Napendekeza itungwe sheria ya kuwaadhibu watu hasa Police wanao banbikia watu kesi za uongo.

Felix

JF-Expert Member
Mar 9, 2014
876
762
Habari wakuu.
Hii tabia ya Jesh la police kumkamata mtu na kumtangaza hadharan kwa uma kwamba ni mkosaji, mfano ni Jambaz, Gaidi, mwizi n.k. Na uma wote tukajua hivyo..

Ikidhibika mahakaman kwamba yule mtu si mkosaji bali alibambikiwa kesi na police kwsbb zao binafsi.

Napendekeza sheria itungwe adhabu ambayo angeipata mtuhumiwa bas akaipate police husika aliye andaa mashtaka ya uongo.

Na pia sheria itungwe na kuwataka jeshi la police lililotangaza kwenye vyombo vya habari mwanzo kuhusu mkosaji, Basi baada ya kudhibitika mahakaman mkosaji hana hatia, Bas Police warudi tena kwenye media na watangaze kumsafisha.

Kwa sasa hvi police au serikali wakishindwa mahakaman huwa wanapotea mazima mtaani husikii wakisema lolote.

Katika vitabu vya dini kama Biblia, kuna mfano wa kesi ya kusingiziwa aliyopewa Daniel chini ya mfalme Dario kati ya Mwaka 600-536 Bc. (Soma Daniel sura ya sita)

Hukumu yake Daniel ilikuwa ni kutupwa kwenye zizi la Simba wamtafune. Wale Simba walikuwa wanakaa siku 7 bila kula chochote hili wapate njaa Sana na walitumika kama ndo chomba cha kutoa haki.

Baada ya Daniel kuwekwa kwenye zizi la Simba, hao Simba hawakumtafuna. Ndipo mfalme akagundua Daniel hakufanya makosa bali alisingiziwa. Ndipo walio mshitaki wakawekwa wenyewe kwenye zizi na Simba wakapata hapetite na kuwatafuna wote.

Nadhan hii ingerudia hapa kwetu. Tungeogopa kusingiziana. Lakini pia ingesaidia baadhi ya police kuacha kulichafua jeshi zima wakati tu kuna wengine wanafanya Kaz kwa haki na nzuri Sana.

Nawakilisha kwenu wanasheria.
 
Polisi anaruhusiwa na sheria kushuku au kuhisi mhalifu ivyo anaweza kukukamata na kukuachia baada ya uchunguzi.
 
Back
Top Bottom