Napenda sana msichana wangu awe ananiomba hela

Nyetk

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
1,648
1,696
Shwari wakuu?

Inawezekana natofautiana kiasi kikubwa na wanaume wengi. Nafahamu wengi hawapendi usumbufu wa kuombwa ombwa vijisenti na wasichana. Mimi ni kinyume kabisa. Msichana kuniomba hela yani najisikia raha sana.

Kama una msichana alafu hakuombi hela na mzigo anakupa basi ujue wewe pengine ni wa kumi kwenye orodha yake. Yaani anakudharau au hajitambui na wapo anaowaamini zaidi yako ila kwako kipo anachofuata. Ndiyo maana mimi nikae muda mrefu msichana wangu hajaniomba hela walahi nampiga chini.

Ili mradi tu awe na jambo la maana la kuzifanyia kazi hizo hela, no problem.
“Kuna kiwanja au shamba nataka kununua”,
“Liko wapi?” Tunaenda naliona;
“Oh, zuri sana hili. Sasa?”
“Oo, mi ninazo kadhaa, nimepungukiwa millioni tatu tu!”
“Poa, hizi hapa.'' kumbe aende kwa nani?

Lakini siyo, “Oo, naomba laki tatu nikatie kucha rangi”, huyo namwambia “hujitambui wewe”. Mwanaume hela, mwanamke mapenzi bana. Au nasema uwongo wakuu?
 
Mtu asiye na hela ndiyo hupenda demu wake awe anamuomba hela!
Hawa wa siku hizi kama unapenda akuombe hela hautabaki na kitu kwenya salio!
 
Ss mkuu tugawie na humu mana watu tunashida na mitaji na hatujui tutaipata wap,hata kwa kutukopesha .

~Umetaja milion 3 duuuuh!!nimejikuta nawaza ni gunia ngap za mpunga huko bonden(kamsamba )na alizeti juu.

~Tusaidie musiwape mademu zenu tuu hata sisi dada zenu tupen.watu tunahangaika mitajianyie mnahonga.
 
Mtu asiye na hela ndiyo hupenda demu wake awe anamuomba hela!
Hawa wa siku hizi kama unapenda akuombe hela hautabaki na kitu kwenya salio!
Mwanaume kuwa huna hela mbona huo ni msiba?
 
Sifa za kijinga.
Sioni kama ni sifa za kijinga. Ndemu mkali siyo kitoto, anajiheshimu, ananipenda mpaka basi, nampenda, ananiheshimu, ana kazi yake nzuri tu ..... Sasa kuna tatizo gani kufanya sehemu ya maisha yangu? Na akipata shida asiponiomba hela mimi aende kwa nani?
 
Usingoje kuombwa a real man anatoa tuu kuombwa mambo ya kishamba sana kuna wengine kumwambia mwanamme naomba hela unahisi vibaya sana hasa mie,hata mume wangu simwambii naomba hela anajua majukumu yake,na hata Wanaume wanao jitambua hawasubiri kuombwa...
Mambo ya mume na mke ni tofauti hapo. Mi nazungumzia demu ambaye hatuishi bado kama mume na mke. Asiponiambia shida zake nitajuaje? Na asiponiomba nitakuwa na mashaka kuna mahali anaenda kuomba. Umenipata?
 
Back
Top Bottom