuwa 'Ukiivuta' tu na 'Akili' zako zinapotelea na Moshi pia.
 
Jengo limejaa wafanyabiashara floor zoet unasema ni godown la wavuta bangi, we haupo bongo inawezekana ulipita tuu ukaoneshwa haoa ndio machinga complex hata ndani ukuingia.
We ndo haupo bongo
 
Habari za uzima Ndugu zangu poleni na pilika za hapa na pale katika kutafuta riziki hasa katika kipindi hiki tunakabikiwa na changamoto kubwa za kiuchumi.

Kwanza nipende kuishukuru serikali kupitia wizara husika kuwajali wafanya biashara wadogo hadi likapatikana wazo la kuwajengea jengo la kisasa la Machinga Complex.

Tangu jengo hilo lizinduliwe nadhani halijawai kutumika sawasawa na ilivyokua kusudio zaidi limekua sehemu ya watu wasio na pa kwenda mjini kukaa, kuvuta bangi godown nk.

Kutokana na changamoto ya Huduma za afya hapa jijini dar es salaam naiomba serikali kupitia mamlaka husika ikiwemo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Tamisemi, Wizara ya Viwanda na Biashara, hilo jengo mlibadilishie matumizi liwe tu hospitali na iitwe Jakaya Mrisho Kikwete, nadhani itafaa saana.

Nawasilisha
Wazo zuri. Ila baada ya maboresho ya barabara ya kawawa na uhuru itakua na matumizi makubwa sana kibiashara
 
Back
Top Bottom