Napendekeza Alfonce Mawazo apewe Unaibu Katibu Mkuu CHADEMA

DALLAI LAMA

JF-Expert Member
Jan 31, 2012
8,651
2,627
Wanajamvi

Naomba kwanza nieleweke kuwa sina ukaribu wowote na kamanda Alfonce Mawazo zaidi ya kuifahamu vyema kazi anayoifanyia chadema kanda ya ziwa.

Kamanda Mawazo aliachana na kazi yake mkoani Arusha na kuhamia alipozaliwa kanda ya ziwa kuyasulubisha magamba na binafsi nimemfuatilia akikieneza chama ktk mikoa ya Mwanza,Kagera,Shinyanga,Simiyu na Mkoa wa Mara kwa usafiri wake binafsi.

Kamanda Mawazo aliachana na udiwani wa Sombetini kwa tiketi ya ccm na kuamua kueneza sumu dhidi ya chama chake cha zamani ccm.

Kazi anayoifanya kanda ya ziwa ni zaidi hata ya mbunge anayetoka kanda hiyo na amekuwa mahiri wa kujenga hoja hatua inayopelekea cdm kung'aa vijijini kanda ya ziwa.

Kijana huyu msomi toka busanda ana uwezo wa kulea chama kwa nafasi ya NAIBU KATIBU MKUU.
 
Mawazo anaganga njaa tu. Kazi ya siasa inalipa kuliko Kazi ya ualimu aliyokuwa anaifanya kabla.
 
Jambo jingine, hata hii thread ameanzisha mwenyewe jamani nyie wachaga muhurumieni mwenzenu naye apate ulaji njaa itamuua.
 
Jambo jingine, hata hii thread ameanzisha mwenyewe jamani nyie wachaga muhurumieni mwenzenu naye apate ulaji njaa itamuua.

mh.werema sina hata jina moja la mtu aliyeficha mabilioni uswiss..zitto
 
Alphonce Mawazo anafaa sana, ana uwezo mkubwa wa kujieleza na anakipenda chama chake, ningekuwa napiga kura ningempa yeye bila shaka
 
Politics si mchezo, hadi uchaguzi mkuu uishe chadema mwakani kuna majeruhi wengi tu wa kisiasa kama inavyokuwaga ccm. Na funga kazi itakuwa ni kwenye nominations za ubunge. Mungu tupe uhai kuona kitakachojiri.
 
anauwezo wa kuvumilia lang'ahi laini za magamba //mfn;-akiahidiwa mil 300 cash,na mjengo kinyerezi na mshahara wa 4.ml kwa mwezi kwa miaka 5 ijayo, hataweza kuiuza cdm yetu? nahitaji majibu fasta
 
Wanajamvi

Naomba kwanza nieleweke kuwa sina ukaribu wowote na kamanda Alfonce Mawazo zaidi ya kuifahamu vyema kazi anayoifanyia chadema kanda ya ziwa.

Kamanda Mawazo aliachana na kazi yake mkoani Arusha na kuhamia alipozaliwa kanda ya ziwa kuyasulubisha magamba na binafsi nimemfuatilia akikieneza chama ktk mikoa ya Mwanza,Kagera,Shinyanga,Simiyu na Mkoa wa Mara kwa usafiri wake binafsi.

Kamanda Mawazo aliachana na udiwani wa Sombetini kwa tiketi ya ccm na kuamua kueneza sumu dhidi ya chama chake cha zamani ccm.

Kazi anayoifanya kanda ya ziwa ni zaidi hata ya mbunge anayetoka kanda hiyo na amekuwa mahiri wa kujenga hoja hatua inayopelekea cdm kung'aa vijijini kanda ya ziwa.

Kijana huyu msomi toka busanda ana uwezo wa kulea chama kwa nafasi ya NAIBU KATIBU MKUU.

Ccm wewe unashauri kinafiki kwa taarifa yako nafasi hiyo tunarudisha kikofia tena awamu hii mwenye msimamo mkali
 
Mawazo anastahili kabisa, ana passion ya kweli ya chama na hawezi kuisaliti chadema, kama mtu aliweza kuacha ajira yake na cheo chake akaweza kuishi maisha magumu kwasababu ya Chama anastahili kupewa nafasi hiyo na ataitendea haki bila shaka yoyote!
 
Mawazo kiongozi wa chama??? akihama tena itakuwaje?? Huyu alikuwa TLP akaenda CCM then CDM huyu ana ugonjwa wa kuhamahama vyama
 
anauwezo wa kuvumilia lang'ahi laini za magamba //mfn;-akiahidiwa mil 300 cash,na mjengo kinyerezi na mshahara wa 4.ml kwa mwezi kwa miaka 5 ijayo, hataweza kuiuza cdm yetu? nahitaji majibu fasta

Inahitaji majibu? Kwa maswali yapi hayo? hapo naona zaidi una jaribu ku express Hisia zako juu ya jambo
 
mawazo huenda ametumwa na ccm tukimpa cheo mapema itatugharimu baadaye ushauri tusubiri mpaka muda ufike angalau hata mwaka 2014 ndo tumpe cheo...
 
Back
Top Bottom