MSATULAMBALI
Senior Member
- Apr 1, 2012
- 187
- 55
Enyi watu mliofungwa akili na pepo la CCM, je, hiyo CCM mnayoipigia debe imeiletea manufaa gani nchi hii kwa miaka zaidi ya 50 iliyokuwa madarakani, hasa mkizingatia wingi wa rasilimali (madini, gesi, mafuta, uranium, misitu, wanyama pori, ardhi nzuri, mito, maziwa, etc) tulizojaliwa katika nchi hii? Mnadhani kwamba bado CCM wanao uhalali wa kuendelea kubaki madarakani kwa mtaji wa umbumbumbu wa wapiga kura, hasa wa vijijini? Tutajieni mafanikio ya CCM ili tupate kuishabikia sio mnashabikia vyama kama mnavyoshabikia mpira (e.g Yanga & Simba).
Ushabiki wa kisiasa ni tofauti na ushabiki wa mpira. Ukishabikia timu mbovu (Yanga au Simba) hata ikishuka daraja hutapata hasara yoyote. Lakini ukishabikia chama cha mafisadi, kisha wakazidi kuifilisi nchi zaidi na kuitumbukiza nchi kwenye umaskini wa kutupwa, sio tu kwamba hautakuwa salama, lakini hata pia jamii yako yote itaangamia sawia. Kumbuka kwamba uchumi wa Tanzania miaka ya 60 ulikuwa sawa na wa nchi kama Malaysia, Thailand, Indonesia, Bangladesh na nchi nyingine nyingi za mashariki ya mbali na kati.
Kwa miaka zaidi ya 50 ambayo CCM imeongoza nchi hii, wamefanikiwa kuimasikinisha nchi hadi kushika nafasi ya 3 kwa umasikini duniani, mbele ya Afaghanstan na Somalia, nchi ambazo zimetopea kwenye vita kwa miaka mingi. Igekuwa hizo nchi hazimo kwenye vita, Tanzania ingekuwa ya kwanza kwa umaskini, pamoja na utajiri wa rasilimali tulizo nao. Je, mnaoshabikia CCM hayo ndiyo maendeleo mnayotambia? Kuweni nyie, msishabikie siasa kama mpira wa miguu. Nyie hamjui jinsi gani hizi siasa za kifisadi za CCM zilivyotufikisha hapa tulipo?
Tunawataka wanaCCM watuambie CCM na serikali yake wameifanyia nini nchi hii tangu waingie madarakani mwaka 1961, sio kutuimbia ngonjera ambazo hazina kiitikio. Kama mnataka kutuaminisha kwamba CCM ni chama cha wanyonge (wakulima na wafanyakazi) kama sera zake zinavyopambanua na kama alama zilizoko kwenye benedera ya chama zinavyoonyesha, mnapaswa kusimama hadharani mtuambie kuliko kuendelea kupayuka, kama vyura wa masika kwenye dimbwi la maji, bila kutoa ufafanuzi yakinifu. Itikadi ya chama inakataza wanaCCM kutopokea rushwa wala kujitajirisha kifisadi.
Ibukeni muitetee hiyo hoja kwa mifano hai na kwa umakini. Teteeni kwamba CCM SIO CHAMA CHA KIFISADI kwa sababu A, B, C, n.k. Sio mnajificha kwenye vichaka halafu mnaitupia mawe CHADEMA mkiwa mafichoni. Kwa kufanya hivyo mnadhihirisha kwamba ama hamjui sera ya chama chenu au hamjui malengo na sera ya chama chenu ni yapi. Mnajiendea tu kama jongoo; tena afadhali jongoo ana antennae/feelers zinazomsaidia kupambanua stimuli kwenye soroundings!