Napendekeza barabara ya Morogoro ikikamilika ipewe jina la Hayati Magufuli

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
3,845
2,000
Ili kuenzi Jitihada za Hayati Magufuli katika upanuzi wa barabara ya Morogoro kuanzia Kimara mwisho hadi maeneo ya Kibaha kwa njia 8, endapo ujenzi wa barabara hiyo utakamilika napendekeza kwa heshima na kwa kuzingatia jitihada kubwa aliyoifanya Hayati Magufuli basi barabara hiyo iitwe Magufuli badala ya Morogoro road.

Lakini pia ili kuboresha na kupendezesha mji nashauri barabara hiyo iwekewe taa za barabarani isiachwe gizani kwa kufanya hivyo itabadilisha mandhari ya Jiji.

Nashauri pia ni vyema Waziri wa Ujenzi, Waziri wa TAMISEMI na Mkuu wa mkoa wa DSM wafuatilie mradi huo kwa karibu na kutatua changamoto mapema kuliko kusubiria.

Nawasilisha.
 

Kambaku

JF-Expert Member
Nov 12, 2011
4,219
2,000
Sasa iitwe hiyo ya njia 8 tu au yote hadi Morogoro?

Ila dah, kubadili jina kongwe kama Morogoro Road sidhani kama ni sawa mkuu. Atafutiwe barabara nyingine mpya iitwe kwa jina lake. Kuna ile moja inaanzia karibu na Kibaha inakuja kutokea pale Vikawe (Baobab sekondari) ni mpya ile mi nashauri apewe ile 🤷‍♂️🤷‍♂️🤷‍♂️
 

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
3,845
2,000
Sasa nasema hivi mtake msitake kwa Heshima ya Hayati JPM kwa kazi aliyo ifanya kwa kuubadilisha Mkoa wa DSM Barabara hiyo itaitwa BARABARA YA MAGUFULI na sio Morogoro road.
wenye kukereka wapitie njia nyingine lkn lazima mtakanyaga tu Magufuli road,
 

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
3,845
2,000
Sasa iitwe hiyo ya njia 8 tu au yote hadi Morogoro?

Ila dah, kubadili jina kongwe kama Morogoro Road sidhani kama ni sawa mkuu. Atafutiwe barabara nyingine mpya iitwe kwa jina lake. Kuna ile moja inaanzia karibu na Kibaha inakuja kutokea pale Vikawe (Baobab sekondari) ni mpya ile mi nashauri apewe ile
Mabadiko yatafanyika kwa Morogoro road yote, kwa maana inapo anzia mpaka inapo ishia, hiyo ndio itakuwa Magufuli road.
 

maroon7

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
9,394
2,000
Na hii ya kutoka Mwenge hadi Morocco ambayo itaifanya Dar kama Ulaya ipewe jina lake
 

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
3,845
2,000
Na hii ya kutoka mwenge hadi morocco ambayo itaifanya dar kama ulaya ipewe jina lake
hii njia kuanzia kimara mwisho hadi maeneo ya kibaha ni njia yenye hadhi ya barabara zenye viwango vya miji ya kimataifa.

ni lango la Jiji la DSM, ni taswira ya Jiji la DSM. ukiangalia Mafuli bus Terminal sio mchezo.
Hakika Hayati Maguli alibadilisha kabisa taswira ya JiJi la DSM.
bado natetea hoja yangu kuwa barabara hiyo ipewe jina lake kwa heshima ya kazi yake.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom