Napendekeza iundwe Tume Huru ya kuchunguza kifo cha Hayati Magufuli

abdulhamis

JF-Expert Member
Aug 2, 2019
1,436
2,292
Habari Watanzania, lengo langu la kuanzisha huu uzi si kwa nia mbaya ila nikutaka tu kumaliza Maswali ya Watanzania wengi wanaoshuku kuwa Hayati Magufuli kafanyiwa hujuma.

Baada ya kuona mambo mengi yanayoendelea kwenye mitandao ya kijamii na mitaani, ni wazi kabisa baadhi ya watanzania walio wengi wanashuku kifo cha Hayati Magufuli na kudhani kuwa kifo chake kina hujuma.

Serikali iheshimu mawazo ya watanzania tunaotilia shaka kifo cha Rais wetu na izingatie kwa kuunda Tume huru ya uchunguzi.

Mimi Binafsi nikikumbuka tukio la ule Moshi uliomfuata Hayati Magufuli mkoani Mtwara alipokuwa kwenye Gari bila kujulikana wapi umetokea na kuzua Taharuki nazidi kuwa na mashaka kuwa huenda zile zilikuwa baadhi ya mbinu za kutaka kujaribu na zilishindwa Lakini waliojaribu hawakuacha.

Pia wasiwasi wetu unakuwa mwingi baada ya Habari kuwa nyingi za Hayati Magufuli kafariki kabla hata ya Serikali kutangaza huku picha za Gari la maiti ambalo lilibeba mwili kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii

Kwanini kina Tundu Lissu na Kigogo walikuwa wanapata taarifa na walikuwa na uhakika kabisa kuwa mzee lazima afe na asipo na wengine kusema kabisa mzee kafa

Kwanini kabla Magufuli yupo hai viongozi walianguka kama kuku tena wa karibu yake ila baada ya yeye kufa hamna kiongozi hata mmoja aliyekufa?

Huwezi kusema ule ulikuwa uchawi sababu hakuna uchawi na wala siamini uchawi kama upo.

Sasa ili kujiridhisha basi serikal ifanye uchunguzi na uchunguzi uwe wa wazi ili kufuta hii shauku ya Baadhi ya watu kwani ikiendelea hivi na Serikal kukaa kimya huwezi jua Baadaye itakuwa na madhara gani pia hutojua maadui baadae wanaweza kuutumia huu uvumi kama silaha so ni bora Serikali ilimalize kwanza ili suala kwani kila siku mambo yanazidi kupamba moto.

Video ya tukio la moshi hiyo hapo chini.

 
Naunga mkono hoja! Halafu Luhaga Mpina awe Mwenyekiti na Biswalo Mganga awe Makamu wake!

Livingstone Lusinde awe Mjumbe, Joseph Kasheku Msukuma awe Mjumbe, Ole Sabaya awe Mjumbe, Chalamila awe Mjumbe, Jenister Mhagama awe Mjumbe, Tulia awe Mjumbe, na Phillipo Mpango awe ndiye mlezi wa hiyo Tume.
 
Tuanze na nyerere maana ilisemekana mkapa ndio kamnaniliu ili abinafsishe mali za umma zikiwemo nyumba alizouza magu, badae akaja mkapa ikasemekana pia magu ndio master mind ili ajiongezee muda wa kutawala...lakini hata hiyo kamati itakuwa na uwezo wa kurudisha roho??
Duh..!
 
Watanzania hao wenye shuku na uchunguzi juu ya kifo cha mpendwa wetu JPM huwezi kuwakuta Jamii Forum au Twitter tuko wachache

Wengi sana hawana ACCESS ya hii mitandao miwili.
Yaaah na ndo wapiga kura halisi, pia wahudhuriaji kampeni, safari hii 2025 huyu mama atapiga kampeni sijui wapi na chama chake.

Ni heri aanze kusafisha kwa kutembelea wananchi.
 
Back
Top Bottom